Tanganyika iko hai bado

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,362
12,706
Birthday ni siku kuu ya kujikumbusha siku ya kuzaliwa ya kitu kilichokohai bado, kikishakufa unaadhimisha siku kilipokufa.

Sherehe za tarehe 9 December zinatukumbusha siku ya uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni na wala sio uhuru wa Tanzania bara. Tanzania bara ilizaliwa tarehe 26 April mwaka 1964 siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wala sio tarehe 9 December kama watu wengine wanavyoziita sherehe hizi za uhuru.

Ni makosa makubwa kuita sherehe za uhuru wa Tanganyika kuwa ni sherehe za uhuru wa Tanzania bara, kufanya hivi ni sawa na mtoto aliyeamua kumuita mzazi wake kwa majina mengine ya kupewa kutokana na matukio mbalimbali kwenye kimaisha, kama vile badala ya baba kuitwa Daudi Kamatta unamuita "baba Mathayo" baada ya kuzaa mtoto anayeitwa Mathayo, au kumuita mzazi wa kike "Mrs. Kamatta" baada ya kuolewa na baba yako badala ya jina lake halisi la Amina Manyata. Je, kisheria Amina Manyata ni sawa na Mrs. Kamatta au Mama Mathayo?

Kwa maoni yangu sherehe za uhuru ziitwe sherehe za uhuru wa Tanganyika moja kwa moja na isiwe za uhuru wa Tanzania bara kama watu wengine wanavyoziita.

Kwa sherehe hizi ni ishara ya kuonyesha kuwa Tanganyika ilikuwepo, ipo na itakuwepo. Kama Tanganyika haipo basi kumbukumbu hii pia isiwepo ili ibaki kumbukumbu ya kuzaliwa Tanzania bara tu hapo tarehe 26 April.
 
Kimsingi Tanzania ndio Tanganyika, hako ka Zanzibar ni ka koloni ketu, huoni sifa kuwa hata sie tulishawahi kuitwala nchi kama wazungu walivyotutawala?
 
Mpendwa, kavulata Kwani Uhuru gani unazungumzia au Wakoloni gani unamaanisha ?!!!
Hao wakoloni mnaowataja, Nahisi bado wanasaidia nchi hii....!!
Hao wakoloni mnaowataja, Bajeti yetu inakadiriwa kwa ufadhili wao ...!!
Hao Wakoloni mnaowataja, Matibabu yetu yapo katika Wema na gharama zao......!!
Hao Wakoloni mnao wataja, Elimu na mafunzo ya Juu yanalipiwa na mfuko wao...!!
Hao wakoloni mnao wataja Wanatoza kodi wananchi wao ili wastawishe Jamii ya nchi zetu za Ufisadi !! (masikni hatujui hata kuwa shukuru) !!
THINK....THINK
 
Last edited by a moderator:
Tanzania bara imezaliwa mwaka 1964 wakati Tanzanyika ikiwa inafikisha karibu miaka mitatu tangu ipate uhuru wake hivyo Tnzania bara bado haijafikisha miaka 53 ya uhuru bali Tanganyika ndiyo imefikisha miaka hiyo. Huu ukweli watu wengine hawataki kuusikia lakini ndio ukweli.
 
Wakati mwingine huwa nashangaa, tunaposherehekea miaka 53 ya kuwafukuza wakaloni ili hali bado misaada ya kibajeti inawategemea hao hao. Huwezi kuwa huru kama bado unamtegemea mtu mwingine katika kuendesha maisha yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom