TANGAZO: Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Muhimbili inasikitika kutangaza taarifa ya kupotea kwa Mwanafunzi wa Udaktari wa Kinywa na Meno(mwaka wa 4)

Dx and Rx

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,303
3,085
HABARI KWA WANAMUHASSO

Mwanafunzi mwenzetu Kelvin Mremi wa Kozi ya Udaktari wa Kinywa na meno mwaka wa nne, anahofiwa kupotea.

Bwana Mremi, alionekana mara ya mwisho, siku ya jumatano (6/03/2019), katika makazi yake huko Kariakoo. Kwa muujibu wa wapangaji wenzake ambao pia ni wanafunzi wenzake, Kevin aliondoka nyumbani siku hio mchana, na hakurudi, wala kuonekana tena.

Vivyo hivyo, hali ya sintofahamu iliongezeka pale, Bw. Kelvin alipokosekana kwenye mtihani ulio fanyika siku ya Alhamisi(07/03/2019) saa nane mchana, huku simu yake ikiwa haipatikani.

Juhudi za kutafuta taarifa za uwepo wake kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki zimegonga mwamba mpaka sasa.

Tunaomba, mwenye taarifa yoyote juu ya mahali alipokuwa Bw. Kelvin Mremi, atoe taarifa haraka iwezekanavyo kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi MUHASSO

0765773224,0789650088,0763749381,0754231027
IMG_20190308_154544_761.jpeg
IMG_20190308_154435_941.jpeg
 
...................unexamined mind is never worth living......."mekuta fb mtu kapost kwenye account yenye jina la mfanano Kelvin Thomas
 
Kumradhi:

Kuna makosa ya kutype tarehe kwenye maelezo ya tangazo la picha

Ni tarehe 6/3/2019 badala ya tarehe 6/3/2018
 
Back
Top Bottom