Miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika ni fahari ya Tanzania iliyobeba historia, utajili na heshima kubwa mno barani Afrika

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
MIAKA 57 YA UHURU WA TANGANYIKA NI FAHARI YA TANZANIA ILIYOBEBA HISTORIA, UTAJILI NA HESHIMA KUBWA MNO BARANI AFRIKA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Friday -7/12/2018

Siku ya kesho kutwa yani tarehe 09/12/2018 taifa letu litasherehekea miaka 57 ya uhuru wake toka ilipojinyakulia uhuru wake huo toka kwa mwingereza tarehe 09/12/1961, Tanzania ambayo ni moja ya mataifa tanzu kwenye historia ya ustawi wa umajimui wa Afrika inatazamwa kama taifa lenye heshima mno kutokana na historia yake ya ushilikiano na kujitoa kwa ajili ya ukombozi wa bara la Afrika.

Tanzania ni jamhuri ya muungano iliyoundwa baada ya Tanganyika na Zanzibar ambazo ziliungana mwaka 1964. Lakini pia Tanzania ni taifa lenye historia ndefu kwani nchi hii ndio mahali ambapo kuligunduliwa mabaki ya kale ya Binadamu (kiumbe aliyekaribiana na binadamu kwa umbile) ugunduzi huo ulifanyika kwenye Sehemu ya Bonde la Ufa katika Bonde la Oltupai George lililoko ndani ya hifadhi ya Ngorongoro , sehemu hii ndiko kulikogunduliwa masalia ya viumbe wa jamii ya watu wa kale wenye umri mkubwa kuliko yote inayojuilika Duniani mpaka sasa

Kutokana na ugunduzi huo,wanasayansi duniani wanaamini kuwa Tanzania ndiko chimbuko la binadamu.Ushahidi wa kisayansi unatokana na nyayo za binadamu zilizogunduliwa katika eneo la Laetoli lililoko kusini kidogo mwa Oltupai, kupitia hoja hizo wataalamu wa mambo ya kale wamethibitisha kuwa uwepo wa masalia ya kale hayo umeongeza uzito wa hoja ya Tanzania kuwa ni chimbuko la binadamu.

Hata hivyo Tanzania ni taifa lenye mchanaganyiko wa makabila tofauti tofauti na karibu jamii 120 za makabila huishi pamoja bila kuwepo kwa migogoro ya kikabila, huku Tanzania ikiwa ndio eneo ambapo mlima mrefu zaidi Afrika wa Kilimanjaro unakopatikana. Safu za mlima Kilimanjaro ndio safu za mlima wa volcano mrefu zaid duniani (World highest free-standing volcano) huku Tanzania ndio taifa lenye kuzungukwa na maziwa makubwa Afrika yenywe maji baridi Afrika ikiwa inazungukwa na ziwa Tanganyika, Victoria na ziwa Nyasa.

Tanzania ndio makazi makubwa zaidi ya hifadhi ya wanyama pori Afrika karibu 25% ya aridhi yake yote ni makazi ya wanyama pori na hifadhi za taifa ambapo Tanzania ikiwa inashika nafasi ya pili duniani nyuma ya Brazil, Tanzania ndio taifa linalongoza Duniani Kwa Kuwa Na Utajili Wa Urithi Wa Asili Baada Ya Brazil tembelea link hii uthibitishe hili nisemalo HOLYBET777: Agen Slot Gacor Slot88 dan Situs Judi Slot Online Terpercaya 2023 pamoja na hayo ziwa Natron ndio ziwa lenye chuvi (alkaline water body) nyingi Afrika na la tatu duniani kwa kuwa na chumvi nyingi.

Eneo la Tanzania lilianza kuona wageni toka karne ya pili (KK) wageni waarabu,Wapeshia na wachina walifika pwani ya Afrika mashariki kwa madhumuni ya biashara na ugunduzi lakini mapema Mwaka 1498 Mreno Vasco da Gama akaanza kuwasili pwani ya Tanzania kufatia ujio wa wareno Mwaka 1506 Wareno walianza kufanikiwa kudhibiti maeneo karibu yote ya pwani ya Afrika Mashariki (rejea makala yangu ya kuanguka kwa dola ya MRIMA).

Mwaka 1699 Wareno walifurushwa kutoka Zanzibar na Waarabu wa Oman. 1884 Shirika la German Colonisation Society lililoanzishwa na Mjerumani Carl Peters na kuanza kuchukua umiliki wa maeneo ya Tanzania bara. Kufatia hatua hiyo mwaka 1886 Uingereza na Ujerumani ziliingia kwenye mgogoro wa maeneo na hatimae baada ya mkutano wa Berlin zilikubaliana na kusaini mkataba wa kuruhusu Ujerumani kudhibiti maeneo ya Tanzania bara tu (Tanganyika wakati huo) na ukanda mwembamba katika maeneo ya pwani unasalia chini ya Sultani wa Zanzibar na Zanzibar kuendelea kuwa nchi lindwa chini ya ya dola ya Uingereza.

Mwaka wa 1905 mpaka 1906 tawala za ndani zilipinga uvamizi wa kikoloni na kutangaza vita mfano wa vita hizo ni ule wa Wapiganaji wa Maji Maji ambao hata hivyo walishindwa vita na wanajeshi wa Ujerumani. Kufatia hatua hiyo Ujerumani aliendelea kutawala Tanganyika mpaka mwaka mwaka 1919 baada ya vita ya kwanza ya dunia ya mwaka 1914-18 katika vita hivyo Mwaka 1916 Wanajeshi wa Uingereza,Ubelgiji na Afrika Kusini walishinda wanajeshi wa Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na kukalia Afrika Mashariki ya Kijerumani (Eneo la Afrika Mashariki ya Kijerumani lilijumuisha Tanganyika, Rwanda na Burundi).

Mwaka 1919 umoja wa Mataifa walimteua Uingereza kuwa mdhamini wa Tanganyika ambayo sasa ndiyo Tanzania bara, Uingereza aliitawala Tanganyika chini ya usimamizi wa jumuia ya umoja wa mataifa League of Nation. Kufatia kuimalika kwa utawala wa Muingereza nchini hatimae vuguvugu la kisiasa lilianza mapema mwaka wa 1929, mapema mwaka huo Chama cha Tanganyika African Association (TAA) kilianzishwa japo kuwa hakikuwa na Marengo mapana ya kisiasa lakini kupitia chama hicho ndio mwanzo wa harakati za mwanzo za ukombozi wa Tanganyika. Mwaka 1946 Umoja wa Mataifa walibadilisha idhini ya Uingereza kuwa mdhamini wa Tanganyika yani kutoka kwa mdhamini hadi kuwa mlezi. Hatua hiyo ililahisisha Tanganyika kupata uhuru mapema bila vizingiti vyovyote.

Kuimalika na muamko wa ukombozi mwaka wa 1954 ulipelekea kuzaliwa kwa TANU baada ya kubadilisha jina kutoka TAA mpaka TANU yani chama cha Tanganyika African Association kuwa Tanganyika African National Union. Baada ya vugugugu na mchango wa mwalimu Nyerere hatimae mwaka 1961 Tanganyika ilijipatia uhuru wake na Mwalimu Julius Nyerere akawa waziri mkuu mpaka ilipofika mwaka 1962 Tanganyika ilipokuwa jamhuri rasmi ndipo mwalimu Nyerere aliapishwa kuwa rais wa kwanza wa Tanganyika na baada ya mwaka 1963 Zanzibar ilipojipatia uhuru wake, mapema mwaka 1964 ziliungana na kuzaliwa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Tanganyika na Zanzibar historia zao ufanana toka historia ya mwanzo kabisa yani toka karne ya 2 (KK), kuunganishwa kwa dola hizo mbili na kuzaliwa kwa Tanzania ni moja ya miungano uliodumu Afrika na unaotazamwa kama moja ya muungano yenye histoaria kubwa japo zipo changamoto nyingi zinazoitwa kero za muungano ambazo huonwa kama moja ya kikwazo kikubwa katika muungano huu.

Zanzibar ambayo uhuru wake ulipatikana mwaka 1963 na serikali hiyo ya Sultani wa Zanzibar kupinduliwa na chama cha Afro-Shirazi Party kwenye mapinduzi ya mlengo wa kushoto yaliyokuwa na ghasia chache ya mwaka 1964 na kuingiza serikali ya Karume madalakani, baada ya mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliamua kuungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Nyerere akiwa rais wa jamhuri hiyo mpya na huku Abeid Amani Karume ambae alikuwa kiongozi wa serikali ya Zanzibar na kiongozi wa chama cha Afro-Shirazi Party akiwa makamu wa rais.

Eneo la Zanzibar ambalo liliungana na Tanganyika lilikuwa ni eneo la Usultani wa Zanzibar toka mnamo 1885, ilikuwa nchi kwenye pwani ya Afrika mashariki kati ya mnamo 1856 hadi 1964, tangu mwaka 1890 Zanzibar ilikuwa nchi lindwa chini ya himaya ya Uingereza. Zanzibari Ilianzishwa wakati wa kipindi cha kuugawa Usultani wa Omani mwaka 1856 ikaishia mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzibar na muungano na Tanganyika ulio izaa Tanzania

Usultani ulianzishwa wakati wa Sultani Sayyid Said alipoamua kuhamisha makao makuu yake kutoka Maskat (Omani) kwenda Unguja. Sayyid Said alikuwa Sultani wa Omani tangu mwaka 1804. Aliimarisha utawala wa Omani juu ya pwani ya Afrika ya Mashariki, Mwaka 1829 alifaulu kuteka Mombasa iliyokuwa mji pekee wa kujitegemea kati ya miji yote ya Uswahilini. Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa chini ya Omani tangu mwaka 1689, baada ya Wareno kufukuzwa katika pwani za Uswahilini. Sayyid Said aliona nafasi kubwa ya biashara ya karafuu kwa ajili ya soko la bara la Uhindi na kwingineko. Mapema Mwaka 1829 akaanzisha mashamba ya mikarafuu kwa kutumia kazi ya watumwa kutoka bara.

Biashara hiyo ikabadilisha uso wa mji wa Zanzibar wa karne ya 19 uliowahi kuwa kijiji kikubwa tu cha vibanda kando ya boma lililojengwa na Omani kama kizuizi dhidi ya Wareno. Baada ya azimio la mwaka 1832 la kuhamisha mji mkuu wa Omani kwenda Unguja,idadi ya wakazi wa mji ilikua kwa haraka. Nchi za nje zikatambua mji mkuu mpya na kujenga uhusiano. Ubalozi wa Marekani ulijengwa mwaka 1837, Uingereza nayo ukafuata mwaka 1841 na Ufaransa mwaka 1844. Sultani mwenyewe aliondoka kabisa Mascat mwaka 1840, Kukua kwa Zanzibar kulisababisha kukonda kwa mji wa Maskat Oman.

Baada ya kifo cha Sayyid Sultan mwaka 1856, usultani wa Oman uligawiwa kati ya wanawe.Sayyid Majid bin Said Al-Busaid (1834/18351870) akawa Sultani wa kwanza wa Zanzibar na kaka yake Sayyid Thuwaini bin Said al-Said akawa Sultani wa Oman akitawala nchi hiyo bila maeneo ya Afrika ya Mashariki. Usultani mpya ulikuwa nchi yenye nguvu kati ya Rasi Delgado (mpakani Msumbiji iliyokuwa koloni la Kireno) hadi Mogadishu (Somalia). Athira yake ilienea kupitia njia za misafara ya pembe za ndovu na watumwa hadi mto Kongo.

Wafanyabiashara kama Tippu Tip waliokuwa raia wa Usultani wakapita Tabora na Ujiji kwenda ziwa Tanganyika na kuingia ndani ya eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo. Wapagazi wao walibeba bidhaa kutoka Zanzibar zilizobadilishwa kwa pembe za ndovu. Watumwa walikamatwa au kununuliwa wakabeba pembe hadi pwani. Sultani wa pili wa Zanzibar,Sayyid Bargash,alijitahidi kujenga uhusiano na nchi za nje. Alifunga soko la watumwa Zanzibar mjini kulingana na mapatano ya kimataifa,lakini akavumilia biashara ya watumwa kuendelea chini chini. Wakati wa utawala wa Bargash majengo mengi ya Mji Mkongwe yakajengwa.

Mwishowe mwa utawala wake aliona kupungukiwa kwa eneo lake kutokana na uvamizi wa nchi za Ulaya kutokana na kuenea kwa mataifa ya ulaya kugombania maeneo katika Afrika baada ya mkutano wa Berlin. Mwaka 1885 Karl Peters alifanya mikataba ya ulinzi na watawala wadogo waliokuwa chini ya Sultani barani Tanganyika.Upingamizi wa Sultani ulishindikana kwa sababu Wajerumani walituma manowari Unguja akapaswa kukubali maeneo mapya ya Wajerumani.

Mwaka 1886 mkataba kati ya Uingereza na Ujerumani ulibana eneo la sultani la bara katika ukanda wenye upana wa maili kumi tu kati ya Rasi Delgado na Mogadishu. Bargash na mfuasi wake Khalifa bin Said waliamua kuuza maeneo hayo na mengine kuyakodisha. Hata hivyo mwaka 1887/1888 pwani ya Kenya ilikodishwa kwa Waingereza. Wakati wa uhuru wa Kenya sehemu hiyo ikaingizwa katika Jamhuri ya Kenya. Pwani ya Tanganyika ikakodishwa kwa Wajerumani mwaka 1888 na hatimaye kuuzwa mwaka 1890. Miji ya kwenye pwani ya Somalia ikakodishwa kwa Italia na mwaka 1892 mpaka mwaka 1906 ikauzwa na Mogadishu iliuzwa mwaka 1924. Hali halisi usultani ukabaki na visiwa viwili vya Unguja na Pemba tu.

Waingereza walisita kuivamia Zanzibar lakini baada ya jaribio la Karl Peters la kufanya mkataba na Sultani ili kuingiza visiwa hivyo katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, Uingereza uliamua kutoa utawala wa ndani wa visiwa. Mkataba wa Zanzibar-Helgoland kati ya Ujerumani na Uingereza ulileta patano ya kuwa Zanzibar itakuwa chini ya Uingereza. Tangu mwaka 1890 waziri mkuu wa Sultani alikuwa Mwingereza aliyepokea amri kutoka London. Lakini tangu mwaka 1913 nafasi ilichukuliwa na afisa mkazi mkuu. Kwa muda wa miaka 26 usultani ulikuwa na sarafu ya fedha yake ya pekee iliyoitwa Riali ya Zanzibar.

Maeneo yaliyoitwa baadaye (1920) "Tanganyika" na baadaye tena Tanzania Bara yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni la Ujerumani lililoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Tangu mwaka 1885 Karl Peters,kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wenyeji katika maeneo ya Usagara,Nguru,Useguha na Ukami iliyoweka msingi wa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo hayo.

Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe. Koloni lile la Kijerumani lilikuwa kubwa kuliko Tanganyika ya baadaye,maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

Uhuru ulio patikana mwaka 1961 na muungano wa mwaka 1964 hatmae uliingiza tanzania kuwa taifa la kijamaa mwaka 1967 baada ya serikali ya Nyerere kuanzisha Azimio la Arusha,ambalo lilihimiza usawa,ujamaa na kujitegemea. Ujamaa ambao ulihubiliwa na Nyerere ulilkusudia kuifanya tanzania kuwa taifa la mfano katika kuutekeleza ujamaa, uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa uliwaleta watanzania pamoja, haraka serikali ya Nyerere iliamua kuhamisha mji kwenda Dodoma hatua hiyo ilichukuliwa Mwaka 1974 pale Serikali ilipotangaza kuhamisha mji mkuu kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Mji wa Dar es Salaam ulikuwa mji mkuu chini ya Wajerumani kuanzia 1891 hadi 1974 ulipoamishwa kwenda Dodoma.

Mwaka 1977 Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) na chama cha Afro-Shirazi Party cha Zanzibar viliunganishwa na kuwa Chama kimoja yani chama cha Mapinduzi, mwaka mmoja baade yani Mwaka 1978 Tanzania iliingia kwenye vita na vita vilivyojulikana kama vita ya Kagera ambavyo vilimalizika mwaka 1979. Mwaka 1985 Nyerere aliamua kustaafu nafasi yake ya uraisi kwa kungatuka na nafasi yake kuchukuliwa na rais wa Zanzibar,Ali Mwinyi. Lakini mapema mwaka 1992 Katiba ilifanyiwa marekebisho kutoa nafasi ya siasa za vyama vingi.

Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995 Benjamin Mkapa achaguliwa kuwa rais wa awamu ya tatu wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika chini ya mfumo wa vyama vingi. Utawala wa Mkapa ulikumbwa na tishio la kigaidi lilotokea mwaka 1998 Agosti 7 katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambao uliripuliwa kwa bomu. Katika utawala huo huo wa Mkapa taifa lilikumbwa na pigo kubwa la kwanza la kumpoteza baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, msiba ulio tokea mwaka 1999 Oktoba 14i. katika uchaguzi ulio fuata wa Mwaka 2000 Mkapa alichaguliwa tena kuongoza kwa muhula wa pili kwa kupata 72% ya kura zote.

Tarehe 26 mwezi wa januari mwaka 2001 kulianza kuzuka machafuka huko Zanzibar pale Polisi wa Tanzania walipo waua kwa kuwapiga risasi watu wawili huku Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba akishtakiwakwa kosa la kuandaa mkutano haramu na kuvuruga amani ya nchi , katika machafuko hayo ya mwaka 2001 siku iliyo fuata yani 27-28 January Watu wapatao 31 waliuawa na wengine 100 kukamatwa huko Zanzibar kufatia maandamano ya kupinga hatua ya serikali ya kupiga marufuku mikutano ya upinzani kufataia hataua hiyo Serikali ya Tanzania bara iliamua kutuma wanajeshi kudhibiti hali ya amani. Baada ya macahafuko hayo hatimae march mwaka 2001 vyama viwili yani Chama tawala,Chama Cha Mapinduzi (CCM), na chama kikuu cha upinzani Zanzibar, CUF vilikubaliana kuunda kamati ya pamoja kurejesha utulivu na kuhimiza watu waliotorokea Kenya kurejea kulejea Zanzibar.

Mapema mwaka 2001 Aprili Maelfu ya wafuasi wa vyama vya upinzani waliamua kuandamana katika mji wa Dar es Salaam, kwenye maandamano ya kwanza makubwa kufanywa na upinzani katika miongo kadha. Mwaka huo huo Julai Mgodi mkubwa wa dhahabu wa Bulyanhulu, ulifunguliwa karibu na mji wa kahama na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa tatu wa dhahabu kwa ukubwa Afrika. Novemba 2001 Marais wa Tanzania,Uganda na Kenya wazindua bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mahakama ya jumuiya hiyo mjini Arusha kwa kusudio la kushughulikia masuala ya pamoja kama vile biashara na uhamiaji.

Mwaka 2002 Juni takriban watu 300 walipoteza maisha kufatia mkasa mbaya zaidi wa ajali ya treni baada ya gari moshi la kubeba abiria kugongana na gari moshi la kubeba mizigo huko Dodoma . mwaka mmoja baadae yani 2002 Agosti Upinzani wali mshutumu rais Mkapa kwa kununua ndege yake kwa gharama ya $21m (£14m) jambo liloleta mzozo mkubwa wa kisiasa nchini. Mwaka 2005 Desemba Jakaya Kikwete, aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni na mgombea wa CCM, alishinda uchaguzi wa urais na kuwa mrithi wa Benjamin Mkapa.

Ujio wa Kikwete ulikumbwa na kashfa ya kwanza ya mwaka 2008 Januari pale Gavana wa Benki Kuu Daudi Balali alipo futwa kazi baada ya ukaguzi wa hesabu wa kimataifa kuonyesha benki hiyo ilifanya malipo yasiyofaa ya zaidi ya $ 120m (£60m) kwa kampuni za Tanzania. Kufataia hatua hiyo mwaka huo huo mwezi februari 2008 Rais kikwete alivunja baraza lake la mawaziri kufuatia kashfa ya ulaji rushwa ya Richmond iliyomfanya waziri wake mkuu wa kwanza katika serikali yake Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kujiuzulu.

Utawala wa Kikwete uliotamatishwa mwaka 2015 hatimae mwezi Oktoba katika uchaguzi mkuu Dkt John Pombe Magufuli wa CCM alishinda uchaguzi na kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25 na kumfanya Magufuli kuwa raisi wa awamu ya tano (5) katika utawala huu wa awamu ya tano umejikita zaidi kwenye maswala ya uchumi wa viwanda na ujenzi wa miradi mikubwa ya kiuchumi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) pamoja na miundombinu mikubwa ya kitaifa.

Katika Diplomasia ya Nchi yetu (Tanzania), ambayo ndio kioo cha mahusiano ya taifa letu toka mwaka 1961 mpaka sasa ambayo sera hiyo ya diplomasia inatafsiriwa kupitia sera yetu ya Mambo ya Nje "Economic Diplomacy" Sera ambayo inajikita kwenye Mambo muhimu matatu kwa Maslahi mapana ya Tanzania yetu, mambo hayo ni 1.Uwekezaji (Investment), 2.Biashara (Trade) na 3.Utalii (Tourism) Haya ndiyo mambo tunayotegemea Mabalozi wetu popote walipo kuhakikisha wanayafanikisha ili kuchagiza kupata wawekezaji, masoko ya bidhaa zetu na rasilimali zetu kuweza kuvutia watalii.

Nje na hayo utawala huu wa awamu ya tano unashutumiwa kuwa unakandamiza demokrasia, haki za waandishi wa habari, uhuru wa maoni pamoja na kutokuwa na utawala wenye kufuta sheria. Matukio ya utekaji na nguvu kubwa kutumika kuzima upinzani ni moja ya dosari kubwa inayo tazamwa kwenye utawala huu.

Tukiwa tunatimiza miaka 57 ya uhuru wa nchi yetu tunapaswa kujitathimini vya kutosha kuwa je hii ndio Tanzania ya ndoto yetu?.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
FB_IMG_1557211475546.jpeg
FB_IMG_1557211482262.jpeg
FB_IMG_1557211490748.jpeg
FB_IMG_1557211485784.jpeg
 
Back
Top Bottom