TANGA: Mzee wa miaka 72 aishi chini ya mti kwa miaka 15, akidai kutafuta haki yake ya shamba

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
5eb06688abf90949130cc57d63bca4c9.jpg


Mzee wa miaka 72 ambaye alikuwa Ofisa Elimu Mkoa wa Tanga mwaka 1975, John Kihendo aliyestaafu mwaka 1989, ameamua kuishi chini ya mti kwa miaka 15 kwa madai kuwa anaitafuta haki ya shamba lake lenye ukubwa wa hekari sita lililoko kata ya Magomeni jijini Tanga.

Hivyo anaiomba Serikali kumaliza mgogoro wa shamba hilo uliodumu zaidi ya miaka saba ili aweze kupata haki na hatimaye ajenge makazi ya Kudumu na familia yake.

Mzee alizungumza na kusema baada ya wapimaji kuja eneo hilo walidai linatakiwa kutumia kama kituo cha jamii (Community Center), hivyo mwaka 2004 alipewa fidia kidogo ambayo haiendani na hilo eneo.

Ameeleza kuwa amekaa eneo hilo tangu mwaka 1978 ambapo hivi sasa shamba lake limekuwa likivamiwa na watu tofauti tofauti pasipo yeye kushirikishwa ikiwa pamoja na Kanisa kujengwa ndani ya shamba lake.

"Niliwahi kuchimba msingi katika shamba hili nijenge, alikuja Mwenyekiti wa mtaa na kuamuru ule msingi ufukiwe nisijenge kwa kuwa eneo hilo ni la kituo cha jamii (Community Center)".

Pia mzee huyo alisema ameshawahi kuandika barua kwa Mkurugenzi wa jiji kuwa sehemu yake ya shamba ambayo haijatathiminiwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1999 ya ardhi.

"Mimi ni mkulima wa shamba langu na sheria ile imeshapita kwa nini nisiipate ile sehemu yangu ambayo kwa miaka 7 haijatathiminiwa. Kitu ambacho hakikutathiminiwa maana yake hakihitajiki basi ningepewa mimi mwenyewe nitumie ikiwemo kujenga nyumba yangu ya kudumu", amesema mzee Kihendo.

Chanzo: Dar24
 
Nani kamwambia haki inapatikana chini ya mti? Na umri wake wote ashawahi kusikia haki itapatikana chini ya mti zaidi ya mahakamani? Aendelee kuishi hapo hapo miaka mingine 10
 
Kosa alilolifanya nikuchukua fidia ambayo anasema haiendani na sehemu yake kwann asingekataa
 
Back
Top Bottom