Tangazo la Nafasi ya Kazi ya Ikulu: Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020-2025

Tangazo la Nafasi ya Kazi ya Ikulu: Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020-2025 (Updated: 06 May 2019 at 8.00 am)

View attachment 1089251

I. UTANGULIZI

Unafahamu kwamba 2020 kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini Tanzania?

Unaelewa kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake yote, unapaswa kugombea nafasi ya kisiasa kupitia chama cha siasa na sio vinginevyo?

Unajua kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini Tanzania hupitia hatua kuu mbili, yaani, kura za maoni ndani ya vyama na baadaye mchuano wa jukwaani kwa njia ya kampeni zinazofanyika kwa siku sabini?

Unakumbuka kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi (1977) hata CCM wanapaswa kuachana na mapokeo yasiyo na tija kwa Taifa, na badala yake, wakajielekeze katika kuendesha mchuano wa kura za maoni ndani ya chama kwa ajili ya kumtafuta mgombea Urais aliye na sifa za kutosha kila baada ya miaka mitano?

Wewe ni mwanamke au mwanamume ambaye ni raia wa Tanzania mwenye akili timamu, maono ya kitaifa, kiu ya haki na umri wa miaka 40 au zaidi ya kuzaliwa?

Umewahi kuwa na ndoto ya Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi wa Serikali ya Nchi huru?

Kama umejibu "ndiyo" kwa maswali haya yote, basi kuna yamkini kwamba, wewe unaweza kuwa Rais wa Tanzania kuanzia Novemba 2020.

Sifa za mwombaji, masharti, majukumu husika na utaratibu wa kuomba nafasi hiyo vinatajwa hapa chini.

Watanzania wote wenye nia hiyo wanakaribishwa kutuma maombi kulingana na maelekezo yanayofuata hapa chini.

II. HATI YA MADARAKA NA MAJUKUMU KATIKA NAFASI YA URAIS WA JMT

(1) Rais wa JMT atakuwa na majukumu makubwa matatu ya kikatiba, yaani Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali ya JMT, na Amiri Jeshi Mkuu.

(2) Katika kutekeleza majukumu yake kama MKUU WA NCHI, Rais wa JMT atakuwa na mamlaka na majukumu yafuatayo.

(a) kuenenda kama alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake;

(b) kusimama kama alama ya umoja na uhuru wa nchi pamoja na mamlaka yake.

(c) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;

(d) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;

(e) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;

(f) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote; na

(g) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuchukua kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(3) Katika kutekeleza majukumu yake kama KIONGOZI WA SERIKALI ya JMT, Rais wa JMT atakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara. Katika kutekeleza majukumu haya, Rais wa JMT atakuwa na mamlaka ya:

(a) kusimamia utekelezaji wa sheria zote halali zilizotungwa na Bunge;

(b) kusaini mikataba ya kimataifa;

(c) kusimamia utekelezaji wa maamuzi yaliyomo katika hukumu za kimahakama;

(d) kusababisha utengenezwaji na uboreshwaji na sera za JMT;

(e) kusimamia utekelezwaji wa sera za JMT;

(f) kusababisha kutengenezwa kwa bajeti ya nchi, kuhakikisha inawasilishwa Bungeni, kujadiliwa na kupitishwa;

(g) kusimamia utekelezwaji wa kwa bajeti ya nchi kwa mujibu wa maamuzi ya Bunge;

(h) kuteua watumishi wa umma wote;

(i) kuthibitisha miswada ya sheria iliyopitishwa na Bunge kwa kuisani ili igeuke kuwa sheria halali za JMT;

(j) kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma wote;

(k) kuigawanya JMT katika mikoa na wilaya kulingana na mahitaji wa nyakati husika;

(4) Rais wa JMT, atahakikisha kwamba Shughuli zote za utendaji za Serikali ya JMT zinatatekelezwa nay eye mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya JMT, ambao watatekeleza shughuli zote za utendaji za Serikali ya JMT kwa niaba ya Rais wa JMT.

(5) Rais wa JMT atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya JMT kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vipaumbele vya kitaifa vifuatavyo vinafukuziwa kwa kasi na ufanisi usiopungua 75% katika muhula husika wa uongozi, ambapo kila kipaumbele kinabeba asilimia za juu zilizoonyeshwa kwenye mabano:

(a) Sekta ya Afya kipengele cha Mama na Mtoto (2%);

(b) Sekta ya Afya kipengele cha Wazee, Walemavu, Yatima na Wajane (2%);

(c) Sekta ya Elimu kipengele cha Elimu ya Msingi (2%);

(d) Sekta ya Elimu kipengele cha Elimu ya Sekondari (2%);

(e) Sekta ya Elimu kipengele cha Elimu ya Juu (2%);

(f) Sekta ya Mazingira kipengele cha kipengele cha kukabiliana na Madhara ya Mabadiliko ya Tabianchi (2%);

(g) Sekta ya Mazingira kipengele cha kukabiliana na Chimbuko la Mabadiliko ya Tabianchi (2%);

(h) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru wa Habari na vyombo vya habari (2%);

(i) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru wa Kukusanyika hadharani au ukumbini (2%);

(j) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru dhidi ya utekwaji na uteswaji wa raia unaoweza kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia kinyume cha utaratibu wa kisheria (20%);

(k) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uchaguzi ulio huru, wazi na haki (2%);

(l) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Ujenzi wa Imani ya Jamii kupitia matukio muhimu ya kitaifa (2%);

(m) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Michezo, Sanaa na Burudani (2%);

(n) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru wa kuabudu (2%);

(o) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru wa Bunge (2%);

(p) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru wa Mahakama (2%);

(q) Sekta ya Uchumi kipengele cha Usafirishaji wa Anga (2%);

(r) Sekta ya Uchumi kipengele cha Usafirishaji wa Majini (2%);

(s) Sekta ya Uchumi kipengele cha Usafirishaji wa Barabara (2%);

(t) Sekta ya Uchumi kipengele cha Usafirishaji wa Reli na Bomba (2%);

(u) Sekta ya Uchumi kipengele cha Mawasiliano ya Simu na Intaneti (2%);

(v) Sekta ya Uchumi kipengele cha Kilimo (2%);

(w) Sekta ya Uchumi kipengele cha Ufugaji (2%);

(x) Sekta ya Uchumi kipengele cha Uvuvi (2%);

(y) Sekta ya Uchumi kipengele cha viwanda (2%);

(z) Sekta ya Uchumi kipengele cha Nishati (2%);

(aa) Sekta ya Jamii kipengele cha Maji (2%)

(ab) Sekta ya Jamii kipengele cha Ajira kwa Vijana na walemavu (2%);

(ac) Sekta ya jamii kipengele cha ujinsia, ndoa, familia na haki za wanawake (2%)

(ad) Sekta ya Usalama kipengele cha kulinda usalama wa mali za watu (2%);

(ae) Sekta ya Usalama kipengele cha kulinda uhai wa watu dhidi ya vifo holela kinyume cha sheria za nchi (20%); na

(af) Sekta ya Diplomasia kipengele cha Mahusiano ya Kimataifa (2%).

UFAFANUZI: Vipaumbele hivi 32, vinazingatia ukweli kwamba, haki ya kuwa huru dhidi ya kifo holela na kuishi kwa amani ni kikonyo cha haki nyingine zote. Marehemu hana haki hata moja, isipokuwa haki ya kuzikwa. Kwa hiyo, vipaumbele viwili vifuatavyo vinabeba 40% ya alama zote: "(j) Sekta ya Utawala Bora kipengele cha Uhuru dhidi ya utekwaji na uteswaji (20%)"; na "(ae) Sekta ya Usalama kipengele cha kulinda uhai wa watu (20%)."

(6) Rais wa JMT atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali katika utumishi wa Serikali ya JMT, kwa maana ya nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba ya nchi au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi unaofanywa na Rais wa JMT.

(7) Rais wa JMT atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi za Serikali katika utumishi wa Serikali ya JMT, kwa maana ya nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba ya nchi au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi unaofanywa na Rais wa JMT.

(8) Rais wa JMT atakuwa na madaraka ya kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya JMT.

(9) Rais wa JMT Rais atakuwa na hiari ya kufuata au kupuuzia ushauri wowote atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba ya nchi au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.

(10) Katika kutekeleza majukumu yake kama AMIRI JESHI MKUU, Rais wa JMT atakuwa na mamlaka yafuatayo:

(a) kutangaza kuwapo kwa vita kati ya JMT na nchi nyingine yoyote;

(b) kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa JMT,

(c) kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika hali ya hatari;

(d) kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu ataona yahitajika, ama ndani au nje ya Tanzania;

(e) kuwateua viongozi katika majeshi ya ulinzi ya JMT;

(f) kuwateua watu watakaojiunga na majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini wanajeshi;

(f) kuwateua wanajeshi watakaoongoza vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi;

(g) kumwamuru mwanajeshi yeyote asitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa na ambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi; na

(h) kupima na kutoa hukumu juu ya jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kwa kuonyesha kama ni halali au batilifu katika mipaka ya amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya nchi.

III. SIFA ZA KIKATIBA ZA MWOMBAJI WA NAFASI YA URAIS WA JMT

Mtu yeyote anayetaka kuomba kugombea nafasi ya Urais wa JMT atapaswa kuthibitisha, kwa kuambatanisha ushahidi, kwamba anazo sifa zifuatazo:

(1) ni raia wa kuzaliwa wa JMT kwa mujibu wa Sheria ya Uraia;

(2) ametimiza umri wa miaka arobaini;

(3) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(4) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge;

(5) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu awe hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

IV. UTARATIBU WA KUCHAGULIWA KATIKA NAFASI YA URAIS WA JMT

Mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Urais wa JMT atachaguliwa kwa kufuata utaratibu ufuatao:

(1) Mtangaza nia kutuma maombi kwenye email tzpresidency@gmail.com baada ya kusoma na uelewa maelekezo yote katika uzi huu na kisha kuambatanisha nakala ya wasifu inayoonyesha taarifa zifuatazo: majina yake kamili; jina la chama cha siasa anachotaka kimdhamini; tathmini yake ya serikali ya sasa kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa vilivyotajwa katika kipengele cha tano (5) kwenye Hati ya Majukumu ya Urais wa JMT hapa kwenye uzi huu; nakala ya cheti cha kuzaliwa; vyeti vya elimu rasmi aliyo nayo; na taarifa nyingine muhimu.

(2) Taasisi ya Mama Amon Limited (MAL) kukusanya maombi yote, kuyafomati vizuri bila kuyahariri, kuyachapisha upya kwenye Jukwaa la JamiiForums, na hatimaye kuwaalika wananchi kutoa maoni yao juu ya sifa za waombaji wote kupitia kitufe cha “Reply” katika uzi husika.

(3) Taasisi ya MAL kuyachuja mamobi yote, kulingana na maoni ya wananchi, na kubakiza waombaji kumi tu watakaokidhi vigezo vizuri zaidi kwa kila chama cha siasa kitakachokuwa kimetajwa na waombaji;

(3) Taasisi ya MAL Kuwasilisha majina kumi bora kwa Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa kwa ajili ya mchujo zaidi kwa mujibu wa vikao vya kikatiba ndani ya vyama vya siasa husika;

(4) Kuvunjwa kwa Bunge la JMT kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofuata.

(5) Baada ya Bunge kuvunjwa, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kuwasilisha kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi ya Makamu wa Rais.

(6) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na mtu hatakuwa amependekezwa kihalali isipokuwa tu kama kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

(7) Endapo itafika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu ambaye anapendekezwa kihalali, Tume itawasilisha

jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge.

(8) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(9) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

(10) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote.

(11) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

(12) Rais mteule wa JMT atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba.

(13) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi: (a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais; au (b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au (c) siku atakapojiuzulu; au (d) siku atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti mengine ya Katiba ya katiba ya nchi.

V. UKOMO WA MUDA WA URAIS WA JMT

Ukomo wa muda wa Urais wa JMT utazingatia miongozo ifuatayo:

(1) Kipindi kimoja cha Urais wa JMT ni miaka mitano tu;

(2) Hakuna Rais atakayetumikia mihula zaidi ya miwili hata kama ni kiongozi bora mithili ya malaika.

(3) Rais aliyetumikia muhula wa kwanza wa Urais wa JMT atakuwa na sifa ya kugombea katika muhula wa pili endapo katika muhula wa kwanza amefanikiwa kutekeleza majukumu yaliyotajwa katika Hati ya Majukumu ya Urais wa JMT hapo juu kwa wastani wa 75% au zaidi, ambapo “skimu ya uhakiki (marking scheme)” itakayotumika kupima kiwango cha ufanisi wake ni Hati ya Majukumu ya Urais wa JMT kama ilivyotajwa hapo awali katika uzi huu.

VI. MSHAHARA WA RAIS WA JMT

(1
) Rais wa JMT atalipwa mshahara na malipo mengineyo, na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, na kiinua mgongo, kadri itakavyoamuliwa na Bunge.

(2) Malipo yote ya Rais wa JMT yatatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya JMT.

(2) Malipo yote ya Rais wa JMT hayatapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya nchi.

VII. UTARATIBU WA KUPOKEZANA OFISI YA URAIS WA JMT

(1) Endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, shuhguli zake zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani: (a) Makamu wa Rais au, kama naye hayupo; basi (b) Spika wa Bunge au, kama naye hayupo; basi (c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya JMT.

(2) Endapo kiti cha Rais wa JMT kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.

VIII. KINGA DHIDI YA MASHATAKA

(1) Wakati wote Rais wa JMT atakapokuwa bado ameshika madaraka yake, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

(2) Wakati wote Rais wa JMT atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.

(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais wa JMT kutokana na kushitakiwa na kutiwa hatiani kupitia Bungeni, itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba.

IX. UKOMO WA MUDA WA KUTUMA MAOMBI

Kuna njia mbili za kutuma maombi.

Njia ya kwanza ni kutuma maombi kupitia email ifuatayo: tzpresidency@gmail.com.

Na njia ya pili ni kutumia kitufe cha "Reply" na kisha ku-attach CV yake kupitia uzi huu.

Maombi yote yatumwe kabla ya sikuku ya Saba Saba 2019.

Maombi yote yatakayotumwa baada ya siku hiyo hayatapokelewa na MAL wala kufanyiwa kazi.

Karibuni Watangaza nia wote.
Hii thread inatofauti gani na yale mabandiko yanayosema uza iphone ukalime matikiti.
Wanakuambia tikitiki moja ni 2000
Hekari kumi zinatoa matikiki 80,000
80,000 x 2,000= 160,000,000
.
Sasa nenda kalime utauona moto wake.
 
Hii thread inatofauti gani na yale mabandiko yanayosema uza iphone ukalime matikiti.
Wanakuambia tikitiki moja ni 2000
Hekari kumi zinatoa matikiki 80,000
80,000 x 2,000= 160,000,000
.Sasa nenda kalime utauona moto wake.
.
Tofauti ni kwamba

1. Tangazo la matikiti ni ubazazi (illusion), lakini tangazo hili hapa kuhusu kazi ya Ikulu ifikapo 2020 ni uhalisia (reality).

2. Tangazo la matikiti halina fungamano na Katiba ya nchi, lakini tangazo hili hapa linarejea Katiba ya nchi kifungu kwa kifungu.

3. Tangazo la matikiti maji sio elimu ya uraia, lakini tangazo hili hapa ni elimu ya uraia tosha.

4. Tangazo la matikiti maji sio elimu ya mpiga kura, lakini tangazo hili hapa ni elimu ya mpiga kura tosha.

Ni Watanzania wangapi wamewahi kuona Hati ya Majukumu ya Rais wa JMT katika sura ya tangazo hili ?

Huu ni ubunifu mpya wa kiuandishi.

Tafakari.
 
Duh.!
 
.
Owkey.

Lakini mie hapa sijamwandika vibaya.

Hawezi kunikasirikia.

Jambo muhimu atoe hesabu yake kulingana na marking scheme iliyopendekezwa.

Kama alama zitatosha sawa, zisipotosha akubali matokeo.

Tanzania ni kubwa kuliko Urais.
Hv huyo kiatu ni nani kwanza?
 
Nimoja ya style ambazo wafalme wazamani walitumia pale wanapotaka kuwajua maadui zao, au kama vile kibwetele alivyo kusanya wafuasi wake na kuwateketeza kwa moto.
THINK TWICE
 
Back
Top Bottom