Tangazo la kazi ya huduma kwa wateja (customer care)

ELIMU PESA

Member
Jul 22, 2017
62
36
MWAMBA’S GROUP U MK

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

MWAMBA’S GROUP imesajiriwa katika kuendesha shuguli za kiuchumi na kijamii. Ilisajiriwa rasmi 17 Mwezi November, mwaka 2014 kwa namba ya Usajili MG/MMC/CBO/00044.

Katika kutimiza majukumu yake MWAMBA’S GROUP inatarajia kufungua ofisi itakayojihusisha na huduma ya pesa kwa njia ya mtandao - Morogoro. Hivyo basi MWAMBA’S inatafuta kujaza nafasi moja (1) ya Huduma kwa wateja (Customer care) mwenye uwezo na hali ya kufanya kazi.

1.O SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe amehitimu elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea

ii. Awe na uzoefu wa kufanya kazi ya huduma ya pesa kwa njia ya mdandao angalau miezi (3) mitatu na kuendelea

iii. Awe anajua kutumia computer vizuri (Microsoft Word, Excel na internet).

iv. Awe anaifahamu vizuri MWAMBA’S



1,1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuhudumia wateja wote kwa wakati katika kuwapa huduma ya pesa hususa kupitia M-PESA, TIGO – PESA, AIRTEL MONEY, CRDB NA NMB

ii. Kufunga mahesabu ya kila siku, wiki, mwezi na mwaka

iii. Kuhudumia wanachama wa MWAMBA’S

iv. Kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi ya MWAMBA’S

v. Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na msimamizi wa kazi.



1.2 MSHAHARA

MWAMBA’S inatoa mshahara zaidi ya kiwango cha kima cha chini kwa mjibu wa sheria ya Tanzania. Hivyo, kiwango halisi kitajadiliwa kipindi cha usahili (Negotiation).

1.3 MASHARTI YA JUMLA



i. Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18) na usiozidi miaka arobaini na tano (45) na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai, kufungwa jera au kufukuzwa kazi.

ii. Mwombaji awe anaishi au awe tayari kufanya kazi Morogoro

iii. Mwombaji aandike barua ya maombi na aambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu (3) wa kuaminika na wanaoijua MWAMBA’S lakini wasiwe mmoja wa wamiliki wa MWAMBA’S.

iv. Kwa hatua hii vyeti vya taaluma havihitajiki

v. Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 4.5.2018 Saa 12:00 jioni. Watakao tuma baada ya mda huo maombi yao hayatapokelewa.

vi. Watakao kidhi vigezo watapigiwa simu kwa hatua nyingine ndani ya wiki mbili baada ya kufunga maombi. Ukiona mda huo hujapigiwa simu utakuwa hujabahatika jaribu siku nyingine.



Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (e-mail): mwambasgroup@gmail.com

N.B Waombaji waliohitimu mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja wapo ya fani zifuatazo: Usimamizi wa fedha, Huduma kwa wateja, biashara, uhasibu, Utawala, Sheria, Maendeleo ya jamii na sanaa, elimu ya jamii na computer kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali wanasifa ya ziada.
 
Kwasababu Mmeweka Vigezo Vigumu,Kwa Hasira Nawadiss!....mdandao ndio nini??..Jera Ndio Nini?...imesajiriwa Ndio Nini??....hususa Ndio Nini??....kwa Mjibu Ndio Nini???...Mda Ndio Nini??..Afu Mlivyokuwa Mabwege Hapo Kwenye NB mmekopi Tangazo La Ajira la Halmashauri La Kuajiri Watendaji Wa Vijiji!!Pumbavu
 
Km unataka hadi mtu aijue hiyo kampuni, basi kulikua hakuna haja ya kutuma umu jf.
 
Hiyo ni kazi ya familia ya Mwamba's wameamua kushare na Jf....nadhan kuna mwanafamilia wa Mwamba anatafutwa aaply kazi ya wajomba, wanamhitaji ila hawana mawasiliano nao lakini wanajua anatumia Jf!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom