Tanganyika yetuuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika yetuuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hassan J. Mosoka, Nov 12, 2010.

 1. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Miaka imekwenda na miezi haigandi tangu Mchungaji Christopher Mtikila alipoleta hoja ya kuwa na Serikali ya Tanganyika. Bungeni ikajadiliwa na kuzaliwa kundi ya G50. Kundi hili lilisakamwa na wakubwa wa ccm na kisha likasambaratishwa kabisa.
  Ukweli huu wa serikali ya Tanganyika hauwezi kufa hata kidogo. nadhani moja ya majukumu ya bunge la sasa bila kujali vyama vyao ni muhimu kufungua macho na kuona jinsi ambavyo wtu wa bara hatunufaiki na Muungano na badala yake tunabeba mizigo ya Zanzibar kila kukicha, wingi wa wabunge wao, ukubwa wa serikali yao, ni matatizo yasiyovumilika. Ni nani hasa anajadili matatizo ya watanganyika? ikiwa matatizo ya Zanzibar yanajadiliwa kwenye baraza la wawakilishi? leo wana bendera, rais makamu wawili, na sasa wanatafuta uanachama wa fifa, vya Tanganyika viko wapi?
  the time has come ni lazima turudi mezani tuutazame muungano upyaaaaa
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Masahihisho!Serikali yaZanzibar haitegemeiTanganyika na badalayake ni kuwa Tanganyika ndio inayofaidi huo Muungano na ndio sababu wakubwa wako hawataki kuileta. Ikija Tanganyika mtashindwa kufanya chochote bila kukaa chini na Serikali ya Muungano kupata baraka zake. Jee iwapo wabunge wa Tanzania watakuwa sawa kati ya tanganyika na Zanzibar kwenyeserikali ya Muungano mtakuwa na uwezo mlionao sasa?
   
 3. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tanganyika yetuu....
  Tanganyika yetuu ndo yeyee... Barani kusifika ndio yeyee!!
  Hilo ndo jambo la Msingi.... Tumeshakuwa na ukweli wa nani anamnyonya mwenziwe utaanza kuwa uchi na hasa ktk kipindi hiki ambacho nchi jirani (ZANZIBAR & PEMBA) Zimeunda Serikali moja ya Umoja wa Kitaifa la Visiwani.. United Repubic of Isles.
   
Loading...