Tanganyika: Nchi huru inayoruhusu raia wa kigeni kuwa viongozi wake

pauli jm

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
391
278
Naam! kama mada inavyojieleza, kwamba Tanganyika ni Taifa huru peke, linaloruhusu raia wa kigeni kuwania uongozi ndani yake.

Ninadiriki kusema haya kwa sababu kama wazenji wanasema wao ni Taifa huru sasa na sisi si ni taifa huru?

Au kama sisi haturuhusiwi kugombea nafasi yoyote ya kiuongozi kule Zanzibar sio kwamba wao sio miongoni mwetu kwamba wao ni wananchi wa nchi nyingine?.

Kama wao wana Amiri Jeshi Mkuu wao na sisi tuna wetu sio kwamba sisi tuu mataifa mawili tofauti?.

Wao wana kila kitu kama katiba yao, bendera yao, serikali yao, majeshi yao nk. Na sisi tuna vyetu ila tofauti hatuviiti vya Tanganyika ila twaviita vya Tanzania ila kimsingi kwa mtazamo wangu nivya Tanganyika maana wao wa Zenji si wana vyao.

Kama sivyo basi viwapi vyetu? Au ndio kusema sisi hatuna chetu na kama tukitengana hatutabaki na vyetu au tutagawana ?

Kwa msingi huo ambapo wa Zanzibar wanaruhusiwa kutafuta uongozi bara, mimi ninaona ni sawa na kumruhusu raia wa taifa rafiki na sisi kugombea uongozi hapa.

Kama wanajiita taifa huru, sasa mbona wanakuja kushika nyadhifa kubwa kubwa hapa bara tena mpaka urais, Ili hali wanajitapa wao ni huru.
 
Huu muungano una malalamiko sana.

Halafu wewe mleta mada utakuwa ni wa huko Zanzibar ila unataka kuchafua hali ya hewa humu.
 
Hopeless kabisa raiya ndo nini?hii mijitu hopeless nayo inaruhusiwa kuja kujaza server za JF? Ndo wale waliomaliza form four wakapata division 5
 
Kwani hivi Rais mstaafu Mwinyi ni wa wapi ? Jumbe je ? Makamo wa pili wa rais kule znz ni nani ? Usiambiwe nawe ukadhani ni kweli , wapo watu kibao wa " bara" wanamiliki majumba, biashara na mashamba ....
 
Mpemba Makame Mbarawa ndie muasisi na mpiga debe mkuu wa ile sheria ya hovyo ya mitandao
Sasa yupo ujenzi anawatumikieni" Watanganyika
Tumsubiri tuone
 
Kweli mambo yanabadilika, kipindi chetu ilikua ni nadra sana kumsikia mtu akitamka neno "tanganyika" tulizoea kusikia tanzania bara
 
Tanganyika inatisika huko kaburini. Iko siku itajitutumua na kutoka kaburini na itakuwa balaa belwa.
 
Pamoja nayote hayo ni Tanganyika inayo ulazimisha na kuu ng'ang'ania huu muungano
 
Kweli mambo yanabadilika, kipindi chetu ilikua ni nadra sana kumsikia mtu akitamka neno "tanganyika" tulizoea kusikia tanzania bara
Hivi ile jeki ya kunyanyua magaidi mazito nini hasa chanzo cha kuitwa Tanganyika jeki? CCM hawana dogo ajabu jina limebakia lile lile hata baada Tanganyika kuzikwa na kuzaliwa Tanzania bara.
 
Back
Top Bottom