Alnadaby
JF-Expert Member
- Sep 28, 2006
- 505
- 41
Leo ndugu wananchi kuna kikao huko ahera kinachohudhuriwa na Mchonga,Kenyatta na Obote.Pia wapo Amin Dadah,Sheikh Karume na wana Afrika Mashariki mashuhuri wakisubiri habari za mgeni ambaye kwa bahati mbaya bado ni mimba lakini ameshakufa.Nyimbo za kumpokea zinasikika kila mahali.
"Karibu toto changa unayeitwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki.Tunaondoa hii misumari iliyoyokuchoma yenye label ya KIBAKI.Karibu Ahera!" Huu ndiyo wimbo unaopamba sherehe ya kumpokea mfu huyu.
Na huku duniani binadamu wapo Vibaka wanaodhani kuwa wao tu ndiyo wanaostahili kutawala wenzao.Wanatangaza uchaguzi kisha wanapika matokeo.Madhara yake wanarudisha nyuma kila lenye heri na kukaribisha shari.
Kuna mtu yeyote ambaye kwa sasa hivi ana tamaa ya kitu kama Shirikisho la kisiasa la Afrika ya Mashariki baada ya mtafaruku wa Kenya?