Geeque
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 936
- 319
Lile tangazo la TTB linalorushwa CNN ni hili hapa unaweza kuliangalia kwa ku-click kwenye hiyo link.http://www.eastafricantube.com/media/1465/Tanzania_Tourist_Board_TV_Commercial/
Samahani Geeque,
Mimi nafuatilia sana CNN na mtazamaji mzuri lakini mbona sijawahi kuona tangazo hilo hata siku moja?
Je, isijekuwa ndio kama nilivyosema toka mwanzo kuwa matangazo yote ktk CNN hutegemea na nchi kwani kila nchi hununua habari za CNN sio matangazo yake. Mathlan hapa nilipo matangazo mengi kama sio yote yanahusu mashirika yanayofanya biashara hapa. Matangazo ya kuzitangaza nchi za nje ambayo nimewahi kuyaona ni South Korea na Jamaica tu.
Nitarudia kusema navyofahamu mimi kila shirika la urushaji vipindi vya TV hununua rights za vipindi vyake pekee lakini sio pamoja na matangazo kwani haya hufanyika locally nikiwa na maana CNN kwa wakazi wa NY na CNN Toronto zina vipindi sawasawa kwa wakati mmoja lakini matangazo yake hutofautina.Hata michezo ya Football ama Basket ball, huwa tunatofautiana matangazo hata kama sote tunatazama mechi moja ktk ESPN.
Naomba maelekezo zaidi kuhusu hili yawezekana bado zijapata ufafanuzi mzuri.
It makes the neighbour see red.