Tangazo la kazi za uhasibu na meneja wa ktc workers saccos limited

Abel Ndundulu

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
845
383
TANGAZO LA KAZI
KTC WORKERS SACCOS LTD
ni Chama Cha kuweka na kukopa cha Wafanyakazi wa Kampuni ya Chai Kagera na BK Tea Blender’s Ltd. KTC WORKERS SACCOS LTD inatangaza nafasi ya za kazi za MENEJA na MHASIBU wa Chama wenye sifa zifuatazo;
  • MENEJA WA CHAMA;
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe raia wa Tanzania;
  • Awe amehitimu Stashahada / Shahada ya Ushirika / Fedha / Biashara na Masoko kutoka chuo kinachotambuliwa na TCU;
  • Awe na ufahamu wa Utawala wa Chama cha Ushirika kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika;
  • Awe na uwezo /uzoefu wa kuongoza watu walio chini yake;
  • Awe na uwezo wa kujisimamia mwenyewe kwenye kazi zake;
  • Awe na uwezo wa kuunganisha Wafanyakazi wenzake na Wanachama katika chama;
  • Awe mwenye kujali Makubaliano /ahadi ‘Deadline”;
  • Awe mwenye weledi wa hali ya juu na awe na uwezo wa kubuni na kushauri masuala ya kukuza na kuendeleza chama;
  • Awe hofu ya MUNGU na mwenye kuishi vyema na jamii.

  • MAJUKUMU YA KAZI
  • Kuandaa na kutunza vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyingine muhimu za chamani;
  • Kupokea fedha yote inayolipwa chamani na kufanya malinganisho ya fedha iliyopokelewa na iliyolipwa kila siku;
  • Kufanya malipo yote baada ya kupata kibali cha bodi;
  • Kukusanya marejesho ya mikopo na faida ya chama;
  • Kufanya malinganisho ya hesabu ya benki kila mwaka;
  • Kuandaa taarifa ya kila mwezi ya hali ya fedha na takwimu zote;
  • Kuwapigia hesabu ya mkopo wanachama wanaokopa;
  • Kufuata masharti na kanuni za fedha na uandishi wa vitabu na Masharti ya Ushirika kwa Ujumla wake;
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na bodi.

  • MHASIBU WA CHAMA
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe amehitimu Astashahada / Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambuliwa na TCU;
  • Awe na uzoefu wa kazl za uhasibu usiopungua miaka mitatu;
  • Awe na ufahamu wa kufunga hesabu kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika;
  • Awe na uwezo wa kujisimamia mwenyewe kwenye kazi zake;
  • Awe mwenye kujali Makubaliano /ahadi ‘Deadline”;
  • Awe hofu ya MUNGU na mwenye kuishi vyema na jamii.

  • MAJUKUMU YA KAZI
  • Kuandaa taarifa za fedha za kila siku (akiba,hisa,Mikopo na baki la benki );
  • Kuhakikisha malipo na makusanyo yote yameingizwa kwenye mfumo wa Kimahesabu;
  • Kuhakikisha malipo kwa wateja yanalipwa kwa wakati na usahihi;
  • Kuandaa taarifa za mwezi ,robo kama atakavyoelekezwa na Meneja au Bodi;
  • Kufanya usuruhishi wa vitabu vya chama na taarifa za benki;
  • Kutunza mali za chama;
  • Kuandaa taarifa za kimahesabu za mwaka na kusimamia ukaguzi;
  • Kuishauri Bodi juu ya namna Sahihi ya Uwekezaji na hatari kwenye mifumo ya fedha;
  • Kiongozi wa idara ya Uhasibu wa chama na Mshauri Mkuu wa Meneja kwenye masuala ya fedha;
  • Atafanya kazi zingine kama atakavyoelekezwa na Meneja au Bodi.

  • MUHIMU
  • KTC WORKERS SACCOS LTD inatoa haki sawa za ajira bila kujali rangi,kabila wala jinsia.
  • Mshahara mzuri kwa atakayepata nafasi hizii utatolewa;
  • Maombi yapelelekwe kupitia anuani ifuatayo;

  • Anwani
  • Mwenyekiti wa Bodi,
    KTC WORKERS SACCOS LTD,
    SLP 462 BUKOBA - TANZANIA.
  • Baruapepe
  • kagerateacompanyltd@gmali.com / info@kageratea.com / drmgimba@gmail.com



  • Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15.12.2018.
 

Attachments

  • TANGAZO LA KAZI - KTC WORKERS SACCOS LTD.pdf
    1.3 MB · Views: 78
Hiyo miaka mitatu uzoefu ,inamaana mie uzoefu nitaanzia wapi kama wewe hutaki kuanza kwako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom