Tanganyika (Tanzania) Ingekuaje kama Wajerumani wangeshinda WW II

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Wajerumani walikuwa na mipango mikubwa sana na Dutch East Africa, mipango hiyo yote ilizimika baada ya kushindwa kwao katika vita kuu ya pili ya dunia (II WW). Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia, lakini mapenzi yao makubwa yalikua Tanganyika na waliamua kuifanya ndio makao yao makuu ya Afrika. Ulishawahi kufiikira tungekua wapi kama wangeshinda wajerumani.
 
Najua tungekuwa tumepiga hatua kimiundo mbinu na tungekuwa na majiji yanayofanana na Munich pia tungekuwa tunatema yai la kigerman mbaya sana.
Hata majirani zetu tungewaacha kwa mbali sana, Mwingereza mshindani wake mkubwa ni Mjerumani na hata kujitoa kwao EU moja ya sababu ni kuwa Mjerumani anawaamrisha na hawana jinsi. Mjerumani alishapanga Tanga uwe mji wa kwanza kutumia post code, yaani unamuelekeza mtu nyumba ya 3 barabara ya 5 na anafika.
 
Ina maana hayo mambo tukashindwa kuyaendeleza.. ?
Sasa hivi akili zetu zimeishia kushindana na mashoga na kuambia watu wasifollow mashoga kwenye insta?
Kweli mkuu wangu akili yako imeishia hapa....? Daah!
 
Wajerumani walikuwa na mipango mikubwa sana na Dutch East Africa, mipango hiyo yote ilizimika baada ya kushindwa kwao katika vita kuu ya pili ya dunia (II WW). Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia, lakini mapenzi yao makubwa yalikua Tanganyika na waliamua kuifanya ndio makao yao makuu ya Afrika. Ulishawahi kufiikira tungekua wapi kama wangeshinda wajerumani.
Historia inaonesha Tanganyika ilitwaliwa na Uingereza baada ya Ujerumani kushindwa WW I(1914-1918). Wakati wa vita vya WW II, tayari mjerumani alikwishapoteza makoloni yake siku nyingi.
 
Mada inaongelea historia kabla ya Mjerumani kupoteza makoloni yake Afrika mkuu.
 
Wajerumani walikuwa na mipango mikubwa sana na Dutch East Africa, mipango hiyo yote ilizimika baada ya kushindwa kwao katika vita kuu ya pili ya dunia (II WW). Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia, lakini mapenzi yao makubwa yalikua Tanganyika na waliamua kuifanya ndio makao yao makuu ya Afrika. Ulishawahi kufiikira tungekua wapi kama wangeshinda wajerumani.
Ingeendelea ila yangewakuta kama ya afrika kusini, Zimbabwe hata msumbiji na mngefanywa raia daraja la pili, jiulize kwa nini zilitokea revolt kama za majimaji war na chief mkwawa, kwa hiyo kama wangeendelea kuwepo na sisi massacre ndo zingekuwa nyingi kwa sababu raia wasingekubali kunyanyasika na mjerumani ni mtu ambaye hakubali kushindwa kirahisi yaani apoteze tu kirahisi. Mtu mweupe siku zote anamwona mweusi ni mtumwa na mtu asiyekamilika rejea hotuba ya bortha aliyekuwa raisi wa afrika kusini. Haya mambo tunaweza kuyafanya wenyewe kama tukiamua tu kuwekeza kwenye maarifa, sayansi na teknolojia hebu tuwaige jinsi Japan walivyofanya na Sera yao ya "copy,improve and innovate" naamini tutafika bila hata kuwategemea hao wantuita sisi manegro.
 
Nimekuelewa mkuu, cha kusikitisha ni kuwa hakuna anaejua katika miaka waliotutawala si wajerumani wala waingereza hakuna anaejua ni kiasi gani cha rasilimali waliondoka nacho, wao ndio wanajua mikoa yenye dhabu na almasi kuliko tunavyofahamu sisi.
 
Sky chat Umenichekesha,
Makaburu ni wadutch (wajerumani) wa koo zilioingia tangu miaka ya 1650-Kumbuka kilichotoke soweto na kwingineko
Hitller mtawala wa Ujerumani, kumbuka alichowafanya wayahudi (israel)
Ni kweli wangejenga miundo mbinu kwa ajili yao, lakini ungechelewa sana kuitumia. Kuna faida gani, Miundo mbinu mizuri africa kusini (bararabara, hospitali, shule, migahawa, bar, n.k) imekuwepo tangu 1650s, waafrica wameanza kupata lau harufu yake karibia 1992.
Afadhali waliondoka tuhangaike wenyewe.
 
Wajerumani walikuwa na mipango mikubwa sana na Dutch East Africa, mipango hiyo yote ilizimika baada ya kushindwa kwao katika vita kuu ya pili ya dunia (II WW). Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia, lakini mapenzi yao makubwa yalikua Tanganyika na waliamua kuifanya ndio makao yao makuu ya Afrika. Ulishawahi kufiikira tungekua wapi kama wangeshinda wajerumani.

Ni vita ya kwanza na siyo ya pili!
 
Sky chat Umenichekesha,
Makaburu ni wadutch (wajerumani) wa koo zilioingia tangu miaka ya 1650-Kumbuka kilichotoke soweto na kwingineko
Hitller mtawala wa Ujerumani, kumbuka alichowafanya wayahudi (israel)
Ni kweli wangejenga miundo mbinu kwa ajili yao, lakini ungechelewa sana kuitumia. Kuna faida gani, Miundo mbinu mizuri africa kusini (bararabara, hospitali, shule, migahawa, bar, n.k) imekuwepo tangu 1650s, waafrica wameanza kupata lau harufu yake karibia 1992.
Afadhali waliondoka tuhangaike wenyewe.
I see ur right, na walipenda sana Tanganyika kuwaondoa ingekua ngumu sana, rafiki yangu anafanya kazi Berlin nilimtembelea, katika maongezi na wazee wa kule walifurahi sana kujua ninatoka Tanganyika (kwa wazee bado ni Tanganyika), walinieleza jinsi walivyopanga mji wa Tanga uwe kama Born. Niliwauliza sababu hasa ya kuanzisha II WW ilikuwa ni nini? Walisema ni kitu ambacho wanajuta na ilikuwa kiburi tu cha Hitler kutaka kuonyesha dunia kuwa Germany ni super power.
 
Uingereza alipewa nchi yetu baada ya vita ya 1 na siyo ya pili!
The African Great Lakes nation of Tanzania dates formally from 1964, when it was formed out of the union of the much larger mainland territory of Tanganyika and the coastal archipelago of Zanzibar. The former was a colony and part of German East Africafrom the 1880s to 1919, when, under the League of Nations, it became a British mandate. It served as a military outpost duringWorld War II, providing financial help, munitions, and soldiers. In 1947, Tanganyika became a United Nations Trust Territory under British administration, a status it kept until its independence in 1961. Zanzibar was settled as a trading hub, subsequently controlled by the Portuguese, the Sultanate of Oman, and then as a British protectorate by the end of the nineteenth century.

Julius Nyerere, independence leader and "baba wa taifa for Tanganyika" (father of the Tanganyika nation), ruled the country for decades, assisted by Abeid Amaan Karume, the Zanzibar Father of Nation. Following Nyerere's retirement in 1985, various political and economic reforms began. He was succeeded in office by President Ali Hassan Mwinyi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom