Tangazo kwa wananchi wanaozunguka shamba la mifugo la Utegi

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya imetoa tangazo kwa wananchi wenye mashamba yao, mali za kudumu kuhakikisha kuwa mashamba hayo, mali hizo ziwe zimetolewa katika muda wa wiki moja kupisha kazi ya uendelezaji wa shamba. Nianze kusema kuwa nia ya Serikali ni nzuri na haipingwi lakini yafuatayo yangetiliwa maanani kwanza. (1) Kwanza lile shamba ni la wananchi mpaka sasa kwa sababu wananchi wana hati. Pamoja na kuwa wananchi walishindwa kuliendeleza nadhani kwanza Serikali ingekaa chini na wananchi na kuwaeleza manufaa watakayopata wananchi wanaozunguka shamba hilo ili wajue manufaa watakayopata siku za usoni. (2) Wananchi wamelima mashamba ambayo kwa muda wa siku saba hawawezi kuvuna mfano kuna mashamba ya mihogo na mengine bado ni michanga. Mhe. Waziri wa Maendelo ya Mifugo angetumia busara yake kuwapa hata muda wa miezi sita kuhakikisha kuwa kila mmoja anatoa mali yake. Muda waliopewa ya wiki moja kwa weli ni muda mfupi sana. Kwa hitimisho, ni vema Mhe. Waziri watalaam wako wangekaa chini na Wananachi wanaozunguka lile shamba kuhusu manufaa watakayopata siku za usoni katika kuliendeleza shamba hilo la mifugo. Tunatakiwa tuwe na Utawala bora hii ni Tanzania yetu. Pale sasa panalindwa na Maaskari wa Suma JKT na unafahamu askari akiishatoa amri hupaswi kuipinga. Wasaidieni hawa wananchi.
 
Back
Top Bottom