Tangazo kuhusu mradi wa bomba la mafuta Tanga, lina ukweli wowote?

babadullah

JF-Expert Member
Feb 21, 2017
508
500
Mara baada ya uzinduzi wa bomba la mafuta Tanga, kumeibuka tangazo la nafasi za ajira, tangazo hilo lina ahidi kulipa 18000 kwa Siku kwa kila kichwa. Tangazo hilo limetolewa na watu wanaojiita wasimamizi wa mradi majina yao ni Mr. Mohammed na Mr Hamisi Mkomesheni.

Wameweka namba zao ambazo ni 0743950889, 0769147744, Katika tangazo lao hawakueka anuani wala mahali zilipo office zao zaidi ukipiga simu kuna e-mail wanakutumia utume details zako baada ya hapo, mzinga unaanza.

Mzinga wa kwanza kunipiga ni baada ya kunitumia fomu wakanambia niilipie 4500 ya fomu kwa uchu wa kupata kazi nilionao nikatuma fasts mwenye huyo namba ya voda hapo juu na niliingia gharama za kuscan kitambulisho na fomu nikawatumia mwenye email yao, halafu,nikawapigia nikawaambia nishatuma nini kinafuata wakanambia tutakupigia simu

Wiki iliyopta wakanipigia wakanambia niwatumie size ya buti na ovaroli halafu nitume 17000 yaan gharama ya hivyo vitu nikashtuka sikutuma. Jana nikapata message yao kuwa niwapigie. Leo wahakiki taarifa zangu na waniambie ni lini tu naenda Chongolean kuanzia kazi. Leo mapema nimewapigia wakaniuliza una bima ya afya nikajibu ninayo ila inaisha mwezi ujao, wakanambia tuma 12000 tui-activate iwe ya kudumu sijatuma. Nina doubt na hawa watu kwa nini hawana office, kwanini wanahitaji pesa sana.

Chakushangaza akanambia safari ya Chongolean inaanza ijumaa so tuma fasta, nilipojaribu kumuulza maswali akawa mkali akanambia kuna wenzio wanapiga simu so kata simu.

Swali: Je, hili jambo ni kweli au ni utapeli? Je, serikali halioni hili tangazo kama kweli ni la kitapeli?

Kwa yeyote ajuaye ukweli kuhusu mradi anijuze. Na kama huu ni utapeli basi Mr. Mkomesheni na mwenzio Mungu anawaona na mtanilipa 4500 yangu yaani mtalpa tu hata, Siku ya kiama.

Naomba kuwasilisha
2c737f3a36903bab4ba2cb2445cbca10.jpg
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,337
2,000
hili litakuwa lile la utoe pesa kadhaa ndo uitwe mahali kuwa makini mkuu kwanza hilo litatoa matangazo kwenye gazeti la sirkali
 

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,708
2,000
Mkuu ushapigwa! Pole sana! Hii ingekua jeshini,sasa hivi ungekamatwa! CDF katoa tangazo kali sana ukiombwa hela kwa ajiri yakujiunga na JWTZ,na ukatoa unakamatwa
 

babadullah

JF-Expert Member
Feb 21, 2017
508
500
hili litakuwa lile la utoe pesa kadhaa ndo uitwe mahali kuwa makini mkuu kwanza hilo litatoa matangazo kwenye gazeti la sirkali
Mkomesheni anatumia digital trick kutapeli aise,ametengeneza e-mail yake inaitwa taug.oil pipeline tanga center.com yan lazma uingie king
hahaha eti wanauliza unavaa buti na over-roll size gani
Afu wapo serious hatary
 

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,452
2,000
Sisi waomba Ajira Wa muda mrefu tunafahamu kwamba anaetangaza kazi haombi pesa wala hasemi nipigie
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,977
2,000
if its too good to be true ....be careful huu ni utapeli mkubwa hakuna malipo kabla ya kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom