Tangazo la nafasi za kazi ofisi ya baraza la mapinduzi

NGOGO CHINAVACH

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
943
368
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi kwa ajili ya Ofisi ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Afisa Utafiti Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ‘Sayansi Jamii’ katika fani ya Utawala wa Umma au Uchumi au Sosholoji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na Uwezo na mbinu mbali mbali za kufanya tafiti za kijamii (social research)

2. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Dereva Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya udereva kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amepata Leseni ya Udereva iliyotolewa Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 02 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.

source: fullview :: President's Office - Labour and Public Service
 
Jamaa wanatubagua sana waTanganyika
Kaka ile ni SMZ (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar), na hii ya Muungano ni SMT(Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania),kwahiyo hiyo ya kwanza ni kwa ajili ya Wazanzibari na hii ya pili kwa ajili ya wadau wote wa Muungano,yaani wazanzibar na watanganyika(Watanzania Bara) hususan kwa zile Wizara za Muungano, na hata zisizo za Muungano kwasababu sifa ni Utanzania ambao Wazanzibari wanao kwakuwa sehemu ya Muungano, na si kila Mtanzania ni Mzanzibari(Watanganyika), that's what I know.
 
Muungano wa kipuuzi kabisa huu, halafu ccm walivyo wajinga wakiambiwa muungano wenye usawa wa serikali tatu wanatoka povu kama wamemeza sumu.... Poor all ccm
 
Apa ndo utaona umuhimu wa serikali 3. Maana nafasi za bara zikitoka sifa ni uwe mtanzania..na sio mtanganyika...udumu muungano.
 
Ubaguzi wa hali ya juu halafu kuna mtu atasema kuvunja watu wakitaka kuvunja muungano hewa
 
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi kwa ajili ya Ofisi ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Afisa Utafiti Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ‘Sayansi Jamii’ katika fani ya Utawala wa Umma au Uchumi au Sosholoji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na Uwezo na mbinu mbali mbali za kufanya tafiti za kijamii (social research)

2. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Dereva Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya udereva kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amepata Leseni ya Udereva iliyotolewa Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 02 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.

source: fullview :: President's Office - Labour and Public Service
Changu chetu chako chako mungano hoyeeee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom