#COVID19 Tanga yafanikiwa kutoa chanjo kwa watu 10,939

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,946
2,000
MKUU wa mkoa wa Tanga, Adam Malima, amewataka watàalamu wa afya kuacha kuingiza siasa katika kupeleka elimu ya kuhamasisha chanjo ya ugonjwa wa Covid 19 kwa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa kikao cha tathimini ya utoaji wa chanjo Corona kwa wananchi wa mkoani huo.
Amewataka wataalamu hao kujikita katika kutoa elimu ili kuweza kuongeza uwelewa kwa wananchi na hivyo kuondoa dhana mbaya iliyoko katika jamii.

"Wataalamu wa afya kama mmeweza kuhamasisha wazazi kuna umuhimu wa kuchanja watoto wachanga basi nendeni mkahamasishe watu umuhimu wa chanjo ili kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona" amesema Malima.

Aidha aliwaasa wanasiasa na viongozi wa dini kuendelea kutumia majukwaa yao kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuona manufaa ya kuchanja ili kuendelea kujilinda na maambukizi mapya.

Hata hivyo akitoa takwimu za chanjo kwa mkoa huo Mganga Mkuu wa mkoa Dk Jonathan Budenu, alisema kuwa lengo ni kuchanja walengwa 139, 000 lakini wameweza kufikia watu 10,939 sawa na asilimia 31

Amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutoa chanjo katika maeneo yenye mikusanyiko kama shuleni, sokoni, kwenye misikiti , makanisa pamoja na vyombo vya usafiri
 

ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
2,017
2,000
Apelekwe kwenye kamati kwa kupotosha jamiii na mamlaka za Serikali
Kipaumbele cha kwanza Elimi Elimu Elimu
 

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,073
2,000
yaani siku mkifanikiwa kumchanja Gwajima amini amini nawambia Watanzania tutachanja kwa 99.9%
 

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,291
2,000
Shida wahamasishaji hawajiamini kwa sbb wamekuwa wakiishi kinafiki kwa awamu iliyopita..Unaju Magu angekuwepo na ikafika akasemq nqoja tuchanje kwa sbb moja hii na hii nakuambia watu tungechanja sana..lakini kwq sasa hata wanaccm na Chadema sijaona wakichanjwa licha ya viongozi wao kutaka hata lazima itumike watu kuchanja
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom