Tanga: Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameuawa na Wananchi wenye hasira kali

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000
Watu 2 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira mkoani Tanga.

Watu wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 100 katika kiwanda cha kutengeneza chokaa cha Nelkanth kilichopo eneo la Amboni jijini Tanga kushindikana.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi wa polisi Juma Ndaki amewataja majambazi waliouawa kuwa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni jijini Dar es Salaam na Mwinyimkuu Hamisi mkazi wa mtaa wa Chanika ambao walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya boxer huku wenzao wawili wakikimbia kusikojulikana.

Wakielezea vyema tukio hilo baadhi ya wafanyakazi na walinzi wa kiwanda hicho wamesema majambazi hao baada ya kuingia ndani ya geti la kiwanda hicho walikwenda moja kwa moja katika chumba cha mhasibu na walipofika walianza kunyonga mhasibu lakini wakati wa kujitetea ndipo sekretari wa mhasibu alipotoka nje ya ofii na kupiga mayoe kuashiria bosi wake amevamiwa na majambazi.

Kufuatia hatua hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho Bwana Amiry Ramadhani ameliomba jeshi la polisi mkoani Tanga kuhakikisha wanafanya upepelezi wa kutosha ili kujua kama huenda kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wamekuwa chanzo cha tukio hilo.
 

kitomondo1

Member
Oct 2, 2014
99
0
Lini hiyo kaka maana mi jana na leo nikikuepo haponsikuipata hata nyepe nyepe au kwa kua nikikua busy na magari
 

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,157
2,000
wange uwawa wote, ingekuwa vizuri zaidi' anyway: tunashukuru kwa kupunguza idadi yao, kwani Polisi wameshindwa kabisa kuhimili vishindo. "asante sana wananchi wenye hasira kali, hiyo ni kazi nzuri ya ulinzi shirikishi, na polisi jamii."
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,527
2,000
Hao sio wananchi wenye hasira bali ni wananchi wenye njaa kali........wangekuwa na hasira kali wangezionyesha kwa wahusika wa ESCROW...........ambao wamewafanya kuwa na maisha duni.....................
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,365
2,000
Timoo mwanafunzi wangu 2005 mwongozo Primary. He was so bright and brave. Mazingira magumu aliyokulia yalimsababisha kuacha shule form three na kujiajiri kwenye bodaboda.
RIP dogo.
 

manking

JF-Expert Member
Feb 8, 2014
1,308
1,195
Timoo mwanafunzi wangu 2005 mwongozo Primary. He was so bright and brave. Mazingira magumu aliyokulia yalimsababisha kuacha shule form three na kujiajiri kwenye bodaboda.
RIP dogo.
kuwa na maisha magumu haimfanyi kuwa jambazi alijitakia mwenyewe wangapi wanaishi maisha maguma zaidi na hawaibi?
 

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,788
1,500
Hao sio wananchi wenye hasira bali ni wananchi wenye njaa kali........wangekuwa na hasira kali wangezionyesha kwa wahusika wa ESCROW...........ambao wamewafanya kuwa na maisha duni.....................

Kuwafikia hao inabidi kuupoozesha mfumo mzima wa ulinzi wa Taifa hili. Macho yote ya hawa jamaa yanawaangalia wao. Nikikumbuka inflation ya exchange rate wakati wananunua ma dorali ili wakapeleke nje uswisi halafu serekale yetu ikakope huko..., ghadhabu tu!
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,135
2,000
timoo mwanafunzi wangu 2005 mwongozo primary. He was so bright and brave. Mazingira magumu aliyokulia yalimsababisha kuacha shule form three na kujiajiri kwenye bodaboda.
Rip dogo.
huyu alikuwa mmoja wa majambawazi? Rip
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,135
2,000
Wauawe tu, maana tumechoka kuibiwa na serikali ya ccm. Tuibiwe na ccm halafu tuibiwe na majambazi? This's too much.
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,527
2,000
acha UNGESE wako mpuuzi mkubwa! unajua siasa inatupotezea fedha ngapi wewe harlot?
Mkuu sehemu kama hizi ndio za kuonyesha ukomavu wako wa kisiasa kwa kuwa siasa si uadui...ingawa CCM wanatulazimisha tuwaone maadui kwa madawa wanayotufanyia......nadhani ingekuwa ni busara ya hali ya juu kama mngebishana kwa hoja....huenda angekuelewa na pengine angerudisha kadi ya CCM.....CALM DOWN KAMANDA........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom