Uchaguzi 2020 Tanga: Mgombea Urais wa ADC aahidi kuboresha Sekta ya Madini na Mfumo wa Afya

ADC Party

Member
Sep 14, 2020
28
29
Mgombea Urais wa Chama cha ADC, Queen Cuthbert Sendiga Leo ameendelea na kampeni zake katika Wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, Kata ya Mabanda (Misima).

Katika mkutano huo, amewaahidi wananchi hao kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha kuwa ataboresha sekta ya Madini kwa kuondoa tozo ambazo hazimsaidii Mchimbaji Mdogo katika Taifa letu, hivyo endapo atakuwa Rais atahakikisha anakwenda kufuta kodi kwa Wachimbaji wadogo nchini ili kumsaidia mchimbaji Mdogo.

Amesema Serikali atakayoiongoza itahakikisha Mchimbaji anatoa tozo ambazo anazimudu, pia atahakikisha wanaanzisha mifuko kwa ajili ya Wachimbaji wadogo ili waweze kunufaika na uchimbaji wao.

Pia amewaahidi wananchi hao kuwa endapo atakuwa Rais ataboresha mfumo wa afya nchini kwa kuhakikisha bima za afya zitakazotolewa zinamtibu Mtanzania na atatibiwa magonjwa yote bila kubagua Dawa au ugonjwa maalum.

1600795110803.png


1600795138226.png


1600795165771.png
 
Back
Top Bottom