Tanganyika na Zanzibar ziende mahakama ya Katiba


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,029
Likes
5,492
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,029 5,492 280
Nafikiri wakati umekwishawadia kwa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar kupata ufumbuzi wa mivutano yao kuhusu muungano kwenye mahakama ya kimataifa ya Katiba ili kujua hamta ya muungano kabla ya kupitishwa rasimu mpya ya Tume ya Jaji Joseph Warioba.

Utashi wa mwaka 1984 wa Rais wa awamu ya pili Zanzibar Aboud Jumbe umetimia, hakuna njia nyingine ya makato itakayoleta suluhisho la utata huo licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuandika na kutoa rasimu inayojadiliwa.


Nasema hivyo kwasababu muhimu kadhaa. Nijuavyo mkataba wa Muungano unaotambuliwa na Umoja wa Mataifa una mambo 11, ulisainiwa na marais wawili wa Tanganyika na Zanzibar, Julius Nyerere na Abeid Amani Karume mwaka 1964.

Nyerere amesaini kama Mkuu wa nchi ya Tanganyika na Karume ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar. Mabadiliko ya 11 ya Katiba yaliondoa nafasi ya Rais wa Zanzibar ili asiwe Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano yamejenga kizungumkuti cha utata wa kikatiba.

Katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar haiwezi kufuta au kuongeza jambo lolote katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na yale yaliosainiwa na maraisi wawili na kufikishwa umoja wa mataifa pasi na kuulizwa wananchi wa mataifa hayo na kuamuliwa .

Ni uamuzi wa wananchi wenyewe aidha kubaki na aina ya muungano uliopo au kama wanataka mabadiliko ya kimfumo na pengine

kuwapo kwa nyongeza kwenye orodha ya muungano , yabaki mambo gani muhimu na mengine yatolewe.

Ni saini mbili za marais wa Tanganyika na Zanzibar ndizo zilizoko umoja wa mataifa zikithibitisha kuwepo kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wenye mfumo wa Serikali mbili.
Serikali moja ni yenye mamlaka ya ndani kwa maana ya Zanzibar na ile inayotambuliwa na umoja wa mataifa ni Jamhuri ya

Muungano wa Tanzanaia.Taifa la Tanganyika lilikufa tokea mwaka 1964.

Tanganyika na Zanzibar zote zimepoteza utambulisho wake katika uso wa kimataifa na kuzaliwa kwa Taifa moja la Tanzania ambalo kwa miaka takriban 50 iliyopita limebeba heshima kubwa hasa kutokana na kupigania thamani ya utu wa Waafrika, ukombozi kusini mwa Afrika, kupinga ubaguzi na kuhimiza umoja.

UN hakuna kitambulisho cha Serikali ya shirikisho ya Tanzania ,mkataba wala Serikali tatu. Pendekezo hili la serikali tatu la Tume ya Warioba limetoka wapi , ikiwa litatokea , limepatikana kutokana kwa ridhaa ya wananchi wa mataifa gani ili maoni hayo yaweze kusimama kama ni utashi wa Wazanzibari au Watanganyika.


Kinachotia shaka ni kuhusishwa suala la Serikali tatu kutokana na maoni ya wananchi wakati Zanzibar kwa upande wao waliotoa maoni wengi wakitaka serikali mbili na mkataba.Kama wazo hilo lilitokana na maoni ya watanganyika kwanini basi waamulie wazanzibari wakati wote wana haki sawa katika umbile la Muungano?.


Ili tuamini muundo wa Serikali hiyo umetoakana na mawazo ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ni vyema Tume ya Warioba ikatoa takwimu halisi kwa vile suala la muundo wa muungano ndiyo uhai wa muungano wenyewe na ulinzi wa misingi ya umoja wa kitaifa.

Kutaka mabadiliko ya kimfumo bila kusikiliza maamuzi ya pande mbili kupitia vyombo husika akiwamo Rais wa Zanzibar na Tanganyika kama wakuu wa nchi, naweza kusema ni mvutano unaohitaji maamuzi ya kisheria kuliko msukumo wa kisiasa.


Katika mchakato huu ambao pia nafikiri umekiuka hatua moja ya kutanguliwa kuunda sheria na baadaye ikafuata Tume ya kukusanya maoni, nadhani kuna dosari ya msingi inayoweza kuibua mtafaruku unaohitaji kutolewa uamuzi na mahakama ya katiba.

Mathalan hatua ya Maalim Seif ya kuweka wazi msimamo wake na wa chama chake kuwa anataka Zanzibar yenye mamlaka kamili anauthibitishia umma kuwa hataki muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kutokana na sheria za umoja wa mataifa (UN) hakuna Taifa moja likawa mwanachama zaidi ya mara moja katika umoja wa mataifa yaani Zanzibar, Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muhimu tupatiwe mfano wa Taifa moja lenye mfumo huo.

Madai ya Maalim Seif , kwa upande mmoja amefanya vyema kuweka msiamamo wake bayana lakini kwa upande wa pili wa sarafu anaonekana akiwa na shauku ya kuvunja muungano uliopo.

Pengine hatua hiyo pia ndiyo inayowafanya Maalim Seif na Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba kutofautiana kimtazamo na
kimwelekeo. Maalim Seif wakati akienda kinyume na sera ya chama chake ya serikali tatu, sasa anatamani muungano wa mkataba.

Pia kumeibuka kundi la wanasiasa wanaopinga mfumo wa Muungano wa Serikali tatu na wengine wakiunga mkono bila ya kutaja

chimbuko na asili ya kuungana kwa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar, makubaliano yaliofikiwa na kuwasilishwa umoja wa mataifa.

Wanasiasa hao ni Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, Waziri wa zamani wa Muungano Peter Kisumo, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Spika wa zamani na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Jaji Mark Bomani, Waziri wa zamani wa Fedha na Gavana Edwin Mtei, wote wakijaribu kutaka kuwasemea wananchi wakati wao tayari wamekwishatoa maoni yao.

Nguvu za wanasiasa hawa za kutaka kuwasemea Watanzania milioni 44 na hatma yao wamezipata wapi wakati huu huku nafasi iliobaki ni ya mabaraza ya katiba ya wilaya, bunge la katiba na kuitishwa kwa kura ya maoni au wamekusudia kuparaganya wananchi kufikia lengo la kupata katiba mpya?


Tunaweza kufanya mabadiliko ya orodha ya mambo ya Muungano lakini iwe ni mwiko kuuchezea mfumo wa muungano kama kweli nia ni kuwaenzi waasisi wa Taifa la Tanzania lililotokana na mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.

Ikiwa hilo litashindikana basi tuelelewe kuwa safari ya kwenda katika mahakama ya kimataifa ya katiba haiwezi kuepukika pia dhambi ya kubaguana haitatuacha ila itatutafuna na kutumaliza.

Kujaribu kuifufua Tanganyika na kuifanya Zanzibar ibaki kivyake, naota kutaibuka madai ya serikali ya kichifu, majimbo na pengine dai kuu la Sultan Jamshed bin Abdullah la kuondolewa katika kiti chake kwa njia ya Mapinduzi kinyume na demokrasia linaweza kufikiriwa na kusikilizwa upya katika siasa za Zanzibar.


Katiba ni mali ya wananchi na nguvu kuu inayotoakana na msukumo wa kisheria, kukubali kuamliwa hatma yao na wanasiasa, utashi wa kisera wa chama husika au malengo yanayoweza kuvuruga umoja na amani, Tanzania inaweza kujikuta ikiacha kulima shamba lake kubwa kwa kutegemea bustani.


Mwinyi Sadala ni Mwandishi wa Habari Mwakilishi wa NIPASHE visiwani Zanzibar. Anapatikana kupitia simu namba 0713276253 ama barua pepe: mwinyisadallah@hotmail.com
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
GHIBUU

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Messages
3,751
Likes
1,492
Points
280
GHIBUU

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2011
3,751 1,492 280
Mwinyi sadala ni mnafiki tunamjua, anatumikiwa na ccm anyway.
 

Forum statistics

Threads 1,275,230
Members 490,947
Posts 30,536,270