Tanganyika Ikirudi Tutarudisha Mipaka ya 1886 kati ya Zanzibar and Tanganyika

Suala la mipaka sio suala nyeti ipo kwenye document na kila nchi inajua mipaka yake, tanganyika,zanzibar, rwanda,kenya, burundi wote wanajua mipaka yao. hili suala la kuvunja muungano kwa tanganyika linaanza kuwa zito kwa hapo, hata mh: lissu aliisema zanzibar na mipaka yake ya eneo la bahari akimaanisha na kilomita kumi pia ni kwamba tanganyika haina bahari, pia ndio maana hata ramani ya tanganyika mji mkuu uko dodoma. hili la mipaka ndio suala la mwanzo waznz tutakalolichukua punde tu ukivunjika.
 
Faida za elimu ya mafungu hizo. Nadhani shule yako wewe ndiyo ndogo, na unatakiwa urudi shule thabiti; umekusanya habari vipande vipande na unadhani kuwa ndiyo historia yenyewe. Nitarudia tena kwa kusisistiza kuwa nchi inayojulikana kama Tanganyika haikuwapo mpaka baada ya vita ya kwanza ya dunia ambapo ile nchi iliyokuwa ikiitwa Deutsch Ost-Afrika ilipogawanywa baina ya Uingereza na Ubelgiji. Vipande vilivyochukuliwa na ubeligiji vikaitwa Rwanda na Burundi, halafu lile pande lilichokuliwa na Uingereza likaitwa Tanganyika. Wakati huo Usultani wa Zanzibar ulishagawiwa kwa Uingereza kwa hiyo haukuwa sehemu ya Deutsch Ost-Afrika tena. Uingereza waliamuia kuliita pande hilo kuwa Tanganyika kwa sababu mbili kubwa; nitakuachia kazi hiyo urudi shule kutafuta sababu hizo.

Mkuu mbona ulishaeleweka muda mrefu sana? Hebu acha kujibizana na hao wapiga ramli. Nakupongeza sana Mkuu wangu. Kumsaidia huyo kichwa maji, asome kitabu kwenye link hiyo hapo chini ingawa kwa hulka zao hawakawii kuja na visingizio vingine kama vile kimeandikwa na Nyerere, na upuuzi mwingine kama huo.

Uk. wa 24 wa hicho kitabu kuna maelezo haya: "
... Britain received the Mandate for the part of German East Africa referred to as TANGANYIKA Territory, A NAME THAT WAS OFFICIALLY GIVEN TO THE British area in JANUARY 1920".

The Political Development of Tanganyika - James Clagett Taylor - Google Books
 
Naona mwisho mbaya hapa , wazenji wanayatafuta makucha ya watanganyika kwa lazima ,
msihofu soon enough tutawaonyesha kwamba sisi hatubwabwaji mbele yenu ila tunatenda
 
Suala la mipaka sio suala nyeti ipo kwenye document na kila nchi inajua mipaka yake, tanganyika,zanzibar, rwanda,kenya, burundi wote wanajua mipaka yao. hili suala la kuvunja muungano kwa tanganyika linaanza kuwa zito kwa hapo, hata mh: lissu aliisema zanzibar na mipaka yake ya eneo la bahari akimaanisha na kilomita kumi pia ni kwamba tanganyika haina bahari, pia ndio maana hata ramani ya tanganyika mji mkuu uko dodoma. hili la mipaka ndio suala la mwanzo waznz tutakalolichukua punde tu ukivunjika.

Mji mkuu kuwa dodoma hausiani na kutokuwa na bahari. Bado siamini kama akiliyako unayoamini ni timamu inaweza kufikiri kifupi hivyo. Kwan bahari na mji mkuu vina uhusiano gani?
 
swadakta mkuu. wazenji weusi wote ni watu wa tabora. walichukuliwa na tiptip hadi bgmy then sagulasagula ikafanyika pale wengine wakaishia unguja.

"taireni jamaa, ni upotoshaji wa mambo huo. si kweli kuwa wazenji weusi wote ni wa asili ya tabora, wapo tunakubali tena sio weusi tu kama unavyofikiri wewe, bali hao uwaonao wewe waarabu wengi wao wana damu za kinyamwezi na kimanyema, mfano Dr Salim A Salim, ana damu ya kimanyema umamani kwake, au kama umemsikia Almarhum Shk Ali bin Muhsin Albarwan (Zaim) anayo damu ya kimanyema umamani kwake. Hili hatulikatai. ndio tukasema muungano wa kijamii tulionao abadan hauwezi kuvunjika (sio kama mnavyodhani, mmeweka roho mbaya tu mbele) muungano TUNAOUVUNJA sisi ni huu wa kisiasa, kama mnapenda muungano si muungane na rwanda/burundi/malawi/uganda n.k? kwanza hata mila/desturi mumefanana? we huoni juu ya kuwa tumechanganya damu (zanzibar + tanganyika + nyenginezo) lakini tupo tofauti kimila/silka ? huwezi kunambia huyo mweusi (mtabora) ulomuona wewe wa hapa zanzibar ni sawa (kimila/desturi/akhlaak) na yule wa tabora"
 
Naona mwisho mbaya hapa , wazenji wanayatafuta makucha ya watanganyika kwa lazima ,
msihofu soon enough tutawaonyesha kwamba sisi hatubwabwaji mbele yenu ila tunatenda

"sisi hatujayatafuta makucha ya waTanganyika (maana hamnayo ya kutushinda sisi, na udogo wetu pamoja na cuhache wa watu), waulize viongozi wako wa ccm wanaoing'ang'ania Zanzibar wakueleze nini Zanzibar?"

 
Nahiyo pwani ya kenya...mombasa, malindi, lamu etc mnarudishaje?
Nadhani mkiweza kurecover eneo hilo basi dar tanga lindi yote yenu?
 
Wazungu (wakoloni) walituweza sana kwa kuchora hiyo mistari.................sasa tumechanganyikiwa kwa tamaa ya madaraka na mali........Mungu tuepushe na hilo
 
Kwanini turudie mipaka ya 1886 ambayo ni matokeo ya uamuzi wa serikali za kikoloni na mkutano wao wa berlin? Muungano ukifa tutarudi nyuma zaidi kabla ya makubaliano ya berlin...zanzibar mtapata kisiwa cha Fumba tu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kweli mleta mada unacheza, kwa kutumia mipaka ya mwaka huo unafikiri hata Kenya watawaruhusu mchukue ufukwe wao wote? Halafu mmege kipande kidogo cha Somalia? Jaribu kuwaza yanayowezekana!
 
Vipi Mombasa na Malindi! Au Sultani kasahau sehemu ya himaya yake!!
 
Mipaka ya 1886 inaweza kuwa ndiyo sababu inayowafanya viongozi wetu waung'ang'anie Muungano huu!
Natambua kwamba kulikuwa na makubaliano fulani ambayo yalimfanya Sultani atoe Coastal strip kwa Wajerumani mwaka 1890!
Nikiiangalia bendera ya Tanganyika na ile ya Tanzania, na kufuatilia maana za rangi, nahitimisha kwamba Tanganyika haikuwa na bahari na Mwl. Nyerere alilijua hilo ndiyo maana bendera ya Tanganyika haikuwa na rangi ya bluu.

Lakini pia kwenye Wikipedia Zanzibar imeelezwa kuwa ina-extend some distance ndani ya Mainland!
Check hapa: Zanzibar - Wikipedia, the free encyclopedia !

Je, viongozi wetu hawajawahi kuona hapa ili wachukue hatua za kusahihisha? Au maelezo haya ni sahihi na wanakubaliana nayo?

Pengine, kwa kujua mgogoro ambao ungejitokeza baadaye-kama Zanzibar isingeunganishwa na Tanganyika- Mwl. Nyerere aliamua kuhakikisha Muungano kati ya nchi hizi mbili unapatikana haraka iwezekanavyo! Nahisi ndiyo ilikuwa sababu kuu ya kuharakisha Muungano!!!

Kama kuna mtu ana taarifa sahihi za mipaka ya Tanganyika aliyokabidhiwa Nyerere na Waingereza naomba atujuze. Naomba wanajamvi mniondolee utata huu!!
 
Let zanzibar go away, nyie wazenji hiyo midomo yenu itawaponza, msione watanganyika tuko kimya, tunawacheki tu mnavyohangaika, kipindi tutakapoanza kuwafukuza huku kwetu mjue hatabaki hata mzenji mmoja huku, na hapo ndo tutaona kama hicho kivaranda chenu kitawatosha, nyie chooooooongeni sana tu, sisi tukianza sio kuchonga tena ni kuwafukuza tu, hata hivyo tumewabeba sana
 
mtatutweza sasa sisi na wakenya wote? mombasa,lamu,kilwa,dar bagamoyo,witu? au mtamtumia jeshi la sultan Qaboos?
 
603558_465865710090237_1118381087_n.jpg



Kama Tanganyika ikirudi tutarudisha mipaka ya 1886 kati ya Tanganyika na Zanzibar - Tanga,. Pangani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Lindi, Mtwara na Mafia zinarudi Zanzibar na hamna ubavu wa kutuzuia, aidha madeni ya iliokuwa Tanzania yatebebwa na Tanganyika maana ndio mliokopa, kwa hiyo Toto Tundu weka akili yako sawa sawa bungeni acha bwabwaja. haya ni maeneo yetu hata Nyerere alikuwa akijua kama hajawaambia bahati mbaya.

Tunaandaa madocument kupeleka UN likilia bwaaa tu tutakutana UN chini cha kamati ya mipaka ya kimataifa.

Kwanini urudishe mipaka ya 1884 na sio mipaka ya 1200?
 
Suala la mipaka sio suala nyeti ipo kwenye document na kila nchi inajua mipaka yake, tanganyika,zanzibar, rwanda,kenya, burundi wote wanajua mipaka yao. hili suala la kuvunja muungano kwa tanganyika linaanza kuwa zito kwa hapo, hata mh: lissu aliisema zanzibar na mipaka yake ya eneo la bahari akimaanisha na kilomita kumi pia ni kwamba tanganyika haina bahari, pia ndio maana hata ramani ya tanganyika mji mkuu uko dodoma. hili la mipaka ndio suala la mwanzo waznz tutakalolichukua punde tu ukivunjika.

Tatizo kubwa la baadhi ya wachangiaji wa JF ni lile alilowahi kusema mwanazuoni mmoja, ninamnukuu kwa lugha ya kwao japo nayo siijui vizuri, mtanisamehe nikikosea. "He who knows not and knows not that he knows not is a big simpleton".

Nukuu hii inahusiana na hapo nilipopatilia rangi nyekundu. Kutokana na uelewa mdogo wa sheria za mipaka za kimataifa kuhusiana na nchi zinazopakana kupitia bahari, mtu anafikiri kwa sababu yeye ni kisiwa basi anaweza kumiliki eneo la bahari atakavyo, hapana. Hapo umelewa. Na kwa bahati mbaya hujui kwamba hujui.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom