Tangazo la Waziri Ummy Mwalimu juu ya Coronavirus (COVID-19) lirekebishwe kukidhi mazingira yetu

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,465
Tangazo ni zuri na linatoa taadhari kitaalam, lakini kuna baadhi ya mazoea ya baadhi ya watanzania ambayo yaweza kuzidisha COVID-19 kusambaa yanakosekana. Wana-sosiolojia walitakiwa kushirikishwa katika kuandaa hilo tangazo.

Mfano, kuna lile kundi la vijana wavuta sigara kugoneana sigara wanapovuta. Sigara moja inavutwa na wastani wa watu wawili mpaka watano.

Pia kuna baadhi ya watu wanatema mate na makohozi barabarani au njiani au chini ovyo ovyo tu. Kiustaarabu, mtu anatakiwa kufikia makohozi au mate; hivyo anapaswa kuangalia na sehemu anayotemea - sehemu sahihi ni yenye mchanga. Kama kuna huduma ya bafu, basi lazima afanye hivyo kwenye bafu au choo.

Bila kusahau wachokonoa pua.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom