Tanga: Watu 10 wafariki dunia baada ya gari aina ya Noah kutumbukia mtoni

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Wakuu poleni na majukumu ya kila siku.

Hivi majuzi kuna ajali ya Noah ilisombwa na maji huko Tanga, sasa nimempata habari kuwa waliokuwa kwenye gari ni mtu na familia yake, na waliangamia kwenye hiyo ajali.

Kuna taarifa kuwa ni watu wa nyumbani na wanazikwa huko Mbeya leo.

Naomba kama kuna anayefahamu lolote kuhusu msiba huu atusaidie taarifa zaidi kama vile majina ya waliofariki nk.

Shukrani.

Noah8.jpg
----- UPDATE----

Watu hao 10 walipoteza maisha baada ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T890 CCX kutumbukia kwenye korongo lilosababishwa na kukatika daraja kipande cha barabara ya Handeni-Korogwe eneo la Sindeni kutokana na mafuriko ya maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kubainisha kuwa kati ya watu hao 10, watu wazima ni nane na watoto wawili.

----

8.jpg

Picha: Majeneza yaliyobeba miili ya wanafamilia waliofariki kwenye ajali ya Noah​
 
Unaposema "ni watu wa nyumbani" una maana gani, samahani kama nitakua nimekukwaza
Mke wa huyo bwana ni classmate wangu tulisoma wote miaka hiyo, kama ni yeye lakini maana sijapata uhakika
 
Sawa ila sidhani kama hapa ni mahala sahihi sana kuuliza majina ya marehemu hao.
Ni bora zaidi kumpiga simu mtu wa nyumbani kwenu au jamaa zako huko mbeya na umuulize juu ya mkasa mzima kama ni kweli taarifa utazipata bila chenga ndugu.
 
Sawa ila sidhani kama hapa ni mahala sahihi sana kuuliza majina ya marehemu hao.
Ni bora zaidi kumpiga simu mtu wa nyumbani kwenu au jamaa zako huko mbeya na umuulize juu ya mkasa mzima kama ni kweli taarifa utazipata bila chenga ndugu.
 
Wakuu poleni na majukumu ya kila siku.

Hivi majuzi kuna ajali ya Noah ilisombwa na maji huko Tanga, sasa nimempata habari kuwa waliokuwa kwenye gari ni mtu na familia yake, na waliangamia kwenye hiyo ajali.

Kuna taarifa kuwa ni watu wa nyumbani na wanazikwa huko Mbeya leo.

Naomba kama kuna anayefahamu lolote kuhusu msiba huu atusaidie taarifa zaidi kama vile majina ya waliofariki nk.

Shukrani.
kuna mmoja ni mzigua anaitwa Abbas
 
Updates..
Taarifa za uhakika nilizozipata nikuwa Wilifrida Raymond ambaye ni mwalimu na Mumewe na watoto wao watatu walifariki kwenye hiyo ajali ya noah iliyosombwa na maji wakiwa njiani kwenda kwenye mahafali ya mtoto wao huko Same. Mazishi ya wanafamilia hao 5 yamefanyika leo huko Dar es salaam Goba. Mungu azilaze roho za marehemu hao mahala pema peponi. AMINA.
NB :Wilifrida Raymond nilisoma nae shule moja kunzia std 1 mpaka std 7.
 
Habari zinachanganya sana, kwenye vyombo vya habari walisema walikuwa wanaelekea mkoani Arusha kupeleka hela za mahari, mtoa mada unasema walikuwa wanaenda kwenye mahafali? Mungu awapumzishe pema.
 
Habari zinachanganya sana, kwenye vyombo vya habari walisema walikuwa wanaelekea mkoani Arusha kupeleka hela za mahari, mtoa mada unasema walikuwa wanaenda kwenye mahafali? Mungu awapumzishe pema.
Wlikuwa wanakisia
 
Kuna watu wanaamini uzito wa Gari Sasa utakuta mtu ana passo, vitz, oppa, spacio, duet, Noah jamani kufa kupo lakini tusikaribishe vifo kizembe, Mungu azilaze pema roho za marehem
 
Back
Top Bottom