Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga zimeanza kuleta madhara baada ya kusababisha kifo cha mtoto mmoja kwa kuangukiwa na ukuta huku mwingine akijeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema kuwa hadi leo mvua hizo zilikuwa zimesababisha madhara katika wilaya za Korogwe, Pangani na Kilindi.
Alisema katika Wilaya Pangani mtoto aliyemtaja kwa jina la Francis Mgabo(4) alikufa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba iliyokuwa ikijengwa ya Mwanaisha Selemani.
Alisema katika tukio hilo Fatma Ali (3) alijeruhiwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba hiyo na amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Pangani kwa matibabu.
Chanzo: Mwananchi