Tangazo La Tanesco Mwisho wa Kulipa Madeni na Katizo la Umeme tarehe 31 March ktk maeneo yafuatayo

Zanika

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,316
752
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA(TANESCO)

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEME - KIGAMBONI

Shirika la umeme nchini Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wote Wilaya ya Kigamboni kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya Ijumaa tarehe 31/03/2017 kuanzia saa 03:00 asubuhi mpaka saa 12:00jioni.

SABABU ZA KATIZO
Kubadilisha nguzo zilizooza, kuimarisha viunganishi vya umeme na kukata miti iliyopita kwenye njia ya msongo mkubwa wa umeme ya Kigamboni (33 KV Kigamboni feeder na 11 KV Ferry feeder).

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI ;
Kata za Vijibweni, Tungi, Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Kisarawe II, Somangila, Kimbiji, Pemba mnazi na Sehemu ya Kata ya Toangoma na maeneo ya jirani.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wote utakaojitokeza.

-Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU
 

Attachments

  • IMG-20170327-WA0006.jpg
    IMG-20170327-WA0006.jpg
    27.5 KB · Views: 59
Back
Top Bottom