Tangazo toka Tume ya Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangazo toka Tume ya Uchaguzi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Lyangalo, Nov 22, 2010.

 1. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kuanzia sasa msishangae matokeo ya uchaguzi kupinduliwa.

  Kwanza, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.


  Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi kitaaluma

  Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
  Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
  Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
  Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john Chiligati
  Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana

  Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania

  Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."

  Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.
  Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.  Haya muwe mnaenda kupiga kura kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.  Nawasilisha;
  Mkurugenzi wa Tume,
  Rajab Kiravu.
  Nakala: Msajili wa Vyama vya Siasa - John Tendwa,
  Dk Slaa
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  MMMMH? hili bango ume copy wapi??
   
 3. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nimeipenda hii, pokea senks yako!
   
 4. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  nimeipenda hii iyagalo maana kwa mfumo kama huu inathibitisha jinsi jamaa asivyojiamini kwa unyenyekevu JWTZ, tutafika tu
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hapa ndo tunatakiwa tufumbue macho na tujue kuwa tunaongozwa kijeshi na demokrasia haitakuwepo kamwe!
   
 6. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo!
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sina cha kusemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona hii sio joke?
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wakuu huu ni uchochezi tuweni makini na tunayoyafanya humu mtakuja jutia nafsi zenu...........
   
 10. g

  geophysics JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Imeniingia akilini kabisa...kapteni, kanali n.k ndio mzee wetu anawasogeza karibu.... Subiri baraza la mawaziri utasikia...
  Good point... I like your post
   
 11. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #11
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tunaposema nchi kama Sudan na nchi nyingi za Afrika Magharibi zinatawaliwa kijeshi tunamaanisha nini ikiwa nyumbani hali iko hivi Mkuu hapo umenena kwa dhati kabisa
   
 12. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Sure japo kuwa joki
   
 13. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waana wa nchi....

  Hii ni hali mbaya wanayioweka CCM na kundi lake lote, lakini siku zote tukumbuke, Mungu anayajua haya yote na kusikiliza kilio cha watu wake kuliko Mwanadamu na nguvu yoyote ile.

  Tukumbuke nguvu za majeshi Binadamu hawa ni kama ZERO juu ya haki na kilio cha watu na taifa lao. ......Tafakarini, maguvu ya akina Goliathi, mfilisti aliangushwa na Daudi, kinda mdogo wa chini ya miaka 20! ....Jeshi kubwa la Ukomunist na Ukomunuist wenyewe viliangushwa hata pasipo fujo ya wananchi au hata vita ya mtutu! ......Ukuta Mkuu wa Hebron (uliokuwa unamilikiwa na Jeshi kubwa la Warumi) uluangushwa na waana wa Israel kwa kupaaza sauti tu (enzi hizo)!, .....Jeshi kubwa la Wamisri chini ya Pharaoh lilimalizikia baharini-Sham, pasipo hata mkono wa Wa-israel kuwapiga!. .....Jeshi hatari la Makaburu wa South Africa, likiwa linamiliki hadi silaha za Nyuklia, lili-collapse dhidi ya kilio cha Watu na taifa la baba na babu zao, waafrika halisi...sasa waliojiona kuwa ni class ya juu, wanatawaliwa na 'Wenye nchi' yao!!.....!!

  Kwa mantiki hii, inaonyesha kuwa CCM si kitu, si lolote ila wenyewe 'wanajilisha upepo' na kujifariji kuwa wanazo nguvu za dola, na mihimili ambayo wanaweza kuimiliki ili kupora haki za wananchi na taifa lote kuwa chini ya miguu yao??.....Kamwe! Tutayakumbuka maneno yasiyopote kamwe kuwa "HAKI HAIPOTEI ..ila INAWEZA TU KUCHELEWESHWA!"...ambalo ndilo wanalolifanya CCM dhidi ya Haki na ustawi wa Watanzania...HAKI ITATIMIA TU!

  Tutafakari kwa makini, na kuwa na Tumaini thabiti lisiloteterema, maana mwisho wao uu waja..........Nawasilisha!
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  uchochezi au ukweli?
   
 15. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  inauma eeeh kuuona ukweli!
   
 16. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nchi inaongozwa na wanajesh? Bwana..
   
 17. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,639
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280

  Kuna uchochezi gani hapo? wala sio joke hii ni ukweli ulio wazi:whoo:
   
Loading...