Tangazo la Vodacom la hapa kasi tu lina maana gani?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
Tunajua kuwa VODACOM ni kampuni ya kibiashara na haifungamani na upande wowote ule katika masuala ya kisiasa hata kama baadhi ya wamiliki/wenye hisa wake ni wafuasi wa vyama vya siasa.

Siku za hivi karibuni kampuni hiyo imezindua TANGAZO la kuhamasisha matumizi ya intaneti ya 4G iliyozinduliwa miezi michache iliyopita.

Maudhui ya TANGAZO yanachanganya maana hayaoneshi dhima iliyo nyooka. MPOKI ambaye ametumika kufikisha ujumbe wa 4G amefanya madoido yanayo ashiria mamlaka ya kisiasa na siyo mamlaka ya kampuni.

Kwanza ameongea kwa kumuiga Mh. Magufuli (Raisi wa Tanzania kupitia CCM ), anaonekana akijibu swali la mwandishi wa habari aliye muuliza kwa niaba ya WANANCHI na siyo WATEJE WA VODACOM, Anatoa ahadi kama mwanasiasa na siyo muhusika mkuu wa kampuni ya VODACOM, Mwishoni Mwandishi anamalizia kwa kutumia slogani ya HAPA KASI TU ikinasibu ile ya Mh. Magufuli ya HAPA KAZI TU.

Kwa kuwa sehemu kubwa ya Tangazo imeonekana kukopi falisafa ya Mh.Magufuli(ambaye ni mwenyekiti mtarajiwa wa CCM)sitokuwa nimekosea kama nikisema yafuatayo juu ya Vodacom.

1. Kwamba Vodacom wanamkubali sana Mh. na falisafa zake.
2. Kwamba kwa kuwa Mh.ni mwenyekiti mtarajiwa wa CCM na wao wanamkubali sana na wanamuunga mkono basi Vodacom wako tayari kukiunga mkono pia chama atakacho kiongoza muda mfupi ujao.

3. Kwamba kwa misingi hiyo ya upendo wao kwa Mh.na chama chake ndo maana wakajikuta wanaongea kisiasa kana kwamba wanaongea na wanachama badala ya wateja wasio na chama.

4. Kwamba Vodacom wako tayari kutengana na watu/wateja ambao hawafuati fikra/falsafa za Mh.

Yapo mengi sana ila itoshe kuwambia Vodacom kwamba wametukwaza sana sisi tusiozikubali falisafa za huyu wanaye muonesha akiongea na wananchi badala ya wateja.

Sisi wateja wa Vodacom tusio penda matangazo ya biashara yenye chembe chembe za kisiasa tunatoa siku mbili tusilione hilo tangazo tena mpaka hapo watakapo libadilisha vinginevyo kama wakikaidi tutasusia kutumia mtandao wao milele. Tutawahamasisha na Wengine ili waone namna siasa inavyojipenyeza kila kona na mwisho wake ni hatari kwa mustakabali wetu kama Taifa.
 
Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,035
2,000
Tangazo ni kama maigizo tu kwani linaweza zunguka huku na kule bora tu mwisho wa siku wafikishe ujumbe wao, yapo matangazo ya sabuni yanoonyesha watu wakicheza mpira, yapo matangazo ya cement yakionyesha uvunjwaji wa nyumba kitu ambacho asilimia kubwa hufanywa na serikali, yapo matangazo yanayoonyesha ma dr. japo hawazungumzii taaluma hiyo nk.

Kuhusu kampuni kuwa itaonekana inamkubali Rais, hilo la kumkubali ni swala la kawaida maana duniani kote kampuni zinasajiliwa na serikali na kutii sheria na kumtambua Rais aliye madarakani......hakuna kampuni hata moja inayojipambanua kuwa ni ya upinzani.
 
stan

Senior Member
Apr 23, 2010
149
250
Hapa kazi tu ni slogan iliyoshinda urais kwa idadi kubwa ya watu wa mikoani 8 mil na ushee hiv, so wameona wa ichague kuwasilisha wazo lao. kwa kawaida marketing plan inabid i-identify target market, na wao wanawalenga hao zaid.
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,662
2,000
Tunajua kuwa VODACOM ni kampuni ya kibiashara na haifungamani na upande wowote ule katika masuala ya kisiasa hata kama baadhi ya wamiliki/wenye hisa wake ni wafuasi wa vyama vya siasa.

Siku za hivi karibuni kampuni hiyo imezindua TANGAZO la kuhamasisha matumizi ya intaneti ya 4G iliyozinduliwa miezi michache iliyopita.

Maudhui ya TANGAZO yanachanganya maana hayaoneshi dhima iliyo nyooka. MPOKI ambaye ametumika kufikisha ujumbe wa 4G amefanya madoido yanayo ashiria mamlaka ya kisiasa na siyo mamlaka ya kampuni.

Kwanza ameongea kwa kumuiga Mh. Magufuli (Raisi wa Tanzania kupitia CCM ), anaonekana akijibu swali la mwandishi wa habari aliye muuliza kwa niaba ya WANANCHI na siyo WATEJE WA VODACOM, Anatoa ahadi kama mwanasiasa na siyo muhusika mkuu wa kampuni ya VODACOM, Mwishoni Mwandishi anamalizia kwa kutumia slogani ya HAPA KASI TU ikinasibu ile ya Mh. Magufuli ya HAPA KAZI TU.

Kwa kuwa sehemu kubwa ya Tangazo imeonekana kukopi falisafa ya Mh.Magufuli(ambaye ni mwenyekiti mtarajiwa wa CCM)sitokuwa nimekosea kama nikisema yafuatayo juu ya Vodacom.

1. Kwamba Vodacom wanamkubali sana Mh. na falisafa zake.
2. Kwamba kwa kuwa Mh.ni mwenyekiti mtarajiwa wa CCM na wao wanamkubali sana na wanamuunga mkono basi Vodacom wako tayari kukiunga mkono pia chama atakacho kiongoza muda mfupi ujao.

3. Kwamba kwa misingi hiyo ya upendo wao kwa Mh.na chama chake ndo maana wakajikuta wanaongea kisiasa kana kwamba wanaongea na wanachama badala ya wateja wasio na chama.

4. Kwamba Vodacom wako tayari kutengana na watu/wateja ambao hawafuati fikra/falsafa za Mh.

Yapo mengi sana ila itoshe kuwambia Vodacom kwamba wametukwaza sana sisi tusiozikubali falisafa za huyu wanaye muonesha akiongea na wananchi badala ya wateja.

Sisi wateja wa Vodacom tusio penda matangazo ya biashara yenye chembe chembe za kisiasa tunatoa siku mbili tusilione hilo tangazo tena mpaka hapo watakapo libadilisha vinginevyo kama wakikaidi tutasusia kutumia mtandao wao milele. Tutawahamasisha na Wengine ili waone namna siasa inavyojipenyeza kila kona na mwisho wake ni hatari kwa mustakabali wetu kama Taifa.
Chunga sana! Huyo Mpoki anaweza kuwa mkuu wako wa wilaya!
 
Naren

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
694
500
Hao wafanyabiashara huwa wanatafuta kauli mbinu itakayozoeleka faster kwa wananchi ili tangazo lao lipendwe au lizoeleke haraka nadhani kwa sababu magu kafunika na kauli yake ya kazi tu wameona nao watokee humo humo
Exactly.
 
Naren

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
694
500
Tangazo ni kama maigizo tu kwani linaweza zunguka huku na kule bora tu mwisho wa siku wafikishe ujumbe wao, yapo matangazo ya sabuni yanoonyesha watu wakicheza mpira, yapo matangazo ya cement yakionyesha uvunjwaji wa nyumba kitu ambacho asilimia kubwa hufanywa na serikali, yapo matangazo yanayoonyesha ma dr. japo hawazungumzii taaluma hiyo nk.

Kuhusu kampuni kuwa itaonekana inamkubali Rais, hilo la kumkubali ni swala la kawaida maana duniani kote kampuni zinasajiliwa na serikali na kutii sheria na kumtambua Rais aliye madarakani......hakuna kampuni hata moja inayojipambanua kuwa ni ya upinzani.
Nimecheka ulivyoongelea matangazo ya cement.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom