Tangazo la kuitwa kwenye usaili: Tume ya Utumishi wa Mahakama. Usaili kuanza tarehe 20/11 - 07/12/2017

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
TANGAZO KWA UMMA

KUITWA KWENYE USAILI

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.Hivyo,

Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia wafuatao ambao waliomba nafasi za ajira za Hakimu Mkazi Daraja la II, Wasaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Makatibu Mahsusi Daraja la III, Maafisa TEHAMA Daraja la II, Walinzi, Madereva Daraja la II, na Wapokezi wafike kwenye usaili kwa tarehe zilizoonyeshwa hapo chini. Aidha,

  1. Usaili kwa ajili ya Hakimu Mkazi Daraja la II utafanyikia katika Chuo cha Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) kuanzia saa 2:00 Asubuhi kwa kila siku na tarehe iliyoonyeshwa hapo chini.
  2. Usaili kwa ajili ya nafasi za Wasaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Makatibu Mahsusi Daraja la III, Maafisa TEHAMA Daraja la II, Walinzi, Madereva Daraja la II, na Wapokezi utakaofanyika kwenye kumbi zilizoko ndani ya uwanja mpya wa Taifa (National Stadium) unaotazamana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Mambo ya kuzingatiwa na Wasailiwa wote;
  • Usaili utaanza saa 2.00 asubuhi kila siku.
  • Unatakiwa kuja na Vyeti Halisi (Original Certificates) kuanzia kidato cha nne, Sita, Stashahada, Shahada na cheti cha kuzaliwa. Watakaoshindwa kuleta nakala halisi za vyeti hivyo, hawatasailiwa.
  • ”Testimonials’’, ‘’Provisional Results’’, ‘”Statement of Results”, hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (Form iv and Form vi results slips) HAVITAKUBALIWA.

Kuona majina ya walioitwa kwenye Usaili wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Bofya HAPA
 

Attachments

  • Orodha ya walioitwa kwenye Usaili - Tume ya utumishi wa Mahakama.pdf
    558.5 KB · Views: 824
Back
Top Bottom