Tanga: Polisi wazuia msafara wa Prof. Lipumba wakidai hawana taarifa na msafara huo

Upo sahihi ndiyo maana tunasema kuwa huyo ni poropesa
Hapo lengo sio Prof Lipumba, kuna kiongozi/chama maarufu cha upinzani watafanya ziara/amsha amsha hapo Tanga(rejea maazimio ya CHADEMA). Wanachofanya ni wamempanga Prof,Kwamba naye wamemzuia ili kufanya figisu kwa hicho chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba amezuiliwa wilayani Mkinga mkoani Tanga, kwa kufanya msafara bila kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Lipumba amewasili mkoani humo leo, Januari 20, 2020 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kuzugumza na Wananchama na viongozi wa CUF ambapo alikutana na katazo hilo la polisi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wameeleza Lipumba na wenzake hawakutoa taarifa juu ya ujio wa msafara wao Wilayani humo.
Na kikofia chake kama mganga wa kienyeji njaa mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishasema, bashiru anachanja mbuga tu jimbo LA zitto Kigoma.kwa sasa mchawi mwingine Wa upinzani Ni polis.
 
Ila jamani kuna wazee hawana mshipa wa aibu!
Hivi Lipumba baada ya aibu zote hizi amekosa hata shughuli nyingine ya kufanya kujiepusha na aibu hii inayoendelea?
Hatari sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyanzo vyao vina vinasaba na lipumbaa ndiyo maana hizo taarifa hazikunasa kwenye mitambo yao
Hawakuwa na taarifa za kiintelijensia kwamba kuna msafara pinzani umepangwa kupita njia hiyo hiyo kuelekea upande wanaotoka CUF na hivyo watakutana katikati na kuashiria uvunjifu wa amani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom