Tangazo kuhusu nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada kwa mwaka wamasomo 2012/2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangazo kuhusu nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada kwa mwaka wamasomo 2012/2013

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by prakatatumba, Mar 13, 2012.

 1. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
  Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  (a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
  (b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
  (c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

  3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
  Mwombaji awe na sifa zifuatazo:

  [FONT=&amp](a) [/FONT]Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
  [FONT=&amp](b) [/FONT]Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
  [FONT=&amp](c) [/FONT]Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.

  VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
  Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
  (i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
  (ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
  (iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
  (iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
  (v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
  (vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
  (vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
  (viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.

  MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
  Maombi yatumwe kwa:
  KATIBU MKUU,
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
  S.L.P. 9121,
  DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)  source: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::
   
 2. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Thank u!
   
 3. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  poa mkubwa,ngoja tuwasubirie wazee wa kilimo kwanza tuwapeleka wadogo zetu
   
Loading...