Tangazo la Kutangaza Utalii la Royal Tour linatangazwa kuliko kuhamasisha watu wafanye kilichopo kwenye tangazo

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,448
19,472
Nimeona juhudi za Kutangaza nchi (Ni Vema na Haki) ila kuna hili Tangazo la Kutangaza Utalii la Royal Tour nimeona kama sasa linatangazwa na kupewa juhudi yaani ya kuangalia Filamu zaidi hata ya kuhamasisha watu wafanye / waangalie kile ambacho kinatangazwa kwenye hilo Tangazo.

Sio vibaya tufanye yote ila Juhudi kubwa zifanyike kutangaza Utalii na Sio kuhamasisha watu watazame Tangazo la huo Utalii wenyewe, badala ya kuwaambia kaangalia tulivyotangaza basi tuwatangazie / kuwaambia tunachotangaza.

Badala ya kuhusisha / na kuwa-connect kila Tom, Dick and Harry (Masanja, Rajabu na Ali) kwamba wamekuja sababu ya hii Tour tuwekeze zaidi kwenye kuwaambia watu waje...
 
How come hii heading imebadilika?

Je hili ina maana sawa na Heading niliyoweka?

"Kutangaza Tangazo la TANGAZO zaidi ya Tangazo lenyewe".

Hii ina maana kwamba badala ya kuwatangazia watu waende kuangalia Serengeti n.k. tunawaambia watu waende kuangalia / waangalie hii tamthiliya, tunasahau kwamba motive ni kuleta wataliii na sio kuonyesha acting skills.

In the end badala ya kuitangaza Tanzania tunamtangaza Huyo Producer na kuwaelekeza watu waende kuangalia series zake nyingine za Rwanda, Israel n.k.
 
Nimeona juhudi za Kutangaza nchi (Ni Vema na Haki) ila kuna hili Tangazo la Kutangaza Utalii la Royal Tour nimeona kama sasa linatangazwa na kupewa juhudi ...
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba.

Bunge zima linafanya Promo ya Royal Tour kwa mfumo au kauli ambazo pia zinawashushia viwango waheshimiwa wetu mbele ya jamii ya watu wenye uelewa wa mambo ya haya utalii nchini.

Wanalazimisha kuihusisha na kila mtalii anayeingia nchini kwa sasa.

Kinyume na uhalisia kwamba kuijua impact ya Royal Tour itabidi kusubiri mpaka mwaka kesho.

Bookings zote zinazotimizwa kwa sasa ni zile ambazo zilikwishafanyika tangu mwaka jana na kurudi nyuma.

Wabunge wanachangia as if watalii walikuwa hawaingii nchini kabisa.

Kwamba mama kaenda kuwaambia sasa njooni.
 
How come hii heading imebadilika ?

Je hili ina maana sawa na Heading niliyoweka ?

"Kutangaza Tangazo la TANGAZO zaidi ya Tangazo lenyewe"...

Hii ina maana kwamba badala ya kuwatangazia watu waende kuangalia Serengeti n.k. tunawaambia watu waende kuangalia / waangalie hii tamthiliya, tunasahau kwamba motive ni kuleta wataliii na sio kuonyesha acting skills.... In the end badala ya kuitangaza Tanzania tunamtangaza Huyo Producer na kuwaelekeza watu waende kuangalia series zake nyingine za Rwanda, Israel n.k.
Mambo ya aibu kabisa
 
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba.
Bunge zima linafanya Promo ya Royal Tour kwa mfumo au kauli ambazo pia zinawashushia viwango waheshimiwa wetu mbele ya jamii ya watu wenye uelewa wa mambo ya haya utalii nchini...
Na hio gharama ya kupoteza muda ingeweza kutumiwa vema kwa kujadili ni vipi tunaboresha hii Sekta..., Au kama vipi hii ndio njia sahihi basi tujikite kwenye kutengeneza thamtiliya... na sio kupeana kudos za kutengeneza tamthiliya
 
Kwani tangazo lenyewe linahamasisha nini?

Mbona una akili ndogo Sana mkuu?
Moja ongea na @Mods sababu ndio wamebadilisha heading.... heading yangu ilikuwa

"Kutangaza Tangazo la TANGAZO zaidi ya Tangazo lenyewe"...

Pili kama unaona motive ya Royal Tour ilikuwa ni Kupata views za Movie basi sawa ila kama motive ni kuongeza / kuwafahamisha watu kuhusu utalii ndio hivyo tena Tangazo la TANGAZO limepewa kipaumbele
 
Kwani tangazo lenyewe linahamasisha nini?

Mbona una akili ndogo Sana mkuu?
Wewe mwenye akili kubwa mbona hujui hata linahusisha nini?

Kwa nini huwa wapumbavu fulani mnajipa hatimiliki ya maoni ya wenzenu?

Acheni u-shwine wenu....hili ni jukwaa huru na kila mtu anatoa maoni kulingana na yeye anavyolotazama jambo.

Hatuwezi kuwaza jambo linalofanana kwa wakati mmoja na wote tukaliamulia kwa jibu moja ndugu.
 
Mimi najua ila namchalenge mtoa mada..

Hilo ni tangazo la kuvutia watalii sasa mtoa mada anahoji nini asichokielewa hasa? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220603-131704.png
    Screenshot_20220603-131704.png
    125.9 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220603-131727.png
    Screenshot_20220603-131727.png
    160.7 KB · Views: 8
Mimi najua ila namchalenge mtoa mada..

Hilo ni tangazo la kuvutia watalii sasa mtoa mada anahoji nini asichokielewa hasa? 👇
Kwahio tangazo la kuvutia utalii linatangazwa kuliko hata kutangaza huo utalii, kwamba angalia tangazo ili upate tangazo ?
 
Kwahio tangazo la kuvutia utalii linatangazwa kuliko hata kutangaza huo utalii, kwamba angalia tangazo ili upate tangazo ?
Hilo Tangazo Limeainisha vivutio ndani ya tangazo.

Harafu ile ni documentary sio tangazo per say.👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220601-150717.png
    Screenshot_20220601-150717.png
    139.3 KB · Views: 7
Filamu yenyewe haina chochote cha maana cha kutosha kuvutia mtu ambaye kweli alikuwa hajui, hivyo tunahamasishana kutazama filamu ili kuibeza na kukejeli English ya yule kiumbe.

Ni FUTUHIIII, ndiyoooo….. ni FUTUHI!!!!
 
Royal tour imeangukia pua, tunasubiri episode two na three ambazo bibi aliahidi….. ila kwa aibu hii hatorudia.
 
Hilo Tangazo Limeainisha vivutio ndani ya tangazo.

Harafu ile ni documentary sio tangazo per say.👇
Documentary ambayo motive yake ni kupata / kufanya nini ?

Okay well and good documentary imeshashutiwa na kupelekwa huko kwa walengwa ili waangalie tukirudi huku kwenye uzinduzi na kuhamasisha watu waangalie kilichofanyika kwenye hio unaona ina tija kuliko kuwaambia tu watu watembelee Kilimanjaro, Serengeti na Zanzibar ? Au unaona ni sawa tuendelee ku-invest hii scarce resource ya muda kuwaambia watu kuangalia hii kitu na sio direct to the point kuhusu hivi vivutio ?, Ukizingatia hii Sinema sio be it end all (sio hata theluthi) yaani nina uhakika huu mwaka hawa watawala wametaja neno Royal Tour zaidi ya neno Twiga, Serengeti au hata Kilimanjaro... Bora hata wangetumia huo muda kuelezea yule Nyati Zeruzeru...
 
Watanzania walio wengi hawawezi kutambua haya maigizo ya Royal Tour.

Tunapaswa kutambua utalii Tanzania una season tatu (3) kuu ambazo ni

1. High/peak season: July-October na December 20th-March 31th, watalii wanakua wengi katika hiyo miezi.

2. Mid season: June 1st-June 30th na November-December 20, watalii wastani.

3. Low season: April 1st-May 31st, watalii mmoja mmoja.

Sasa hii Roho tour kiuhalisia imefanyika kumkuza Mama kisiasa tu, impact yake ni ndogo sana kwenye secta ya utalii. Kazi kubwa ya kutangaza utalii wa Tanzania inafanywa na tour operators wenyewe. Na hata sasa booking zote za watalii kwa high season na mid season sio impact ya royal tour kabisa.

Nawashauri Serikali na Wizara ya Utalii acheni drama za kisiasa, fanyeni marketing zitakazoleta impact kwenye sekta. Hakuna asiyejua nini mnapaswa kufanya kukuza utalii wetu huko dunia.. kama hamjui kaeni na tour operators mbadilishane uzoefu na muwe na priorities.

Tanzania yetu inapaswa kua cheap and the best destination around the world na inawezekana.
 
Na hio gharama ya kupoteza muda ingeweza kutumiwa vema kwa kujadili ni vipi tunaboresha hii Sekta..., Au kama vipi hii ndio njia sahihi basi tujikite kwenye kutengeneza thamtiliya... na sio kupeana kudos za kutengeneza tamthiliya
Sukuma gang kugeuka wapinzani
 
Documentary ambayo motive yake ni kupata / kufanya nini ?

Okay well and good documentary imeshashutiwa na kupelekwa huko kwa walengwa ili waangalie tukirudi huku kwenye uzinduzi na kuhamasisha watu waangalie kilichofanyika kwenye hio unaona ina tija kuliko kuwaambia tu watu watembelee Kilimanjaro, Serengeti na Zanzibar ? Au unaona ni sawa tuendelee ku-invest hii scarce resource ya muda kuwaambia watu kuangalia hii kitu na sio direct to the point kuhusu hivi vivutio ?, Ukizingatia hii Sinema sio be it end all (sio hata theluthi) yaani nina uhakika huu mwaka hawa watawala wametaja neno Royal Tour zaidi ya neno Twiga, Serengeti au hata Kilimanjaro... Bora hata wangetumia huo muda kuelezea yule Nyati Zeruzeru...
Kwa mujibu wa Serikalini, documentary nyingine nyingi zitaandaliwa ,Hii ni awamu ya kwanza ime cover hayo maeneo..

Mwisho mbona nimekuwa na attach na matokeo yake Chanya ila hayo huyaoni au? Shida yako hasa ni Nini Kuhusu Royal tour?
 
Rudia kusoma tena heading ambayo mods walibadirisha...

Kutangaza Tangazo la TANGAZO kuliko hata Tangazo lenyewe...
 
Back
Top Bottom