THE GREAT CAMP
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 765
- 194
Hongereni kwa kazi wana JF wote. Leo nilikuwa nafuatilia Matangazo ya mpira Barclays Premier league kati ya Sunderland na West Brom kupitia Supersport channel. Kati ya vitu nilivyopendezwa navyo ni kuona Tangazo linalosomeka SELOUS GAME RESERVE IN TANZANIA; THE WORLD'S LAGEST GAME RESERVE.Tangazo hili lilikuwa linapita kwenye mbao za matangazo zilizo pembeni ya uwanja wa mpira wa timu ya Sunderland. Binafsi nawapongeza walioweza kupeleka tangazo hilo kimataifa. Naamini tuna mambo mengi ya kufanya ili kuitangaza tanzania yetu. Kama wenzangu mlishaliona tangazo hilo, je mna maoni gani kuhusu kuzitangaza rasilimali zetu kimataifa? Nawasilisha.