Tanga.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
tanga1.jpg

As you can see it is a cross between the traditional with the little thatched kiosk and the modern with the concrete building. I think this may be pretty typical of much of Africa. Although the facilities at Emau Hill are limited - well there aren’t any, but there is a mobile phone signal which is more than can be said for my home village. So no running water - well unless you count the river, no electricity, no sewage but you can text the world. As you drive towards the city of Dar es Salaam every second billboard by the side of the road is for a mobile provider. There is a two year old report by the BBC which states that 97% of Tanzania has got mobile phone coverage. Fishermen from the island of Zanzibar take their mobiles out with them to check the prices in the markets. If the price is too high in Zanzibar, they sail to Dar es Salaam and sell their catch there.
 
Tanga bwana,
Barabara za pale mjini ni safi sana na karibu zote zina lami!
Sema tu nyumba za makuti mjini ndo utamaduni- watu hawataki kubadilika. Tanga ranks 2nd in Tz kwa ukusanyaji kodi TRA though- kutokana na bandari!
 
Unachosema ni kweli. Lakini sababu moja ni kuwa nature ya baadhi ya watu walioko kule ni yale mambo ya kukaa kunywa kahawa na kuendekeza utamaduni usio na maana. Kuna tabia ya kuendekeza uvivu. Nadhani watu walioko kama Arusha na Mwanza wangepelekwa kule wangesaidia kuboost maendeleo. I might be wrong, this is just my opinion
 
Mzee,
Naomba kutofautiana na wewe, hiyo ya kwako ni stereotype na ni mbaya sana..........kuna tatizo Tanga na ukiongea na Tanga insiders watakwambia hasa nini kilichokwenda kombo!!!!. Tanga imeanza kuanguka baada ya kutokuwa tena mji mkuu, marehemu babu yangu alikuwa anamlaumu Nyerere kwa kuua Tanga....mie sina uhakika, lakini hiyo yako hapo juu ni "dhana" na ningekuomba ukatembelee Tanga!!!.
Kwanini Tabora haipo kwenye Top 3 kama ilivyokuwa enzi hizo za Tanganyika?? je pia ni uvivu?. Kwa taarifa yako kuna lawama ktk cycles flani zinatupiwa hasa kwa awamu ya kwanza kwa kusambaratika Tanga, Tabora na Z. Anywayz hii ni story ndefu nitaiachia hapo.
 
YournameisMINE,
Shusha historia ndugu yangu! Sisi wengine tumezaliwa wakati wa CCM na tunapenda kujifunza!
Ila mbona mapishi mazuri ya Wali wa nazi Tanga mbona hayajabadilika Yahee?
 
Kaka Mzalendo,
Ubaya wenyewe hii thread ipo kwenye jokes/udaku, sasa hapo inabidi kutoichukulia seriously. Ungekuwa mtu wa Tanga au mwenye asili ya Tanga basi unaweza kunielewa kiurahisi sana!!!. Tanga ni kubwa zaidi ya Tanga mjini, so ku-generalize kwamba watu wa Tanga hivi au vile si jambo zuri.
Ukisema kwamba watu wanakaa vijiweni kunywa kahawa, lazima ujiulize ni mida gani hiyo? je ni Tanga peke yake? Huku Magharibi ya mbali ninapoishi pia vijiwe vya kahawa kedekede, ila vina majina tofauti....vingine vinaitwa Dunkin Donuts, Finagle A Bagle, Starbucks, Mike's Coffee, Seattle's Best na kadhalika. Tena vinafunguliwa 5AM na kufungwa 12AM. Utakuta watu hapo kila dakika, wale wanaopiga soga haya, wenye kusoma magazeti wamo, wenye lap tops alkadhalika......lakini hakuna mtu hata mmoja alosema ati "hawa" ni wavivu kwasababu tu wanakunywa kahawa!!!!!!!!.
Tanga hasa pale mjini hakuna la kufanya kwasababu ya sera mbovu za serikali ya Dar es salaam kuanzia ile ya awamu ya kwanza. Viwanda vilikuwapo kibao Tanga, je ni chepiiiiiiiiiiii kilichofungwa ati kwasababu tu hakuna wafanyakaziiiii?? Kuna wale walio thubutu kusema kwamba bandari ya Tanga si dili kwasababu ipo karibu na MSA hivyo biashara si nzuri na bla bla bla!!.....hiyo hapo Tanga, inakusanya kodi Tanganyika second to Darisalama, now what??? Kaka hii story ndefu, lakini muda hakuna .....ipo siku tutaomba kujitoa kwenye jamhuri tuwe kivyetu, halafu wenyewe mtasema kama Wa-Tanga ni wavivu au la (joke)!!!!!. Happy thxgiving man!.
 
tanga1.jpg

As you can see it is a cross between the traditional with the little thatched kiosk and the modern with the concrete building. I think this may be pretty typical of much of Africa. Although the facilities at Emau Hill are limited - well there aren’t any, but there is a mobile phone signal which is more than can be said for my home village. So no running water - well unless you count the river, no electricity, no sewage but you can text the world. As you drive towards the city of Dar es Salaam every second billboard by the side of the road is for a mobile provider. There is a two year old report by the BBC which states that 97% of Tanzania has got mobile phone coverage. Fishermen from the island of Zanzibar take their mobiles out with them to check the prices in the markets. If the price is too high in Zanzibar, they sail to Dar es Salaam and sell their catch there.

duh!!! umenikumbusha mbali sana ndg Mwiba kutokana na hiyo picha hapo juu!!! kwani hiyo ni njia moja wapo kati ya nilizokuwa nikipendelea kutumia wakati wa kwenda ama kurudi mafundisho au kanisani wakati wa utoto wangu !!! na mara ya mwisho nilipita hapo nilipokwenda kumuhifadhi aunt yangu ktk nyumba ya milele !!!

ila shutuma zote ni kwa baba wa taifa kwa kuudidimiza mji wa Tanga
 
Tanga jamani. nakumbuka Jeshini tulikuwa na wimbo unaitwa Tanga Tanga, halafu vinatajwa vitongoji vyake, makolola, majani mapana, ...chumbageni ilikuwa burudani ya aina yake.

Wakati fulani Tanga ilivuma nadhani hata mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini. ulikuwa huwezi ukataja Sabuni, Chuma, mazuria ya katani n.k bila kuihusisha Tanga. Sijui what went wrong.
 
"Tanga Kunani". Katika wimbo huu, Wagosi wa Kaya Walitoa malalamiko mengi sana kuhusu kusahauliwa kwa mkoa huu maarufu. Walilalamikia kufa kwa viwanda, kumbi za sinema, mashamba ya mkonge nk.
Ukiangalia mamshamba haya kwa sasa yanatia huruma,angalia zile kota pale karibu na Hale (ukitoka Segera), ama zile za Mombo. Sina uhakika kilipokuwa kiwanda cha sabuni, lakini nimejionea ule uchovu wa kiwanda fulani pale Majani Mapana, mkono wa kulia kama unakwenda mjini.
Kusema kweli hali ni mbaya, lazima sirikali ifanye juhudi za makusidu kuuhuisha mkoa huu maarufu. Hata zamani tukiwa shule za msingi, tulisoma mambo mengi sana muhimu kuhusu mkoa huu, kama vile "Ndoto ya Kimweri", "Mapango ya Amboni" nk. Inakitisha sana kwamba mambo haya yote muhimu yamesahaulika.
 
Hadithi ya Tanga huwa naifananisha kwa MBALI na ile ya Detroit, Cincinatti, Toledo, Cleveland na St Louis combined!!. Yaani ni kusahauliwa, uzembe kwa kiasi flani, sera mbovu za serikali na MUDA. Muda hapo ni kwamba, kadri miaka inavyokwenda ni lazima ziwepo adaptations za kwenda na wakati. Kwa bahati mbaya sana hazikuwepo hasa kwa wenyeji na kwa upande mwingine serikali!!.
Bwana Sahara umenikumbusha sana vile viwanda pale, maana ilikuwa njia yangu enzi nikitembelea Tanga wakti wa likizo. Nilikuwa nafikia Chuda, kuna skuli mate wangu wa high school kwao ilikuwa Kwa-Minchi na family members wengine walikuwa wakiishi Nguvumali.......basi ilikuwa lazima nipite kwenye yale magofu ya viwanda. Kuna siku isiyojua watu nikamwuuliza m-sure, kwani kulikoni ikawa vile?? Majibu nilopata siwezi ku-share hapa!!.....story ya Tanga inasikitisha, lakini kama kuna haja ya ku-vitalize mji basi serikali kuu bado haijachelewa!!. Imagine kwamba bandari ya Tanga ingekuwa imekucha, fikiria nini kingetokea ktk bandari ya MSA?. Utalii, Kilimo hasa matunda na mboga mboga. Mkonge inaeleweka kwamba bei ili anguka kwenye soko la dunia tokana na competition toka kwa synthetic fibers. Lakini jamani ile advantegeous location na natural resources za Tanga including ardhi yenye rutuba na watu wake haviwezi kutumika kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima??. Watu wa Tanga sio wavivu ni very proud na hupenda familia zao, hivyo basi ni wachapa kazi wazuri kama lipo la kufanya!!. Kwani si ni wao watu wa Tanga walioanza kuzurura dunia nzima kutafuta green pastures baada ya kuwa na hakuna la kufanya nyumbani?? Jamani mie sina la kusema, ila awamu ya kwanza ipo responsible kwa kuporomoka kwa Tanga.
 
Tanga kama mikoa mingine (tabora, Rukwa n.k) iliyosahaulika enzi zile, ina changamoto kwa wananchi wake kuhangaikia maendeleo ya mikoa yao badala ya kuisubiri serikali,
Si mtaalamu wa 'policy', lakini nimesomeshwa kwenye 'health system' kuwa Tanzania imekuwa decentralized,if it is true for other sectors too, then mikoa husika/watendaji wao/wananchi wanatakiwa kukaza buti kuleta maendeleo na kuacha zile fikra za kuwa serikali italeta/itawapatia wananchi hiki na kile, kwani priority za hao wanaoahidi ni tofauti na priority za wananchi walio wengi.
 
Hadithi ya Tanga huwa naifananisha kwa MBALI na ile ya Detroit, Cincinatti, Toledo, Cleveland na St Louis combined!!. Yaani ni kusahauliwa, uzembe kwa kiasi flani, sera mbovu za serikali na MUDA. Muda hapo ni kwamba, kadri miaka inavyokwenda ni lazima ziwepo adaptations za kwenda na wakati. Kwa bahati mbaya sana hazikuwepo hasa kwa wenyeji na kwa upande mwingine serikali!!.
Bwana Sahara umenikumbusha sana vile viwanda pale, maana ilikuwa njia yangu enzi nikitembelea Tanga wakti wa likizo. Nilikuwa nafikia Chuda, kuna skuli mate wangu wa high school kwao ilikuwa Kwa-Minchi na family members wengine walikuwa wakiishi Nguvumali.......basi ilikuwa lazima nipite kwenye yale magofu ya viwanda. Kuna siku isiyojua watu nikamwuuliza m-sure, kwani kulikoni ikawa vile?? Majibu nilopata siwezi ku-share hapa!!.....story ya Tanga inasikitisha, lakini kama kuna haja ya ku-vitalize mji basi serikali kuu bado haijachelewa!!. Imagine kwamba bandari ya Tanga ingekuwa imekucha, fikiria nini kingetokea ktk bandari ya MSA?. Utalii, Kilimo hasa matunda na mboga mboga. Mkonge inaeleweka kwamba bei ili anguka kwenye soko la dunia tokana na competition toka kwa synthetic fibers. Lakini jamani ile advantegeous location na natural resources za Tanga including ardhi yenye rutuba na watu wake haviwezi kutumika kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima??. Watu wa Tanga sio wavivu ni very proud na hupenda familia zao, hivyo basi ni wachapa kazi wazuri kama lipo la kufanya!!. Kwani si ni wao watu wa Tanga walioanza kuzurura dunia nzima kutafuta green pastures baada ya kuwa na hakuna la kufanya nyumbani?? Jamani mie sina la kusema, ila awamu ya kwanza ipo responsible kwa kuporomoka kwa Tanga.

Yournameismine,
Miji iliyochanua baada ya 1980s ni Arusha, Mwanza, Dar, na Zenj. Miji mingi imeshuka chart, Tanga, Tabora, Kigoma n.k Mimi sijui kama ni sera za Awamu ya kwanza- ni circumstances tu kama za Detroit and TIME!
Miji kama Arusha na Moshi (The northern circuit) imekuwa hot sports kwa utalii Tz- what happened to Tanga with magnificant scinery of Amboni, Lushoto na Pangani not to be part of 'actual' nothern circiut wakati kuna vivutio kibao vya watalii?
 
Kaka Mzalendo,
Ubaya wenyewe hii thread ipo kwenye jokes/udaku, sasa hapo inabidi kutoichukulia seriously. Ungekuwa mtu wa Tanga au mwenye asili ya Tanga basi unaweza kunielewa kiurahisi sana!!!. Tanga ni kubwa zaidi ya Tanga mjini, so ku-generalize kwamba watu wa Tanga hivi au vile si jambo zuri.
Ukisema kwamba watu wanakaa vijiweni kunywa kahawa, lazima ujiulize ni mida gani hiyo? je ni Tanga peke yake? Huku Magharibi ya mbali ninapoishi pia vijiwe vya kahawa kedekede, ila vina majina tofauti....vingine vinaitwa Dunkin Donuts, Finagle A Bagle, Starbucks, Mike's Coffee, Seattle's Best na kadhalika. Tena vinafunguliwa 5AM na kufungwa 12AM. Utakuta watu hapo kila dakika, wale wanaopiga soga haya, wenye kusoma magazeti wamo, wenye lap tops alkadhalika......lakini hakuna mtu hata mmoja alosema ati "hawa" ni wavivu kwasababu tu wanakunywa kahawa!!!!!!!!.
Tanga hasa pale mjini hakuna la kufanya kwasababu ya sera mbovu za serikali ya Dar es salaam kuanzia ile ya awamu ya kwanza. Viwanda vilikuwapo kibao Tanga, je ni chepiiiiiiiiiiii kilichofungwa ati kwasababu tu hakuna wafanyakaziiiii?? Kuna wale walio thubutu kusema kwamba bandari ya Tanga si dili kwasababu ipo karibu na MSA hivyo biashara si nzuri na bla bla bla!!.....hiyo hapo Tanga, inakusanya kodi Tanganyika second to Darisalama, now what??? Kaka hii story ndefu, lakini muda hakuna .....ipo siku tutaomba kujitoa kwenye jamhuri tuwe kivyetu, halafu wenyewe mtasema kama Wa-Tanga ni wavivu au la (joke)!!!!!. Happy thxgiving man!.

Nakuunga mkono YournameisMINE.
Mimi niliwahi kuishi Tanga mwishoni mwa miaka ya sitini na kuondoka pale mwaka 1975 kabla sijarudi tena 1981. Lakini kwa hivi sasa sipo tena pale isipokuwa tanga imebaki kuwa ni nyumbani kwetu japo si wa asili ya Tanga. Nakumbuka wakati wote nilipokuwa ninaishi kule sikuweza kuona tofauti yeyote kati yangu na wenyeji, ni watu wakarimu na wanaoshirikiana bila ya kujali tofauti ya dini zao. kwa wakazi wa Tanga dini zao ni kwa ajili ya kuabudu tu na si vinginevyo.
Kuhusu Maendeleo ya mkoa wa Tanga, sina haja ya kuongelea mkonge kwani umeongelewa vizuri tu, isipokuwa nchi zote duniani hutenga maeneo ya nchi yake kwa ajili ya kuyapendelea kwa shughuli maalum. Kwa mfano, Arusha-Moshi (Utalii) Iringa (Kilimo cha mahindi) Morogoro (Elimu) Dodoma (makao makuu/ Shughuli za Bunge) Mwanza (Lake zone Business Centre) nk Dar es Salaam (Kila kitu) Tanga(?)
Kasi ya maendeleo ya mkoa wa tanga imepunguzwa kwa kitendo cha kuhamisha au kuendeleza kila jambo lililokuwepo tanga kufanyika Dar es salaam. Kinachotakiwa sasa hivi ni serikali itekeleze azma yake ya kuipanua na kuifanya bandari ya Tanga ihudumie kwa asilimia 100 mizigo yote inakwenda na kutoka Uganda badala ya bandari ya Dar es Salaam. Kwa kushirikiana na serikali ya Uganda na wadau wengine iimarishwe miundo mbinu ya kusafirisha mizigo baina ya Tanga Port na entry town kule Uganda. Baada ya hapo masuala mengine ya kiuchumi yatachukuwa mkondo wake.
 
Wakuu mliotangulia kuandika ktk Thread hii sina budi kuwapongeza kwani mmenikumbusha mambo mengi ya Tanga,Ni ukweli usiopingika kuwa hapo zamani ukizungumza mikoa minne Bora,Kwetu Tanga hakukosekani,lakini leo hata ukisema mikoa 15 Bora Tanga itaingia kwa kulazimishwa.

Kuna sababu nyingi zilizoifanya Tanga Ididimie,Lakini kuna mzee mmoja aliniambia kuwa Mwalimu Nyerere pia alichangia kwa kiwango kikubwa kuizorotesha Tanga,baada ya kuwagombanisha Sheikh Seleman Takadiri wa Dsm na Yule Sheikh Mkuu wa Tanga,na kwa ugomvi huo Tanga ikasuswa(Sina ushahidi na hilo nami nimelisikia tu).Lakini sababu kubwa ninayoiona mimi ni kufa kwa EA na kuzorota na hatimaye kufa kwa Shirika la Mkonge.

Niliwahi kupata Wakati wa kuzungumza na Mbunge wa Tanga Mjini Mzee Bakari Mwapachu,na kumuuliza swali hilo kwanini Tanga inakufa?Hakuweza kunipa majibu mazuri,lakini baadaye niligundua kuwa nae ni muhamiaji Tanga,kwani maisha yake yote kaishi Dar,kwa sasa anaishi Mwambani kwa ajili ya kutetea Ubunge wake tu!na si mtu mwenye Utanga haswa kama alivyo Yanga Bwanga,Zuberi Zimbwe au Marehemu Hamisi Mduruma (Bwana Kaka).

Tanga ilikuwa kila kitu,Toka kwenye Uchumi,Enzi hizo Reli ilipokuwa inafanya kazi,Bandari ilikuwa inatoa ajira kubwa kwa wakazi wa Tanga,Viwanda vya Chuma,Fertilizer na Foma vilikuwa kimbilio la walio wengi,kuwepo kwa shule za Mkwakwani,Nguvumali(Galanos) na Popatlal kulifanya mji uwe active,ukija kwenye Michezo nani asiyeijua jeuri ya Coastal Union na African Sports walipocheza Mkwakwani?

Leo Hii Tanga ipo kimya,Waungwana kifanyike nini ili Tanga yetu irudi kwenye hali yake ya zamani? Ile ya kuwa na Bashasha kutoka Nguvumali mpaka Raskazoni,na kule Mwakidila mpaka Mwambani.Turudi huko na mikakati ya kurudisha Uhai wa Tanga.Wale waliopo Lahore (Pakistan) na Johannesburg (S/A) Tuwawekee mazingira ya kurudi Limbachea kwetu, ili waje kuijenga Tanga yetu!!!!.Tukiamua Tutaweza!!,Wajenga nchi ni Wanainchi wenyewe.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom