Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
Sijui tatizo ni shule ama ni exposure ama ni kuchukulia mambo kirahisi rahisi.
Kwa mtu prideful of my race, dignity and country hili duka hata lingekuwa na nguo za watoto nzuri kiasi gani siwezi kumpeleka mtoto wangu humu kamwe, maana akiona haya matangazo ataanza na yeye kutukuza wazungu toka mdogo manake subliminal message hapa ni kwamba huwezi kupendeza unless uwe mzungu. Ndo maana wakaona wakitumia picha za vitoto vi model vya kizungu mali itauzika.
Halafu to top it all off, location ya duka lenyewe, another reason why I would never come close to this store. Barabara tumebadilisha jina from a historic and meaningful Bagamoyo road to Mwai Kibaki, of all the people. Nchi za watu wenye raia walio na uelewa na upeo, li-mayor moja la jiji ambalo kesho kutwa linaondoka kwenye cheo haliwezi likaamka asubuhi ghafla limeshauriwa sijui na nani nyumbani kwake huko likaja likawaambia kuanzia leo jina la huu mtaa ni Yoweri Museveni! Watu watachoma mtaa! Tatizo moja kubwa la Watanzania ni kwamba hatujipendi, hatujithamini, hatujijali na hatufikiri.