bluetooth23
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 348
- 324
Sisi wana Kigoma hatujui mwakilishi wetu amepotelea wapi, juhud zetu za kumtafuta zimegonga mwamba, namba za sim alizokuwa anatumia kwenye kampen hana tena ashazibadili, tumepata habari tu kuwa anapatikana sana maeneo ya Mikocheni dsm kwenye bar iitwayo Cruz Inn akiwa sana na Fred Lowassa, mara chache sana dodoma na monduli sijui anafanya nin kule. Ni miaka miwili hajaja kwetu huku, mara ya mwisho alikuja kumpokea raisi alipokuja huku na tunafikiri aliondoka naye, afadhali anayeonekana huku hata kidogo ni Zitto Kabwe mbunge wa jimbo jirani naye anapita tu akitokea Tanganyika Beach Hotel. Atakayetuonea mlengwa wetu ampe salamu kuwa tumemkumbuka sana na sura yake tumeanza kuisahau.