Tanganyika Law Society-taarifa Kwa Umma

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
taarifa
TAARIFA KWA UMMA

Sisi Chama cha wanasheria Tanzania Bara tumepokea kwa masikitiko nakala ya barua kutoka kwa Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu Mh. Addy Lyamuya kwenda kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu kuhusu malalamiko dhidi ya Wakili Msomi wa kujitegemea Fatma Karume kwenye shauri la ndoa kati ya Bwana Sadiq Ahmed Walji (Petitioner) na Bibi Saeeda Hassan (Respondent) leo tarehe 22/11/2007.

Barua hii ilieleza malalamiko dhidi ya Wakili Msomi Fatma Karume ambaye ni mwanachama wa chama cha Wanasheria Tanzania Bara ambaye anatuhumiwa kusumbua mahakama na kuchelewesha kesi kwa vurugu ambazo hazikuwa za lazima tarehe 21/11/2007 katika mahakama ya Kisutu wakati shughuli za mahakama zinaendelea

Tumeijibu barua ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu na kumhimiza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama wa Kisutu, Mheshimiwa Mwangesi, ayasikilize malalamiko haya ili kuthibitisha ukweli wa tukio hilo kwa haraka. Sisi kama Chama wa Wanasheria tuna wajibu wa kutetea wanachama wetu pale wanapoonewa na pia tuna wajibu wa kuwachukulia hatua kuendana na sheria na kanuni zetu pale inapothibitika kwamba mwenendo wao umekiuka maadili ya taaluma yetu.

Tuko tayari kushirikiana na Mahakama kufikia maamuzi ya kweli na haki. Endapo itathibitika kwamba Wakili Msomi Fatma Karume aliyafanya hayo yanayodaiwa itakuwa ni kitendo ambacho kitastahili kukemewa/kukaripiwa na kutolewa adhabu kwa mujibu wa kanuni za sheria kwa sababu ni kinyume na maadili ya Mawakili ambao wana majukumu kama maafisa wa Mahakama kulinda uhuru, kuiheshimu na kuisaidia Mahakama kufikia maamuzi huru na haki.


Joaquine De-Mello
Rais,
Tanganyika Law Society
22 Novemba 2007
 
ikithibitika amefanya hivyo ninafikiri sheria itachukua mkondo wake bila kujali ni mtoto wa nani. kwa mfano angelikuwa ni wakili mtoto wa mlalahoi ingekuweje?
 
Tanganyika kumbe bado ipo? Inapendeza sana, na wiki mbili zijazo tunaadhimisha uhuru wa Tanganyika.

Tanganyika Legal Society (TLS)
Tanganyika Plantations Company (TPC)
Tanganyika Farmers Association¨(TFA)
Tanganyika Instant Coffee (Africafe)
International school of Tanganyika (IST)
.................................>
Jazia
 
naaam hatimaye tunaona malezi ya watoto wa vigogo wetu.... kumbukeni wanlelewa na serikali hawa pale ambapo baba zao wanakuwa na majukumu ya kitaifa.... Heko fatma kuonesha picha ya nyuma ya pazia.
Heko Tanzania Law Society
 
Wakili Msomi Fatma Karume

Hivi 'wakili msomi' ni kisifa wanachotumia mawakili?

Any way, tuone mwisho wake, kutokana na taarifa za magazeti zinasema kuwasemea mbovu mahakimu ndio zake, ndio maana akajenga kiburi cha kujiamini,

Hakuna kitakachoendelea, 'dito best' man kabadilishiwa makosa itakuwa 'damu halisi'.
Tusubiri mazingaombwe........
 
Mimi nasubiri huo uchunguzi ufanyike ukweli uanikwe, hopefully, na hatua zichukuliwe, if any, manake bongo yetu tunaijua...
 
[QUOTE=kasana;103097]Hivi 'wakili msomi' ni kisifa wanachotumia mawakili?

Neno "learned so and so" ni kwa lawyers tu. Hawapendi litumike na mtu wa fani ingine yo yote.
 
Back
Top Bottom