Tanganyika hatukupaswa kuwa nchi huru

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Ukitazama kwa makini hoja za wachangiaji wengi humu, utaamka na jambo moja tu, hizi akili zetu si za kawaida na lakini pia sijitusi kwa kuwaza kuwa hatukupaswa kuwa huru!
Tuanzie hapa, kwanini tulitaka Tanganyika huru?
Kwanini tunakuwa na serikali?
Kwanini taifa linakuwa na viongozi wanaogharamiwa na umma?
Wengi wetu tumekuwa mashabiki wa taasisi na watu, kuna makundi ni dhambi kuyahoji na trick ni nyepesi tu, ikihojiwa ufanisi wako, wewe jibu through kabila lako, dini yako au chama chako! Watwana waliochini ya mkoloni kabila, dini au chama, watamtetea bwana wao milele bila ya kujali faida au hasara itokanayo na maamuzi yao!
Kiufupi watawala wazalendo wana shield ya watumwa wanaowatetea! Wao wataendelea kuwa mabwanyenye milele na watwana watawalinda!
Angalia hoja zinazomtaka Lowasa ajibu utakuta kuna watwana milioni wakimuongelea na yeye hatojibu milele!
Hoja ambazo kikwete anatakiwa kuzijibu, wapo watu watakwepesha mada kwa kuzungumzia personality, performance etc! Ila hoja ya msingi itakuwa diverted!
Magufuli akijadiliwa kwa utendaji wake leo, kuna watu watainunua hiyo kesi, ili mradi tu asiulizwe!
Sasa Hawa watu tunaowapa majukumu lengo letu wakafanye nini hasa? Kwanini basi tuwaachie dhamana za rasilimali zetu?
Kabulu Botha na Trump nadhani hawakosei kutufikiria watu weusi kuwa ni species tofauti!
Kwa maneno ya Botha "Mjusi kufanana na Mamba haimfanyi ndio awe na uwezo kama wa mamba"
Inawezekana sisi tunafanana na watu, so we need kuwa chini ya watu wanaojitambua! Arguments zetu nyingi ni mufilisi na huoni Substance ktk utendaji, kauli na mipango!
Sorry naonekana naongea kama mtwana lkn huo ndio ukweli tunaouonesha kwa michango yetu!
Tutakuwa huru siku tukiweza kuchanganua hoja bila ya kuchanganya issues zilizoletwa na kuwajibika kwetu dhidi ya "mabwana" zetu wa kiroho, kikabila au kichama!
 
Nakubaliana na kichwa cha habari yako kwa 100%, sisi tunatakiwa tutawaliwe tena na Mzungu kwa miaka mia (100) ijayo, tatizo kwa sasa tunatawaliwa na mkoloni mweusi, maana yake itatuchukua miaka mia mbili (200) kupata akili
 
Back
Top Bottom