Tangazo la tuwapishe Wazee wapate Huduma za kijamii Kwanza liboreshwe ili lisilete mkanganyiko na migogoro Kwa watu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,030
50,932
TANGAZO LA TUWAPISHE WAZEE WAHUDIMIWE KWANZA LIFANYIWE MABORESHO ILI LISILETE MIGOGOGORO

Anaandika Robert Heriel.

Jana nilikuwa moja ya Hospitali za hapa Jijini DSM, nikakuta tangazo limeandikwa MPISHE MZEE AHUDUMIWE KWANZA" Sasa nikawa najiuliza Hapa Mzee anayezungumziwa ni mtu wa Aina gani.

Je, ni uzee wa umri?
Je, ni uzee wa rika?
Je, ni Mzee kutokana na Cheo au pesa au wadhfa?

Au ni Mzee mwenye connection ya wahudumu wa Hospitalini ambao wao hupita moja Kwa moja?

Sio kwamba nilikuwa sielewi TANGAZO, Hasha! Nilikuwa nalielewa kuwa huenda lilikuwa linamaanisha Mzee wa umri na naamini watu wengi wanafikiri Kama Mimi.

Foleni yangu ilipofika ya kuchukua Kadi ili nikamuone Daktari, nikamuuliza Yule mtu wa mapokezi; hivi hili tangazo linazungumzia Mzee wa namna gani?

Akanijibu: wewe hujui Mzee?
Nikamjibu: Simjui. Maana mmeandika tuu mpishe Mzee apate Huduma Kwanza.

Akasema akiwa kakereka, Mzee mtu mzima mwenye umri mkubwa.
Nikamuuliza umri mkubwa unaanzia miaka mingapi? Akaniambia Kwa hasira wewe hujui umri Mkubwa,
Wengine wakaanza kuniandama pale, lakini hawakujua nini namaanisha.

Akanijibu Mzee mwenye umri kuanzia miaka 60 kuendelea,
Nikamwambia basi muwe mnaandika hapa ili msiwachanganye watu.
Sio kila mtu anajua uzee unaanzia miaka 60.

Nikampa mfano, Sisi kwetu mtu mwenye umri wa miaka 60-70 bado sio Mzee anaonekana ni mtu mzima mwenye nguvu, nikawapa mfano wa Babu na Bibi zangu ambao ukimkuta mwenye miaka 75 utadhani anamiaka 60.
Nikamwambia wengine wanamiaka 50 tuu na wanaoonekana Wazee wa miaka 70 huko.

Basi nikatoka hapo na mjadala huo ukaisha.

Tukaenda Kwa madaktari kila mmoja kadiri alivyopangiwa namba ya chumba cha Daktari cha kuingia.

Huko ndipo msala ulipotoka wa yaleyale niliyokuwa nawaambia.

Utaratibu ni kuwa mkifika kwenye foleni ya kuingia Chumba cha Daktari, mtasubiri mpaka Daktari atoke achukue hizo Kadi. Lakini Kwa vile muda ulikuwa umeenda huo utaratibu ulivunjika ikawa atakayewahi kuingia ndiye atakayehudumiwa😀😀 si unajua mida baada ya Lunch mahospitalini kulivyo,

Basi akaja mama mtu mzima hivi ambaye age yake Kwa makadirio ni miaka 55-60 hivi.

Akawa naye anasubiri Daktari akitoka agombee aingie. Sasa hawa wengine kumuona huyu Mama wakamheshimu pasipo kuambizana lakini Dada mmoja ambaye Kwa makadiro anaumri Kati ya 30-33 hivi yeye hakuelewa somo. Mlango unafunguka tuu ili atoke aliyekuwa anahudumiwa aingie mwingine, Yule Dada wakasukukana na Yule Mama mtu mzima, watu karibia wote wakapiga kelele wakimshutumu Yule Dada kuwa Hana adabu.

Wakamshtumu mpaka alipotoka Daktari naye akamshutumu.

Kama mnavyowajua Watanzania ni watu wakufuata mkumbo, dada wawatu akawa kimya Kwa aibu.

Mimi nikawanyamazisha, nikasema huyu Dada sio CHIZI, lazima atakuwa anasababu, aulizwe Kwa nini amefanya haya yote.

Yule Dada akajibu; yeye anajua Mzee ni Yule asiyejiweza na Yule anayetembea Kwa fimbo au Kwa msaada wa mtu. Akaongeza kuwa yeye anavyomuona Yule Mama sio Mzee.

Nikasema, si nilisema Kule mapokezi, nikamwambia Daktari ni Bora muandike kabisa Mzee mwenye umri kuanzia miaka mingapi.

Nikamuuliza Yule Mama kwani anamiaka mingapi, akajibu anamiaka 52. Watu wote wakawa wanatoa macho.

Nikamuuliza Daktari Mzee anaanzia miaka mingapi Kwa mujibu wa Serikali, akajibu miaka 60.

Nikawaambia huyu Dada Hakuwa na makosa yoyote, isipokuwa Tangazo halijajieleza vyema ili kuwafanya watu wote wajue, sio kila mtu kasoma Ajue kuwa Mzee ni mtu mwenye miaka 60.

Wengine hiyo miaka 60 ni mtu mzima kulingana na koo zao wanaishi miaka mpaka Mia moja. Wakati wengine koo zao kumfikisha miaka 70 tuu ni mbinde na wanakuwa wapo Hoi wamechoka Kama wanamiaka 100.

Kesi ikawa closed

Migogoro hii pia hujitokeza kwenye vyombo vya usafiri.

Tangazo hili pia naliona Kwenye Huduma za usafiri wa mwendokasi
Ati mtu akiwa na Mvi tuu ndio Mzee😀😀😀 wakati ukimkadiria hatoboi miaka 50.

Wito: TANGAZO likitolewa liwe specific lisiache maswali Kwa watu.

Ni Sawa na Tangazo la pombe au bia lingesema, HAIRUHUSIWI KUTUMIWA NA WATOTO WADOGO, lingezua mkanganyiko, kuwa mtoto mdogo ni Nani.

Lakini Kwa kusema mtu aliyechini ya miaka 18 TANGAZO linaeleweka moja Kwa moja.

Ni Yule Mzee asiye na Mvi!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom