Tangazo Maalum: Kwa Wana JF Tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangazo Maalum: Kwa Wana JF Tu!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by W. J. Malecela, Apr 12, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Ninapenda kuwaarifu ndugu zangu wote hapa JF, kwamba kwa furaha kubwa sana mimi na ndugu zangu tuko katika matayarisho makubwa sana ya kumfanyia sherehe nzito sana mzazi baba yetu, siku ya Jumamosi ijayo ikiwa ni kwa ajili ya siku ya kuzaliwa kwake, tarehe 19, April miaka 75 iliyopita. Sherehe hizi tutazifanya rasmi siku ya Jumamosi ijayo tarehe 18, April nyumbani Sea View. Siku hiyo tutakua na shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kusaidiana kuboresha shughuli za nyumba mbali mbali za watoto wa yatima, mjini Dar.

  - Nimewaomba ndugu zangu kunipatia nafasi chache kwa ajili ya wanachama wenzangu kutoka katika jamii hii ya Jamii Forums au JF, walioko Dar na popote pale duniani ambao wangependa kushiriki nasi katika kusherehekea maisha ya mzazi wetu. Kwa wale ambao ni members wa hii forums na wangependa kushiriki nasi ninawaomba kwamba tuwasiliane kupitia PM ya hii forums ili niweze kuwa-include katika list ya wageni waalikwa, kwa vile ushiriki wa hii sherehe ni kwa wageni waalikwa only na hii kutokana na uwezo wetu mdogo wa kifedha ambazo tumechangishana sisi wanandugu.

  - We are so excited na grateful kwa Mwenyezi Mungu kwa mzazi wetu kufikisha miaka 75, hasa tukiangalia safari yake ndefu sana kimaisha iliyoanzia na kelelewa na a single Mom baada ya baba yake, yaani babu yetu Mzee Yohana (John), kufariki wakati mzazi wetu akiwa na miaka 5 tu, kule kijijini kwetu Mvumi, safari ambayo mpaka leo bado inaendelea na tunamuombea Mungu amuongezee zaidi.

  - Again kwa wale wote members wa hii forums ambao wangependa kushiriki nasi ninawaomba tuwasiliane haraka kupitia PM ya hii forums, nitapatikana kwenye namba zangu za simu kuanzia Jumanne kwa sasa niko safarini na nina a very limited access ya mtandao na simu, ingawa unaweza kuniachia message na nitarudisha simu yako au ujumbe wako maramoja na hii ni kwa members wote wa hii JF-Makini bila kumbagua yoyote yule.

  Ahsanteni Ndugu Zangu Wote Wana-JF, na Pasaka Njema.

  William.
   
 2. Moderator

  Moderator Content Quality Controller Staff Member

  #2
  Apr 12, 2009
  Joined: Nov 29, 2006
  Messages: 479
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Utakuwepo mkuu? Kama upo basi count me in. Kama kuna mchango tufahamishane kwa PM
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  shukran
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Count me in Mkuu, it will be nice kujikumbusha enzi zetu Mkuu huku tukimuezi mzee wetu kwa kushirki shughuli nzima
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unaweza kutoa ratiba itakuwaje? Mambo ya unywaji? unaweza niPM ili nijikomit sisi wengine kama alcohol hamna hatutokei! Happy Easter
   
 6. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Asante kwa mualiko tunamuombea Mungu amzidishie na mika mingine 75 itakayokuwa yenye furaha zaidi
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Asante Mzee, tutajumuika.
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mungu amjalie Baba kwa umri huo. Nawatakia maandalizi mema ya party.
   
 9. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #9
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Shukrani wakuu, ratiba ni kwamba shughuli itaanza siku ya Jumamosi nakuishia Jumapili, Jumamosi itakuwa ni kanisani na watoto wa yatima, na Jumapili kuanzia jioni mpaka asubuhi itakuwa mambo yote kuanzia chakula mpaka muziki na hotuba mbali mbali kwani viognozi wote wakuu wataifa wa CCM na Upinzani watakuwepo,

  - Naomba kuwakumbusha wale ndugu zangu wenye ambitions za siasa hapa ndipo mahali muhimu sana pa kuanzia katika kukutana na wanasiasa, nimepatiwa nafasi 4 tu kwa ajili ya JF tu, kwa sababu wengine wote watakuwa ni wanasiasa tu, kwa hiyo in the way ni nafasi nzito na muhimu sana kwa wanaoelewa vizuri.

  Ahsanteni.

  William.
   
 10. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyo baba yetu anaitwa nani?

  Ninaweza kubahatisha kuwa atakuwa anaitwa Malecela. Malecela yupi?

  Huwezi kutoa mwaliko wa sherehe ya baba yako bila kutaja wewe ni mtoto wa nani.
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Nitakuwepo kuanzia jioni J2 mpaka asubuhi.....hata nafasi zikijaa nitazamia...
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mazee si lazima uende, jitahidi kuwa na heshima na punguza masihara kwenye mambo ya msingi! unakuwa kama Abdi wa St Louis! Ebo

   
 13. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  teh teh hilo kubwa. No kilaji No turnup
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Hata na wewe unakaribishwa sana mkuu, hatubagui mtu maana naona kama unajishuku shuku hivi, usiwe na wasi wasi karibu sana mkuu.

  William.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  W.J.Malecela,
  natanguliza shukran zangu kwa mwaliko pamoja na kwamba najua sijaweza kufika.. Duh! ingekuwa bomba kichizi yaani nawakumbuka woote tulokuwa pamoja enzi zile kuwepo hapo basi hata nguvu sina..
  Hata hivyo, tunamshukuru sana mzee Malecela kwa kulitumikia Taifa kwa moyo mmoja tena naweza kusema ni kati ya viongozi wachache waliokuwa na Uzalendo kwa nchi yao..
  Mwenyezi Mungu amjalie kwa kila la kheri...
   
 16. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Nami nakushukuru kwa mwaliko huo kwani ni wachache ambao wanaweza kuwashirikisha katika masuala ya familia, huu ni upendo mkuu. Nawatakia heri na kumuombea Baba yetu Mungu amwongezee uzima.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi tatizo langu litakuwa hapo kwenye utambulisho. Nadhani baada ya hiyo sherehe tutafanya kile ambacho watu wanaita "to break the codes". Itabidi mods akubali sasa watu tubadili majina au ndo tutakuwa tumebatizwa upya kwenye jamii. Kwamba mimi nimebadili jina kwa sababu ya JF na sasa naitwa DC!! Mhhh ipo kazi hapo. Nadhani baada ya hiyo party sitaandika tena kama DC! Hata hivyo nafurahi sana kwamba members wengi humu ndani tunafahamiana sana. Long live JF.
   
 18. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Safisana tunamtakia mzee maisha marefu, Na mafanikio mema katika sherehe pia kwakuwakumbuka yatima.

  Mbarikiwe kwa moyo wa upendo.
   
 19. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Unatumia jina lako halisi...akija kukutafuta uku hakupata kamwe..kwa kuwa unatumia Nick name.
  Mzee location ya nyumba ni wapi...kwani seaview ni ni kubwa....na kuanza kuuliza uliza...kwa mzee malecela ni wapi wengine si hobby..tupe coordnates.....
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kadi ya mwaliko itaandikwa jina lipi? Naona JF inapiga hatua. Naona next time RA na maswahiba wake watatupiga bonge la offer kwenda kutesa Kempsky!! Naona pazia litafunguliwa na hapo itakuwa shughuli kweli kweli!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...