Tangazo La Dharura: Hali Mbaya Ya Mgonjwa, Mtanzania Mwenzetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangazo La Dharura: Hali Mbaya Ya Mgonjwa, Mtanzania Mwenzetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Jan 17, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakuu wote hapa na ndugu zangu, kwa masikitiko makubwa sana ninaomba kuwafahamisha up-todates, za mgonjwa ndugu yetu Sister Pendo Magaluda ambaye amekuwa akisumbuliwa sana na ugonjwa wa Breast Cancer, habari ambazo ziliwahi kutolewa huko nyuma kwenye chombo cha habari cha Brother Michuzi.

  - Since then, ndugu yetu mpendwa Sister Pendo, amekuwa akipata nafuu na kuzidiwa pia, lakini recently hali yake imekua sio nzuri sana kwa wale mnaofahamu vizuri madhara ya ugonjwa huu hatari ninaamini kuwa mnaelewa ninachokisema. Baada ya kutibiwa sana between USA, Tanzania, South Africa, na back tena to New York City, USA, Pendo alihamishiwa katika Hospitali ya kitongoji cha Rochester, yaani Up-Sate New York umbali wa maili 350 kutoka NYC.

  - Ninamfahamu Sister Pendo, na mumewe Abel na watoto wao wadogo watatu wa kiume, mkubwa mwenye umri wa miaka 11, anayemfuatia miaka 9 na mdogo mwenye miaka 4 na wote wa kiume, na hii familia nzima wako pamoja huko Hospitali Rochester. Betweeen kumhudumia mkewe na watoto katika hiki kipindi kigumu sana kifamilia, ndugu yangu Abel ilibidi aache kazi na ku-dedicate muda wake wote kumuuguza mkewe, ninamuombea nguvu zaidi na busara za Mwenyezi Mungu zimtangulie mbele ili asikate tamaa.

  - Sasa ndugu zangu kama kawaida yetu bina-adam, kusaidiana kwa hali na mali na hasa katika kipindi cha matatizo kama hiki kwa hawa ndugu zetu, ambao kwa kweli bado ni vijana sana in their 30s, ambao walikuwa huko US kwa ajili ya masomo na matibabu pia. Hivi ninapoandika nipo njiani nikielekea huko Rochester kwenda kuwaona na kutathmini kwa karibu hali halisi, ninawaomba tena ndugu zangu kwamba kwa yoyote mwenye kujaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa na uwezo wa msaada wa aina yoyote ile, kuwasaidia hawa ndugu zetu, unaweza kutuma kwenye:-

  -Checking Account # 526-410-230, benki ya HSBC, kwa kutumia majina ya Pendo au Abel Magaluda

  - Kwa yoyote mwenye maswali zaidi, tafadhali tuwasiliane kwenye PM, na pia kwa wale walioko karibu na huo mji wa Rochester, ndugu zetu wako kwenye Hospital ya Rochester University unaweza kuwapata kwenye namba ya simu 1-585-414-1481, kutokana na pilika pilika walizonazo, sio rahisi kuwapata kwa mara moja kwa hiyo tafadhali jaribu kuacha ujumbe ikibidi na watakujibu baadaye.

  Ninaomba kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote ambao wamekua wakiwasaidia ndugu zetu kwa muda sasa, na pia kwa wale wote walionipatia misaada mbali mbali mzito ya kuwafikishia huko ninakokwenda kuwaona, na ninategemea kuwepo nao huko kwa siku mbili zijazo, Mungu awabariki na awazidishie zaidi.

  Samahani sana wana-JF, na hasa Mods kwa kuiweka hapa hii ni kwa sababu tu ya udharura wa hali halisi, lakini mnaweza kuipeleka inapotakiwa ikibidi.

  FMES.
   
 2. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu kwa kuuguliwa na hao wapendwa wetu. Mwenyezi Mungu awajaze nguvu na neema zake mgonjwa apone haraka.

  Tuko pamoja katika sara zetu.

  Wengine tuko huku mbali mikoani lakini I hope wenye uwezo ambao wako karibu wanaweza kusaidia chochote.

  Once again poleni sana na Mungu mwenye rehema awape nguvu za kumuuguza dada yetu na amponye na huo ugonjwa.

  Masanja,
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Friends in need is a friend indeed. Hapa ndipo haswa ninapoipa heshima ya pekee JF. Member wa JF tunaungana na kuunganisha nguvu na sala zetu pamoja to wish Pendo a speedy recovery.

  Asante FMES, Tuko pamoja waiting for more update.
  BWANA akutangulie, na kusimamia uponyaji.
  Kwa YEYE, yote yanawezekana.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni maombi yangu kwa Molla mgonjwa apate ahueni na kurejea afya njema. Amina.

  SteveD.
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona siku hizi unapotea sana? zamani nilijua ni kwa sababu umeme unaleta shida huko Malampaka kama kwetu Kwimba..sasa mwenzangu naona siku hizi uko Mysore India..na huko kuna shida ya umeme? au ilikuwa ni pilika pilika za kuhama ;-)

  Anyway...Its good to see you once again....

  Weekend njema,

  Masanja
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  namuombea mgonwja apate nafuu na kupona haraka. familia ipate nguvu ya kuyashinda majaribu wanayokabiliana nayo kwa sasa-amen
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Shukrani wakuu kwa sala na salam, sasa hivi nipo Hospitali na mgonjwa tayari nimemuona baada ya ku-pick up gari NYC na kuendesha usiku kucha kuweza kufika hapa, kwa kweli hali kama nilkivyosema huko nyuma sio njema kabisa, again ninasema shukrani kwa sister kutoka Adis Ethiopia kwa msaada wako mzito wa dola $ 500 za US,

  - Pia natoa shukrani nzito kwa Mama Migiro, kwa msaada wako na ushirikiano mkubwa on this situation na ofisi yetu ya ubalozi wa New York, na hasa Sister Rose Mkapa, na wengine wote maofisa wa ubalozi wetu huu kwa misaada yenu mbali mbali, Mungu awabariki wote,

  NDUGU ZANGU KABLA HATUJAFA HATUJAUMBWA, JUST THINK ABOUT IT.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi Mungu awasaidie katika kipindi hiki kigumu kwa familia hiyo na pia ampe nafuu mgonjwa dhidi ya ugonjwa unaomkabili.
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu acheni kuyeyusha, mshapewa account namba hapo juu lakini mmeng'ang'ana na kumuombea kwa Mungu amsaidie! kinachotakiwa hapa ni hela, maombi yenu mnaweza kuyafanya kivyenuvyenu kimyakimya bila hata kuyaleta hapa.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jamani mnaweza kuweka paypal. Wengi tuna credit cards tu.
   
 11. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mtu akituma fedha au msaada wowote kwa mlengwa si lazima atangaze hapa. Nakushangaa Mkuu K-K-N kuweka ujumbe kama huu hapa. watu wanaweza toa pole na salamu hapa na si lazima waeleze wanafanya nini Behind The Scene.
   
 12. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Sijasema kuwa mtu akitoa mchango atangaze hapa, nilitegemea kuona kauli nyingi za "ntarekebisha kesho mkuu" au "angalio salio mkuu" na sio "Mungu amsaidie" kwa sana. FEMEs ametoa account namba hapa na ni wazi nini kinahitajika, wanaotaka kumtumia mgonjwa salamu watafute address ya hospitali wamtumie kadi, tuache longolongo jamani.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ndugu zangu Wa-Tanzania wenzangu wote kwa hapa sasa ni saa za jioni ni baridi isiyokua mfano, nipo nyumbani kwa familia ya mgonjwa sister wetu Pendo, after a very long day ndio kwanza tumemaliza kufanya shughuli za shopping kwa ajili ya familia hii kujitayarisha kurudi nyumbani next week kama itawezekana kutokana na kibali cha madakitari kwa ajili ya kuweza ku-board kwenye ndege, ninasema iwapo itawezekana maana inategemea majaliwa na Mungu.

  - Again hali ya mgonjwa sio nzuri na haina unafuu kabisaa, toka asubuhi imekua in and out between nyumbani na Hospitali, na hapa nipo na watoto wadogo watatu wa mgonjwa ambao kwa kweli kama mnavyojua malaika wa Mungu, hawana habari kabisa na kinachoendelea, wao wanachojali ni kukutana na watoto wangu na mchezo mpaka lyamba, lakini nimefarijika na mume wa mgonjwa kutokana na moyo wa ujasiri alionao na kuweza kukubali reality as it is. Na pi animefarijika na wana-JF walioitika mwito, again proud to be Mwana-JF, maana tupo kila mahali.

  - Again ahsante kwa kila kitu hasa misaada, ninaomba ndugu zangu tuzidishiwe na Mungu wetu wa maajabu ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu hawa wapendwa, shukrani kwa wote popote mlipo, sasa hivi ninarudi tena Hospitali kabla ya kuanza kujitayarisha na safari tena. Shukrani kwa wote na tuzidi kuwa na moyo wa upendo wa kusaidiana.

  Ahsanteni na Baadaye!
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Mkuu kwanza shukran kwa taarifa hii, nadhani tumewahi kuzungumza siku za nyuma..Itakuwa vizuri sana kama unaweza kufuatilia mawazo ya Zakumi...tupo pamoja katika kila la kheri..
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jan 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita nimepoteza ndugu watatu kwa tatizo la namna hiyo; kweli inakatisha tamaa sana kwa ndugu wa karibu wa mgonjwa hasa kwa vile mgonjwa mwenyewe anakuwa anapata maumivu makali sana yanayomfanya kuwa analalama muda mwingi na hivyo kuwafanya ndugu nao waumie sana

  Natoa pole sana kwa mgonjwa na wote waliokaribu naye kwa vile katika kipindi hiki wana wakati mgumu sana.

  FMES,

  Account ya Benki inasaidia tu kwa wale ammbao wanaweza kupata muda wa kukimbia kwenye benki zao na kutuma wire; siyo benki nyingi zinazoruhusu kutuma wire online. Hivyo, wengine ambao wanakuwa kibaruani muda mrefu wanaweza kuchelewa kutuma michango yao. Ningeshauri uweke taratibu mbadala za utumaji pesa kama vile Paypal, Westernunion, Moneygram na njia nyingezo zinazoweza kutumiwa baada ya saa za kazi.
   
 16. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Dada Pendo, Mungu akuzidishie nguvu na kwa wale tunaoamini katika miujiza yake Muumba kwa pamoja, Bwana aweze kutenda Muujiza katika afya yake Dada pendo. Nakukumbuka sana tulipokuna ukiwa na watoto wako watatu wadogo wakati tukishughulikia wote Viza, Nyumbani Tanzania.

  Naomba Mungu atende Muujiza wake. Mungu amjalie Mumeo nguvu ya kusimama na kutokata tamaa.

  Kwa jina la Bwana, naamini Bwana muumba wetu atatenda muujiza.

  Amen
   
 17. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  I am sorry labda nimeona vibaya au miwani yangu imeharibika. ACC OK. I did not see is the sort code. Ta
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Bob, nimnekusikia bado niko safarini lakini nitarudi later!
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Zakumi, Bob na Kichuguu,

  - Nimewasikia kuhusu maoni yenu on paypal na moneygram, naomba mnipe muda kidogo on that, lakini kwa wengine wote mnaoweza tafadhali ni kutuma tukwenye hiyo account.

  - Now naomba tena niikweke hii ishu inapotakiwa, ni kwamba hali ya mgonjwa imekua haina unafuu kabisa, kwa hiyo uamuzi umekua ni kujaribu kumfikisha nyumbani Tanzania na hasa kwao Mwanza. Mume na watoto wanazo return tickets za ndege kwa hiyo sio tatizo kwao nauli.

  - Tatizo liko kwa tickets za mgonjwa, kwa sababu shirika la ndege lina utaratibu wake, kama litakubali kumchukua alivyo sasa, safari itakuwa anytime kuanzia Jumatatu kuna fomu moja inayotakiwa kukukubaliwa nao, baada ya kua approved na madakitari kwamba it si okay kumchukua na kumsafirisha. Hilo linaendelea kwa kasi kubwa sana likisukumwa na Sister Rose Mkapa wa ubalozi wetu NY Mungu ambariki sana.

  - Shirika la ndege wameshafahamisha kwamba ili wamchukue na kumsafirisha, basi itabidi awe katika machela yake na hivyo kuwapeleka wao kuondoa viti sita vya abiria ili waweze ku-fit machela ya mgonjwa, sasa ni lazima hivi viti sita vilipiwe kama vilivyo, I mean kwa ajili ya abiria sita mgonjwa anayo return moja kwa hiyo kuna kulipia extra five seats. Hapa ndio penye a real ishu inayonifanya niwaombe ndugu zangu ku-chip in kwa chochote kile.

  Again, familia inatoa shukrani kwa misaada na sala zetu, na pia binafsi bado ninaomba niwashukuru sana wote waliokwisha itikia wito kati ya juzi na jana, na leo pia, na wale wote walionikabidhi misaada, yote ilifika.

  Otherwise, heshima zangu kwa wote na tutanguliwe na Mungu ili kuweza kuisaidia hii familia ya ndugu yetu Sister Pendo, ambaye ni hivi karibuni tu alimaliza Masters ya Accounts, huko Universty of Rochester.

  Mungu Aibariki Tanzania.
   
 20. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Poleni sanana Pole kwa familia.
  FMES!
  Tafadahali weka hata adress yao hapa ili iwe rahisikutuma kwa westunion,moneyorder na njia nyingine.Tukiwa na adress ni rahisi, weka adress yao tafadhali.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...