Tanganyika haijawahi kuchangia hata sh.1 katika muungano, kwa nini inyooshewe kidole?

Patrick Elias

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
332
108
Kuna kasumba imeibuka hasa huku Tanganyika (nchi hewa) ya kuongeaongea hovyo eti Zanzabar ktk miaka 20 haijachangia gharama za muungano tena pasipo kusema Tanganyika imechangia kiasi gani.

Ajabu kabisa hata mbunge wa CCM chama ambacho kinaamini hakuna Tanganyika anasema hivyo pia. Suala ni kwamba kama Zanzibar haichangi na Tanganyika haipo je nani anagharamia muungano?

Jibu ni serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kama ndivyo kwanini sasa watanganyika inainyooshea kidole Zanzibar wakati hata Tanganyika haigharamii muungano?
 
aliposema zanzibar haichangii,kwa upande wa pili alimaanisha tanzania bara inachangia(ccm walilibaka jina tanganyika na kuiita tanzania bara)..nafikiri umenielewa..
 
aliposema zanzibar haichangii,kwa upande wa pili alimaanisha tanzania bara inachangia(ccm walilibaka jina tanganyika na kuiita tanzania bara)..nafikiri umenielewa..

Sijakuewa asee, hebu fafanua kidogo, zanzibar yenye smz haichangii, tanzania yenye SJMT ndo inagharamia muungano kupitia kodi inazokusanya na misaada ya wahisani, je hiyo tanzania bara inachangiaje? Na inatoa wapi pesa ya kuchangia hizo gharama? Ufafanuzi tafadhali
 
Back
Top Bottom