Tanga: Watu wawili wapoteza maisha na 21 kujeruhiwa baada ya basi la Royal Classic kupata ajali

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa huku sita kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la Royal Classic waliokuwa wakisafiria, kuacha njia na kupinduka eneo la Kibaoni wilayani Lushoto jana Jumanne Desemba 11.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema basi hilo lilikua likisafiri kutoka Tanga kwenda wilayani Lushoto. Amedai chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

“Majeruhi sita kati ya 21 hali zao ni mbaya na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa matibabu zaidi,” amesema Bukombe
AJALI.jpeg
 
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa huku sita kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la Royal Classic waliokuwa wakisafiria, kuacha njia na kupinduka eneo la Kibaoni wilayani Lushoto jana Jumanne Desemba 11.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema basi hilo lilikua likisafiri kutoka Tanga kwenda wilayani Lushoto. Amedai chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

“Majeruhi sita kati ya 21 hali zao ni mbaya na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa matibabu zaidi,” amesema BukombeView attachment 965504
Dah kwetu huku... Inauma, tuwaombee majeruhi wote nafuu ya haraka, na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu
 
Back
Top Bottom