Tangazo la mkutano mkuu wa CUF taifa (MMT)

Jamhuri ya Zanzibar

Senior Member
Jul 17, 2012
126
195
MKUUTANO MKUU WA CUF TAIFA (MMT)2014 LIVE!

TANGAZO!
Tunapenda kuwaarifu wanachama, wapenzi na watanzania wote kwa jumla waliopo ndani na nje ya nchi kwamba tutarusha matangazo ya moja kwa moja (live) ya kikao cha Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23/06/2014 hadi tarehe 27/06/2014 hapo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine MMT itamalizia mchakato wa uchaguzi wa ndani ya Chama kwa ngazi iliyobaki ya Taifa ambapo Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Chama, Makamo Mwenyekiti, Katibu Mkuu na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa watachaguliwa.

Viongozi mbali mbali wa chama na waasisi wa chama watahudhuria.

Wageni mbalimbali waalikwa kutoka katika serikali, vyama vya siasa na asasi za kiraia wanatarajiwa kuhudhuria.
Halkadhalika wajumbe wa Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar wanatarajiwa kuhudhuria. Kwa heshma ya kipekee pia anatarajiwa kuhudhuria aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na waliokuwa makamishana wa Tume hiyo.

Mgeni rasmi siku ya Ufunguzi anatarajiwa kuwa msajili wa vyma vya siasa nchini, Mheshimiwa Jaji Fransis Mutungi.
Usikose kufuatilia matangazo haya ili kukujuvya kinachoendelea kutokea MMT-CUF 2014.

Ni katika kupanga kikosi imara cha kuing'oa CCM madarakani 2015.

Matangazo yataanza saa 1:00 za asubuhi kwa saa za Afrika ya Mashariki siku ya Tarehe 23/06/2014.

Kama utakuwa na internet yenye nguvu basi pata matangazo ya sauti na picha hapa: www.ustream.tv/channel/mazruimedia

Kama kasi ya internet yako haitakuwa na nguvu basi pata matangazo ya sauti pekee hapa; www.ustream.tv/channel/karafuumedia

Tutakaokuwa tukikuletea matangazo hayo ni mimi Ahmed Omar na Mwenzangu Mwanahabari Hamed Mazrui.

KARIBUNI NYOTE MKUTANO MKUU WA CUF TAIFA 2014!


mazrui.jpg
 
Mnakiongozi msomi mzuri mh lipumba ila kashindwa kuwendeleza
Chama chenu na kukitanuwa au kukisambaza kwa wananchi hususani bara
Nawapongeza ila mjitasmini sana na kuweka mikutano mingi vijijini na mijini sio daresalama tu
 
"Hatutashirikiana na Chadema kwa sababu ya kauli za kuudhi dhidi ya CUF kama vile CUF CCM B, CUF waliberali, CUFimeolewa na CCM. Chadema wanatumia fursa ili kujipatia wafuasi Zanzibar" Seif Shariff Hamad
 
Ni njambo jema ila sasa muachane na ile tabia yenu ya kurusisha majina yalele utadhani chama cha Kifalme ni wa sasa wa Lipumba na mwenzake Sharifu kuwaachia kina Mtatiro uongozi pamoja mengi waliyoyafanya ni mda muafaka wa wao kupumzika na kubaki kuwa tu washauri
 
jitahidini sana, tv channel/radio channels wanataka mamilioni mengi

Kwakuwa tunayo TV Station ya Taifa (TBC), na kwakuwa hili ni jambo lenye maslahi kitaifa, na kwakuwa hawajiendeshi kibiashara (Shirika la Umma), na kwakuwa tunawachangia pesa Watz wote kwa kodi zetu, ingefaa wao ndio warushe live.
Mkuu, mliwapa taarifa wakakataa kurusha wakidai mamilioni kama ya kibiashara japokuwa nyie hamtangazi biashara hapo?
 
Fanyeni uchaguzi kuwapata viongozi watakaokitumikia chama kwa amani, uzalengo na watakaoleta tija kwa taifa na siyo kwa ajili ya kuing'oa CCM madakani, mkishaing'oa?
 
Kwakuwa tunayo TV Station ya Taifa (TBC), na kwakuwa hili ni jambo lenye maslahi kitaifa, na kwakuwa hawajiendeshi kibiashara (Shirika la Umma), na kwakuwa tunawachangia pesa Watz wote kwa kodi zetu, ingefaa wao ndio warushe live.
Mkuu, mliwapa taarifa wakakataa kurusha wakidai mamilioni kama ya kibiashara japokuwa nyie hamtangazi biashara hapo?

haujasomeka, inaonesha kama wewe na jamhuri ya zanzibar ni mtu mmoja vile!
 
Back
Top Bottom