Tanganyika nimekosa nini mpaka watu wangu hawanitaki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika nimekosa nini mpaka watu wangu hawanitaki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 28, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jaji Warioba: Katiba mpya Z’bar imeleta changamoto


  na Shehe Semtawa


  [​IMG] WAZIRI Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema marekebisho ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika hivi karibuni yamewafanya watu wa bara nao kudai serikali ya Tanganyika.
  Jaji Waroba alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwenye mjadala uliozungumzia muungano wa Tanzania na mchakato wa kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.
  Alisema mawazo ya watu kutoka bara ambayo yanapaswa kuheshimiwa yamekuja baada ya Zanzibar kurekebisha katiba yake na kutambulika kama nchi.
  “Zanzibar ina wimbo wake wa taifa, bendera na nembo na kwa mujibu wa marekebisho ya hivi karibuni na katiba ya Zanzibar ina ufafanuzi kwamba Zanzibar ni nchi na kwamba ni moja ya majimbo mawili yaliyoungana katika Muungano,” alisema Jaji Warioba.
  Warioba alibainisha kuwa maoni ya watu hao kutoka bara, yana nia ya kutaka kuhifadhi utambulisho wa sehemu mbili za Muungano kwa kuanzisha serikali kwa ajili ya Tanzania Bara.
  Hata hivyo, Jaji Warioba alisema iwapo serikali ya Tanganyika itaanzishwa na kuwa imara basi nayo inawezekana kwamba pia kuwa na wimbo wake wa taifa, bendera, nembo yake huku ikitambulika kama Tanganyika.
  Warioba alisema serikali hiyo ya Tanganyika inaweza kuja kuwa kama ile ya Zanzibar kwa kuzuia haki ya wapiga kura, kuchaguliwa, mamlaka ya bara na watu kutoka Zanzibar na watu wenye asili ya Zanzibar.
  Jaji Warioba alitahadharisha kuwa iwapo hali hiyo itatokea anaamini kuwa ni hatua ya kuurudisha nyuma Muungano pia kupoteza haki za kiraia na kisiasa kwa pande zote mbili.
  Akizungumzia Zanzibar alisema bado kuna kazi ya kufanya kutokana haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wabunge na serikali za mitaa kupewa watu walioishi katika jimbo husika kwa kipindi cha miaka mitatu kitendo ambacho ni kinyume cha demokrasia.
  Kwa Upande wa Shirikisho la Afrika Mashariki alibainisha kwamba kinachokwamisha juhudi hizo ni viongozi wa nchi wanachama kung’ang’ania nafasi zao za kisiasa wanazoshikilia.  [​IMG]


  juu[​IMG]
   

  Attached Files:

Loading...