Tangazo kwa vijana kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea mwaka 2020

the_legend

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,611
7,047
Siku ya jana tarehe 20 August 2020 Mkuu wa tawi la Utawala JKT Kanali Julius Kadawi kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mang'era Mbuge aliwatangazia watanzania nafasi ya vijana wenye sifa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea. Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa Wilaya na za wakuu wa Mikoa wanakotoka waombaji, kuanzia mwezi Agosti 2020. Vijana watakaobahatika kupata nafasi hiyo watatakiwa kuripoti katika makambi watakayopangiwa mwezi Oktoba 2020. Aidha, Kanali Kadawi alisisitiza kuwa 'JKT HAIAJIRI'.

***UPDATE:***
“Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana kuwa watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira kwa vijana na pia halihusiki na kuwatafutia vijana ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali serikali na yasiyo ya serikari bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara tu wanapomaliza mkataba wao pale tu wanapomaliza mafunzo yao ya Jeshi la kujenga Taifa”

“Sifa za mwombaji awe raia wa Tanzania elimu na umri ,vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35” alisema kanali Kadawi.

Amesema kutokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu [COVID 19] nchini tahadhali za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama zilivyoelekezwa na serikali kupitia wizara ya afya zitazingatia kwa kipindi chote vijana watakapokua makambini.

Hata hivyo kanali Kadawi ametoa wito kwa vijana wote watakaopata fursa hiyo ya kujiunga waitumie ili wajifunze uzalendo ukakamavu stadi za kazi na stadi za Maisha na pia kuwa tayari kulinda na kulitumikia Taifa.

MWISHO
 
Vijana wazalendo watafurika kwa maelfu, huo msisitizo kuwa JKT HAIAJIRI wala hautustui... mtaani hakufai bora huko kambini.
Ni kweli. Ukiwa kambini lolote linaweza kutokea, kila mwaka wapo wanaotoboa kwa njia hiyo, na wapo pia wanaorudi mtaani baada ya mkataba kuisha
 
Kila la kheri vijana wazalendo watakaochaguliwa. Wacha wakajaribu bahati zao japo maumivu ya kutoboa mkataba ni balaa jingine.
 
Haifunguki.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
“Sifa za mwombaji awe raia wa Tanzania elimu na umri ,vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35” alisema kanali Kadawi.
 
“Sifa za mwombaji awe raia wa Tanzania elimu na umri ,vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35” alisema kanali Kadawi.
Apo sipo.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom