Tanga: Ramadhani Kailima alipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kukiendeleza Chuo cha Zimamoto kilichopo Chogo, Handeni

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
KAILIMA ALIPONGEZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KWA KUWA WABUNIFU, AZINDUA MIRADI MBALIMBALI CHUO CHA CHOGO, MKOANI TANGA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kukiendeleza Chuo cha Zimamoto kilichopo Chogo, Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Kailima pia amepongeza jitihada na juhudi kubwa ambazo wanafunzi wamefanya na kuahidi Wizara itaandaa mikakati mbalimbali Ili kuweza kukiendeleza na kukikuza zaidi chuo hicho kwani tayari juhudi binafsi kuanza kuonekana.

Naibu Katibu Mkuu Kailima, amezungumza hayo wakati akifunga mafunzo ya Uongozi ya Kijeshi kwa Maafisa wa ngazi mbalimbali ya Jeshi hilo, Chogo, Wilayani humo, Ijumaa Desemba 17, 2021.

"Nawapongeza sana kwa jitihada na juhudi kubwa ambazo wanafunzi mmefanya, Wizara itaandaa mikakati mbalimbali Ili kuweza kukiendeleza na kukikuza chuo hiki kwani tayari juhudi binafsi zimeonekana," alisema Kailima.

Pia alizindua baadhi ya majengo ya Chuo hicho ambacho ni kikubwa na kina miradi mbalimbali ya ujenzi inayoongozwa na Jeshi hilo.

"Pia nampongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkuu wa Chuo hiki cha Zimamoto na Uokoaji pamoja na wasaidizi wake wote kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo katika na ninawaahidi kuendelea kuishauri Serikali kulisaidia Jeshi hili na kuhakikisha linafikia malengo yote yaliyopangwa," alisema Kailima.

Majengo aliyozindua na kuweka jiwe la msingi ni pamoja na majengo mawili mapya ya mabweni ya wanaume na tanki kubwa la kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Kailima alishangazwa na jitihada za uongozi wa Chuo pamoja na wanafunzi ambao wamekuwa wakipita chuoni hapo kwa namna ambavyo wamekuwa wakijitolea kufanya ujenzi wa majengo hayo pasipo kupata fedha toka Serikali Kuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Naibu Kamishna (DCF), Kennedy Komba alisema majengo yote mapya yanayoonekana ni nguvu za wanafunzi ambao wamekuwa wakiendelea kutoa michango kutoka mifukoni mwao, pamoja na jitihada za wadau mbalimbali ambao walichangia vifaa vya ujenzi.

20211218_092102.jpg


20211218_092105.jpg
 
Back
Top Bottom