Tangazo toka jkt

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,057
309
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA
VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-
1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA
DIVISION I NA DIVISION II.
2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA
MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.
3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT
TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI
ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU
KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA
NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE
WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.
5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA
NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.
6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI
YA HAPA NCHINI.
Source:website ya jkt www.jkt.go.tz...kama utafungua kwa simu ikishafungua nenda desktop site
 
si ajabu hata mikopo wakanyimwa.

hii system yakwenda jkt naona ni upuuzi tu manake haohao walienda jeshi wakienda chuo wanakosa mkopo....mimi naona pesa inayotumika kwenda kurukisha kichura watu na kuwafanyisha mazoezi wangei-invest kwenye elimu kwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu
 
Ntajuaje kambi niliyopangiwa au nilipoti kambi yeyote ntakayoamua maana mi bado sijalielewa hili TANGAZO!
 
Usishtuke kwani ni haliya kawaida kwa serikalikuwatenga wanafunzi WA arts.mfano,fedha za capitation mashuleni,vita u vinavyotakiwa kununuliwa nivya sayansi tu na siyo arts.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom