TANGAZA UTALII TANZANIA: ATCL na TANAPA wana nini cha kuwapa wanafunzi 10 (bora) waliofanya vizuri Darasa la Saba 2020?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,374
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Wiki moja baada ya kutangazwa matokeo, shirika la ndege la ATCL pamoja na mamlaka ya hifadhi ya TANAPA ina nini cha kuwapa wanafunzi 10 bora (waliofanya vizuri) katika mitihani ya darasa la saba kwa mwaka huu wa 2020?

images (8).jpg

Ninajua kuna watu watakuja hapa na kusema ATCL na TANAPA wanasubiria matokea ya kidato cha nne ili itoea zawadi kwa wanafunzi wote kwa pamoja. Mimi nitakataa kwa maana mbona wanafunzi 10 bora katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2020 hawajawapa motisha yoyote?

Mbona mimi ninaona kama hii ni fursa ya kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine waliopo darasa la sita, kidacho cha tatu pamoja na cha tano? Vile vile pamoja na kutangaza/kuhamasisha vema utalii wa ndani?

Baraza la Mitihani la Taifa nchini Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi Graiyaki iliyopo mkoani Mara, Herrieth Japhet Josephat kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (Psle).

images (7).jpg

Herrieth anakuwa msichana pekee kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, waliotajwa na baraza leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 wakati Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitoa taarifa ya matokeo hayo.

Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Huma Masala Huma kutoka shule ya msingi Kwema Morden ya Shinyanga na nafasi ya tatu ikienda kwa Gregory Mtete Alphonce kutoka Twibhoki shule ya msingi iliyopo mkoani Mara.

Aliyeshika nafasi ya nne ni Nyambina Musa Nyambina kutoka shule ya msingi Graiyaki iliyopo Mara pia.

Andrew Elias Mabula kutoka shule ya msingi Kwema Morden ya Shinganya, ameshika nafasi ya tano, Jonas Nyamataga Ayubu (Little Flower) Mara, Emmanuel Kashinje Paul (Kwema Morden) Shinyanga, Emmanuel Peter Marwa (Kwema Morden) Shinyanga, Prosper Aspenas Tumbo (God’s Bridge) Mbeya na nafasi ya 10 ilikwenda kwa Yesaya Mnkondo Bendera kutoka shule ya msingi God’s Bridge ya jijini Mbeya.

ATCL na TANAPA wana motisha gani ya kuwapa mashujaa hawa 10 wa taifa?

images (19).jpg

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,345
2,000
Hapana sisi tunawatambua tu wakina ggy knde shyshy amblulu basi hao wanafunzi wpambane na Hali zao 😂😂😂

Ova
 

tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
837
1,000
Mkuu tuwe serious kidogo!!!
Bado sijaona muunganiko wa hawa watoto na kutangaza utalii ni kundi dogo sana na hata halitaleta matokeo chanya labda useme wafanyiwe hivo kama motisha tu lakini sio kwa kutangaza utalii.

Kutangaza utalii na vivutio vyetu kunaanza na wewe . mfano kwenye magroup ya shule na vyuo ulivosoma washawishi washikija mwisho wa mwaka huu mkatembelee hata Mikumi na wao watawaambia ndugu na jamaa na hapo sasa mtaongeza pato la taifa pamoja na kueneza hamasa na nakuhakikishia mkifanya hivo hamtaacha yani kila mwaka mtaenda.

Kingine anza wewe n familia yako yaani wazoeshe watoto wako waone utalii ni sehemu ya maisha yao kila mwisho wa mwaka wapeleke hifadhi moja wapo hii itawajenga hata wakiwa wakubwa mwamko wa kutembelea vivutio vyetu utakua mkubwa.

Upande mwingine ni Tanapa pamoja na Serikali kuboresha miundo mbinu hasa barabara kufika hifadhini na malazi mazuri katika vivutio yaani hata mtu leo akifikiria kwenda Gombe National Park asianze kupata wasiwasi wa kufika na kulala.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,374
2,000
Bado sijaona muunganiko wa hawa watoto na kutangaza utalii ni kundi dogo sana na hata halitaleta matokeo chanya labda useme wafanyiwe hivo kama motisha tu lakini sio kwa kutangaza utalii.
Kwani motisha haitangazi utalii? Watoto hao wakipata treatment nzuri kutoka ATCL na TANAPA hauoni kama watazitangaza vema mamlaka/mashirika hayo kwa ndugu, jamaa na rafiki zao?

Kamwe usidhara vitu vidogo kwa maana even a small leak can sink a ship...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom