Tanga: Eneo la Mandera Wilayani Korogwe barabara kuu kutoka Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam haipitiki

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
48,281
53,246
Mvua Zinazoendele Kunyesha Mikoa Ya Kaskazini Mwa Tanzania, Zimesababisha Eneo La Mandela Hasa Barabarani Umbali Wa Mita 60 Kujaa Maji Na Kusababisha Njia Hiyo Kutoonekana.

Baadhi Ya Watu Waliofanya Safari Usiku Wa Jana Wamelala Hapo Na Idadi Ya Magari Kutoka Njia Kuu Ya Tanga Kwenda Kilimanjaro Na Kilimanjaro Kwenda Tanga, Dar es salaam

Kushindwa Kuiona Vema Barabara Hasa Suala La Usalama.
Chanzo Cha Kuamini Kuna Jamaa Yangu Yupo Safari Amelala Hapo Hadi Asubuhi, Na Analazimika Kutafuta Usafiri Mwingine

Bila Shaka Kwa Eneo Hilo Magari Yatalazimika Kupitia Yanayotoka Dar es salaam
Mkata Hadi Handeni Halafu Korogwe Ili Waweze Kuendelea Na Safari Pia Wanaotoka Kilimanjaro Hivyo Hivyo

======



MAELEKEZO TOKA KWA RTO WA TANGA TAREHE 12/10/2019

Ameelekeza magari yote kutoka Chalinze. yakunje Mkata kupitia Handeni na Korogwe yapite kupitia Handeni hadi Mkata, hali ya Segere Mashine si nzuri kutokana na mvua ni hatari kwa usiku!!
IMG_20191013_093451_553.jpg

#PICHA Hapa ni katika eneo la Mandera, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo maji yamefurika na kuharibu miundombinu ya daraja. Tahadhari kwa wanaosafiri kupitia eneo hilo kuelekea Kilimanjaro, Tanga na mikoa mingine.
 
Nina safari kutoka kili to dar by kesho bora nikwae pipa tu
Ipo Njia Nyingine Ukifika Korogwe Unapitia Handeni Halafu Mkata Ndiyo Dar es salaam, Changamoto Kubwa Mvua Nyingi Sana Eneo Hilo Barabara Haionekani, Huo Usiku Imebidi Magari Yalale Hapo.
Habari Zinasema Misururu Ni Mirefu Sana Maana Usiku Wa Saa Nne Hadi Asubuhi Hii
 
Naam awamu ina baraka tele Hii
Mvua za vuli zimekuwa za msimu
Kwa Tanga mvua inamwagika sio masihara..jana tangu asubuhi mpaka usiku...Leo asubuhi hii naona nje bado anga lina dalili zote la Maji kumwagika tena.
 
Huyu waziri wa ujenzi ana taarifa kweli?? afuatilie kipindi hiki cha mvua barabara nyingi zitampa majibu,mfano hata hapo jangwani anashindwa kuvunja kituo kile akajaza kifusi aweke tunel barabara iwe juu man yapite chini, maana jangwani mvua kidogo tu hapaptiki, Cha ajabu wanahangaika kuremba jiji huku wanaacha kero.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom