Tanganyika Ikirudi Tutarudisha Mipaka ya 1886 kati ya Zanzibar and Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika Ikirudi Tutarudisha Mipaka ya 1886 kati ya Zanzibar and Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumbatu, Jul 7, 2012.

 1. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  [​IMG]


  Kama Tanganyika ikirudi tutarudisha mipaka ya 1886 kati ya Tanganyika na Zanzibar - Tanga,. Pangani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Lindi, Mtwara na Mafia zinarudi Zanzibar na hamna ubavu wa kutuzuia, aidha madeni ya iliokuwa Tanzania yatebebwa na Tanganyika maana ndio mliokopa, kwa hiyo Toto Tundu weka akili yako sawa sawa bungeni acha bwabwaja. haya ni maeneo yetu hata Nyerere alikuwa akijua kama hajawaambia bahati mbaya.

  Tunaandaa madocument kupeleka UN likilia bwaaa tu tutakutana UN chini cha kamati ya mipaka ya kimataifa.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Let zanzibar go!!!
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa nini hamtuachii Tanganyika yetu tupumue?
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona sasa watu mnatutafuta KIPIGO chaa mbwa-mwizi kwa kila namna nyie hapo visiwani!

  Kwanza wewe unayeongea hapo unahabari kwamba kwenu ki-uhalisia alikotoka babu yako ni Tabora kabla ya kudakwa kama panzi na kuuzwa sokoni Bagamoyo sawa tu na samaki kaa pale feri.

  Huko unakochokonoa wewe sasa na nyie tutawarudisheni kwanza Tabora kule mlikokua kabla ya 1886 ndipo sasa mazungumzo yaanze huko huko UN Mkuu.

   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nadhani huelewi historia sawasawa kwa sababu mwaka 1886 hakukuwa na nchi inayoitwa Tanganyika. Baada ya mkutano wa Berlin mwaka 1884, sehemu kubwa ya ardhi inayojulikana leo kama Afrika ya Mashariki ilichukuliwa na wajerumani ikawa inajulikana kama Deutsch-Ostafrika; ilienea sehemu yote ya Tanzania ikiwamo na Visiwa vya Zanzibar, hadi Rwanda na Burundi. Mwaka 1890 ndipo ujerumani ilipowagawia wingereza visiwa vya Unguja, Pemba na Wilu kusudi wao wapewe visiwa vya Heligo (Heligoland). Ingawa records za kihistoria zimekuwa zinatofautiana kuhusu mkataba wa Heligoland-Zanzibar, na nafasi ya Zanzibar katika utawala wa wajeurumani kabla ya mkataba huo, zote zimekuwa zinakubaliana kuwa visiwa vya zanazibar vilikuwa chini ya himaya ua ujerumani baada ya Mfalme Bismarck wa ujerumani kutuma manowari za kivita kuvamia visiwa vile baada ya Sultan wake kupinga pwani ya kuanzia Mtwara hadi Lamu kuchukuliwa na wajerumani. Ni baada ya mgongano huo ndipo wajerumani walipojenga makao makuu ya utawala wao pale Bagamoyo.

  Nchi inayoitwa Tanganyika leo ilianza baada ya vita ya kwanza ya dunia kuisha mwaka 1919, na jina hili lilianza kutumika kati ya mwaka 1920 na 1922 hivi. mara tu baada ya vita, eneo lote linaloitwa Tanzania leo lilikuwa linajulikana kama the British Protectorate, na lilikuwa linahusisha Usultani wa Zanzibar na sehemu ambayo baadaye ilikuja julikana kama Tanganyika.

  kwa hiyo ukitaka kurudisha mipaka ya 1889, basi hautakuwa na Zanzibar wala Tanagnyika, nadhani ni vizuri ufikirie mipaka ya kuanzia mwaka 1922 kukiwa na nchi ya Tanganyika na Usultani wa Zanzibar
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,213
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Umefafanua vema sana mpaka nimekosa chakuongeza au kupungu mkuu!
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hiyo ni Mipaka ya Berlin Conference haikuwepo kabla ya hapo

  Yeah, Kama ni Mikopo Tanganyika ndiyo itaibeba lakini na pia Zanzibar ilipe Deni la UMEME ambalo haijalilipa

  Ni hilo Moja tu.

  Kingine ni Viwanda Vya Wazenji Dar Viachwe kama hicho Kizuri cha AZAM; hayo Magorofa huko Kariakoo...

  Wapemba hatuna Ugomvi nao sana Watakaa Waliko hapo Dar; na Unajua

  Mafuta yapo kati ya TANGA na PEMBA na sio ZANZIBAR nyie ni MIDOMO TU; kutukuza Uarabu na Unajua 1963

  Hao Waarabu ndio walioiba Uchaguzi wa Majority African Shiraz.
   
 8. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Tatizo liliopo kwa wenzetu (Tanganyika) ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu" Mwanasharia Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud - 2012
   
 9. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano' aliwaambia wawakilishi wa zanzibar kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.
   
 10. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa hizo points wakishajitenga mbona vita itatokea,maana kutakuwa na vitu wanavidai Tanganyika kama hivo viwanda
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Watavibebaje Kuvivusha Bahari; Tutasema hatuvitaki vichukue...
   
 12. J

  JULIUS MBIAJI Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuvunja huu Muungano ni sawa na wajukuu kuvunja ndoa ya babu na bibi yao.Kuuchokonoa ni sawa na watoto kuwaambia wazaz wao mkafunge ndoa vizuri achen kuishi kihorera.Kama tuna serikal imalize tatizo hili sisi raia halituhusu ingawa linatuumiza.
   
 13. m

  mkataba Senior Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Rudi shule haraka, naona sasa unatuongopea Watanganyika, ktk history tanganayika (Mrima) ilianza mwaka 1886 chini ya mipaka ktk hiyo map, lkini baada ya mkutano wa Heligoland ndio Zanzibar ikapunguzwa na kubakishwa Unguja, Pemba, Mombasa na visiwa vidogodogo.

  Kwa hiyo tokea hapo Z'bar ilibakia chini ya Mfalme Sultan Sayyd akiwa chini ya Uengereza na Tanganyika ilikuwa haina uhusiano kikoloni wa kuwa dola sawa na Z'bar kwani Tanganyika ilikuwa chini ya Ujerumani na ndio maana Z'bar uhuru wao ni 1963 chini ya waziri Mkuu Mohammad Shamte na Tanganyika ni 1961 chini ya Nyerere.
   
 14. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,371
  Likes Received: 8,463
  Trophy Points: 280
  Hwa Wanaojiita Wanzibat naona kuna kitu wanakitafuta kuna dalili zote za Boko harum na Alshabaab na wanatafuta pa kuanzia dawani kuzamisha kisiwa
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Faida za elimu ya mafungu hizo.

  Nadhani shule yako wewe ndiyo ndogo, na unatakiwa urudi shule thabiti; umekusanya habari vipande vipande na unadhani kuwa ndiyo historia yenyewe. Nitarudia tena kwa kusisistiza kuwa nchi inayojulikana kama Tanganyika haikuwapo mpaka baada ya vita ya kwanza ya dunia ambapo ile nchi iliyokuwa ikiitwa Deutsch Ost-Afrika ilipogawanywa baina ya Uingereza na Ubelgiji. Vipande vilivyochukuliwa na ubeligiji vikaitwa Rwanda na Burundi, halafu lile pande lilichokuliwa na Uingereza likaitwa Tanganyika. Wakati huo Usultani wa Zanzibar ulishagawiwa kwa Uingereza kwa hiyo haukuwa sehemu ya Deutsch Ost-Afrika tena. Uingereza waliamuia kuliita pande hilo kuwa Tanganyika kwa sababu mbili kubwa; nitakuachia kazi hiyo urudi shule kutafuta sababu hizo.
   
 16. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,334
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Natamani iwe keeeshooo
   
 17. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ama watanzania tunamatatizo kweli yaani tunafikiria kinyumenyume na hatupati jibu. suala hapa ni kufikiria namna ya kuimarisha muungano na si vinginevyo. Tukitaka kutengana sawa lakini suala la mipaka tuanzie ya mwaka gani ni issue nyeti na hakuna mwenye haki ya kutupangia wala kuamua. Tena ningepewa nafasi ningesema tuchukue mipaka ya BC or AD. 1800 ni juzi tu hapo. Hii ardhi yetu ina miaka nenda miaka rudi. Sultan S S aliondoka juzi tu Oman kuja kujitanua huku ndoo ajifanye mmiliki na atutenganishe. Hii hoja ya kutengana ina maslahi binafsi ndani yake na kuna wanaodhani tukitengana basi misosi itakuwa inajipeleka mezani. NO WAY
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  jana kupitia radio 1 nilisikia kuna kikundi ch uamsho huko iraq ni kajiuliza kumbe uamsho hii ya akina cuf ni tawi tu..
   
 19. 2

  2000yrs Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swadakta mkuu. wazenji weusi wote ni watu wa tabora. walichukuliwa na tiptip hadi bgmy then sagulasagula ikafanyika pale wengine wakaishia unguja.
   
 20. kituma12

  kituma12 JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  good bye Zenj
   
Loading...