Tanganyika kuzidi kunyanyasa wazanzibari, sasa kujazwa magerezani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika kuzidi kunyanyasa wazanzibari, sasa kujazwa magerezani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 19, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by administrator // 18/06/2012 // Habari // 4 Comments


  Salma Said,
  Wazanzibari wapatao 33 leo walifikishwa katika mahakama ya wilaya Mfenesini wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya mkusanyiko isivyo halali.Watuhumiwa hao wakiwemo wanawake wa wanane, wanaume 25 na watoto wawili wa miaka 15 na 17 walidaiwa kutenda kosa hilo juzi huko Donge wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wamefikishwa mbele ya hakimu Fatma Muhsin Omar kujibu mashitaka hayo.
  Pamoja na shitaka hilo, watuhumiwa hao pia walishitakiwa kwa kosa la kukataa amri ya kutawanyika, mashitaka ambayo yaliyasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Mkaguzi wa Polisi Khamis Abdulrahman.
  Akiwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashitaka huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Muhammad Nyange Haji (28) mkaazi wa Mkwajuni, Idd Makame Alawi (36) anayeishi Chumbuni, Juma Pandu Salum (30) wa Mwanakwerekwe, Kassim Abdulrahman Abdallah (30) anayeishi Mbweni pamoja na Juma Faki Juma (27) mkaazi wa Chumbuni.
  Wengine ni Mohammed Juma Jongo (30) anayeishi Sogea, Khamis Humoud Khamis (39) wa Magomeni, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Salum Shaabani Hamadi (18) wa Amani, Mussa Hassan Haji (15) mkaazi wa Magomeni, Suleiman Abdallah Khamis (32) anayeishi Mwanakwerekwe, Seif Adinani Seif (31) wa Mwanakwerekwe na Mohammed Najim Suleiman (23) mkaazi wa Darajabovu.
  Watuhumiwa wengine ni Khamis Ali Jamali (28) mkaazi wa Bububu, Mohammed Salum Bakari (27) anayeishi Nyerere, Mussa Hamadi Mussa (32) wa Magomeni, Othman Ali Khamis (22) mkaazi wa Tomondo, Kassim Shehe Khamis (5) wa Mahonda, Kheri Jecha Kheri (21) anayeishi Donge, Shukuru Pembe Juma (20) mkaazi wa Donge, Khamis Juma Ali (38) wa Donge na `Machano Omar Amour (27) mkaazi wa Bumbwini.
  Pamoja na watuhumiwa hao, watuhumiwa wengine waliotinga katika kizimba hicho ni Ali Haji Makame (45) wa Fukuchani, Nahoda Haji Ussi (60) mkaazi wa Donge, Jabu Simai Sharif (17) anayeishi Mkwajuni, Riziki Omar Chande (42) wa Mfenesini, Halima Ali Kassim (38) mkaazi wa Bububu na Zuhura Salum Said (23) anayeishi Amani.
  Wengine ni Mtumwa Haji Omar (47) mkaazi wa Kianga, Maryam Mohammed Bakari (30) wa Amani, Khadija Salum Juma (23) anayeishi Darajabovu, Hafsa Mohammed Mahfoudh (19) wa Kinuni pamoja na Saada Ali Ramadhani (28) mkaazi wa Jang’ombe.
  Wote hao walidaiwa mahakamani hapo kwamba, kinyume na vifungu vya 55 (1) na 56 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, walipatikana wakiwa wamekusanyika isivyo halali kwa dhamira ya kutenda kosa.
  Sambamba na shitaka hilo, pia walidaiwa kukataa amri ya kutawanyika mara baada ya kuonywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kufanya hivyo, kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
  Mahakama iliambiwa kuwa, matukio yote hayo yalitokea Juni 17 mwaka huu baina ya saa 9:45 alaasiri na saa 10:35 katika maeneo ya Mahonda na Donge wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
  Wakati watuhumiwa 32 wakikana mashitaka hayo, mshitakiwa Ali Haji Makame hakuwepo mahakamani hapo licha ya kusomewa shitaka hilo, na habari zilizoelezwa mahakamani hapo zimedai kuwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
  Watuhumiwa wote hao wanasimamiwa na Wakili wa Kujitegemea Suleiman Salim Abdallah, ambaye aliiomba mahakama hiyo iwapatie wateja wake dhamana kwa masharti nafuu yatakayoweza kutekelezeka, ombi ambalo halikupingwa na upande wa mashitaka.
  Akikubaliana na hoja hizo, hakimu Fatma Muhsin Omar aliwataka watuhumiwa hao kila mmoja kujidhamini kwa bondi ya shilingi 100,000 pamoja na kuwasilisha wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, ambao kila mmoja atasaini bondi ya kiwango kama hicho cha fedha.
  Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kuiarisha na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa, ili kupata muda zaidi wa kukamilisha upelelezi huo, ambapo hakimu Fatma aliiahirisha hadi Julai 2 mwaka huu kwa kutajwa.
  Wakati watuhumiwa hao wakiwa mahakamani hapo, ndugu na jamaa zao wa karibu hawakuruhusiwa kusogea katika eneo la mahakama na kutakiwa kukaa mbali, huku hali ya ulinzi katika eneo zima la mahakama hiyo uliimarishwa kwa askari Polisi wa Kikosi cha Kuzuwia Ghasia (FFU) waliokuwa wamevalia mavazi maalumu pamoja na mikononi mwao kushikilia silaha za mabomu ya machozi ili kukabiliana na hatari yoyote itakayo jitokeza, na askari Polisi wa kawaida na wengine waliovalia kiraia kutanda kila eneo kwa madhumuni ya kuimarisha hali ya usalama.
  Imehaririwa na www.MZALENDO.NET
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Hizi ndizo hizo amri za Kikwete na Mjimbi kwa vile hana ndugu zake Zanzibar kwa hio hana hasara yoyote wazanzibar kunyanyaswa ,lakini hii powa maana ndio kuzidi kuwachukia Watanganyika kwa Ukoloni wao Zanzibar.
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  nafanisha wazenzji na mwanamke aliyepata kazi na kuanza kumdharau n kumchafua mumewe
   
 4. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi employment rate ya Zanzibar nani anaifahamu?
   
 5. s

  swrc JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Kakke. Inaelekea wewe ni mbaguzi namba 01. Inakuaje kila kitu ni uzanzibari na utanganyika? Hata kwa mambo ambayo dhahiri siyo?:llama:
   
 6. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ulichokiwasilisha hakilingani kabisa na kichwa cha habari. kufikishwa mahakamani si kufungwa madam, isitoshe na dhamana iko wazi. Utanganyika na Uzenji umetokea wapi? hiyo dhambi ya ubaguzi itawatafuna sana kwa kujiendekeza kwenu. MUNGU awaepushe any way.
   
 7. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeongoa na Kiongozi mmoja wa Serikali ndogo ya Tanzania Zanzibar, amenidhibitishia kuwa Uamsho ni CUF kwa wanaamini tukufika kipindi cha Uchaguzi mkuu katika hali hii basi ni dhahir kuwa CUF ndio washindi, na wakishinda wao kama serikali watabadilisha zaidi katiba na pia kubadilisha aina ya Muungano ili Tanzania Zanzibar iendelee kujitoa kidogo kidogo
   
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  kama walikiuka amri ya polisi ya kutawanyika..polisi inayo haki ya kuwapeleka mahakamani kwani hakuna aliye juu ya sheria..kama suala ni muungano si waombe kibali cha kuandamana??
   
Loading...